Wapiganaji wa kiisilamu
wameuteka mji uliokuwa unadhibitiwa na wanajeshi wa serikali licha ya
harakati za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao kwa usaidizi wa Ufaransa.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian
alisema kuwa mji wa Diabaly, ambao uko umbali wa kilomita 400 kutoka mji
mkuu ulitekwa katika makabiliano yaliyofanyika kati ya wapiganaji hao
na wanjeshi Jumatatu.Aliongeza kuwa wapiganaji hao waliweza kutoroka na kukimbilia Mashariki mwa nchi lakini akakiri kuwa wanjeshi wa Ufaransa wanakumbwa na wakti mgumu kukabiliana na waasi ambao ambao wamejihami vilivyo.
Awali waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius alisema kuwa harakati za jeshi la Ufaransa katika kusaidia wanajeshi wa Mali dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu hazitachukua muda mrefu sana.
Juhudi zao zitadumu tu wiki chache.
Mnamo Jumapili, Jeshi la wanahewa la Ufaransa liliimarisha mashambulio yake dhidi ya wapiganaji hao hasa kwenye miji ya Gao na Kidal.
Wizara ya Ulinzi ya ufaransa inasema mashambulizi hayo yatakamilika katika muda wa wiki kadhaa.
Jeshi la Ufaransa lmekuwa likipambana na wapiganaji hao tangu Ijumaa , wakisaidia wanajeshi wa serikali kutwa maeneo yaliyotekwa na wapiganaji hao na hata kufanikiwa kutwa mji wa Konna.
Ufaransa imeitisha mkutano na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, baadaye hii leo.
Akiwahutubia waandishi wa habari,bwana Fabius alikataa kikosi kushirikishwa kwa muda mrefu kama ilivyo nchini Afghanistan chini ya NATO.
''Baadaye tutaweza kuondoka lakini hatuna nia ya kukaa hapa kwa muda mrefu.''
Bwana Fabius alisema kuwa ikiwa Ufaransa isingeingilia mgogoro huu, kulikuwa na tisho la wazi kuwa wapiganaji hao wangeweza kuingia zaidi ndani ya Mali na hata kufika mji mkuu Bamako, huku athari kubwa zikijitokeza.
No comments:
Post a Comment