Je ulikuwa unafahamu kuwa sukari ina
vimelea muhimu vya uhai? Ingawa hii haimaanishi kuwa kula vitu vitamu
kwa wingi ni kuongeza uhai. Sukari imetengenezwa kwa fomula rahisi
iliyotokana na kemikali ziitwazo carbon, hydrogen na oxygen. Kemikali
hizi ndizo zilizojenga karibu kila mwili wa kiumbe hai anayepatika hapa
duniani pamoja na kemikali nyingine ya nitrogen.
Hivyo basi timu ya wanaastronomia kwa kutumia telescope yenye nguvu wameweza kuona sukari kwenye gesi zinazopatikana
kuzunguka nyota ndogo yenye ukubwa sawa na Jua letu. Sukari ilishawahi
kuonekana angani, lakini hii ni mara ya kwanza kuonekana kwa ukaribu
katika nyota inayofanana na Jua. (Umbali uliopo kati ya sukari hii na
jua ni sawa na umbali uliopo kati ya Jua na sayari ya Uranusi). Na kwa
vile sukari ina vimelea vya maisha, kuonekana kwake karibu na nyota
inayofanana na jua ni habari nzuri sana. Kitu ambacho kinaonyesha kuwa
maisha kama yetu yanawezekana kupatikana katika sayari nyingine
ulimwenguni!
Wanaanga hawa wamegundua pia, sukari hii
huingia ndani kuelekea katika nyota. “ Sukari hii siyo tu kwamba ipo
katika sehemu sahihi ya kuweza kuingia kwenye sayari, lakini pia
inasogea kuelekea katika uelekeo sahihi” anasema mwanaastronomia Cécile
Favre.
Jihusishe: Je ni kitu
gani ungeweza kukigundua kama ungekuwa unashughulika na moja kati ya
telescope kubwa zaidi Duniani? Papo hapo ili kusheherekea miaka 50 ya
Kituo cha Anga cha Ulaya Kusini unaombwa kupiga kura juu ya kitu umbacho
ungependa kichunguzwe na telescope yake kubwa iitwayo VLT!
No comments:
Post a Comment