Wacheza kamali wanataka kucheza
karata zao vizuri kuhusu kinyang'anyiro cha ubingwa wa Kombe la Mataifa
ya Afrika mwaka 2013. Wacheza kamali hao wataelekeza karata yao katika
timu ya Nigeria wakiipa nafasi ya kuwa katika timu tatu bora za juu.
Timu ya Nigeria, The Super Eagles,
imeshiriki mara 16 katika mashindano ya kombe hilo na kushinda mara
mbili, ikishika nafasi ya pili mara nne na mara saba katika nafasi ya
tatu, ikiwa ni rekodi ya kujivunia katika kipindi cha miaka 50.
Kocha wa sasa Stephen 'Big Boss' Keshi, kocha asiye na mzaha ambaye alikuwa katika kikosi cha wachezaji wa Nigeria walioishinda Zambia kwa kuilaza magoli 2-1 katika fainali zilizofanyika Tunisia, miaka 19 iliyopita. Alikuwa mchezaji kiungo imara ambaye aliongoza kwa mfano na alitumia wiki chache zilizopita kufanya mazoezi katika kambi nchini Ureno akijaribu kujenga moyo wa ushindi kwa timu yake ya Super Eagles.
"Ni vizuri kuona wachezaji wakifanya jitihada kuwania namba katika kikosi changu cha kwanza. Ushindani huo unanipa changamoto nzuri. Hakuna mwenye namba ya kudumu katika timu-- ni lazima wapiganie na pia wapiganie kuhifadhi namba wanayopataKocha wa Mlinzi wa kati na nahodha wa Super Eagles, Joseph Yobo, analeta changamoto sawa katika rekodi ya mchezaji bora wa zamani wa mwaka wa Afrika Nwankwo Kanu kwa kucheza katika fainali sita za Kombe la Afrika.
"Kushinda kombe si kazi rahis lakini naahidi kutafanya kwa uwezo wetu wote kufikia lengo hilo. Nawaomba Wanaigeria kutuombea na kuwa na imani na timu hii,"anasema mchezaji huyo kiungo wa zamani wa Everton ambaye kwa sasa anacheza soka nchini Uturuki.
"Tunasafiri kwenda Afrika Kusini tayari kupeperusha bendera ya taifa letu na hatutachoka hadi tutakapotimiza lengo letu. Bahati nzuri tuna kikosi kizuri cha wakufunzi ambacho kinatufahamu vizuri na nina uhakika wachezaji wako tayari kwa hilo.
No comments:
Post a Comment