MENEJA MSAIDIZI wa kampuni hiyo ABDALLAH MBENA amesema wananchi wanahitaji elimu yak kutosha juu ya namna gani wanaweza kuweka mazingira yao safi na kwamba kwa kupitia kampeni hiyo wananchi wataweza kujinufaisha kiuchumi kupitia taka rejea na kuweka mazingira yao safi na salama.
Kwa upande wake MENEJA UENDESHAJI wa kampuni hiyo ELIZABETH SCHEEPERS amesema takataka zinafaida nyingi ikiwemo kutumia madafu kutengenezea mkaa ambao utawasaidia watanzania kuepukana na suala la ukataji miti ovyo
No comments:
Post a Comment