Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83. Tume ina Wajumbe 32 ikiongozwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti. Tume ina Sekretarieti inayoongozwa na Katibu na Naibu Katibu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, jukumu kuu la Tume ni kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, jukumu la Sekretarieti ni kuiwezesha Tume kufanya kazi zake.
Kuhusu Tume
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83. Jukumu kuu la Tume ni kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu kupatikana Katiba Mpya.Tume pia inatekeleza majukumu mengine yafuatayo:-
a) Kuandaa na kuendesha programu za kuelimisha umma;
b) Kuitisha na kusimamia mikutano na mabaraza ya katiba;
c) Kutathmini na kuchambua maoni ya wananchi;
d) Kupitia na kuchambua michango, mawazo, maoni, taarifa na mapendekezo yaliyokusanywa na
kufanyiwa tathmini siku za nyuma;
e) Kupitia na kutafiti usahihi na ulinganifu wa masharti ya kikatiba yanayohusu mamlaka ya wananchi,
mifumo ya kisiasa, demokrasia, utawala wa sheria na utawala bora;
f) Kumuomba mtu yeyote kufanya majadiliano na Tume au kuwasilisha nyaraka kuhusu mabadilioko ya Katiba;
g) Kuchapisha Rasimu ya Katiba katika Gazeti la Serikali na magazeti mengine ili kutoa fursa kwa wananchi kusoma
na kutoa maoni zaidi kwa Tume kupitia mabaraza ya Katiba;
h) Kutayarisha na kuwasilisha ripoti kwa kila hadidu ya rejea; na
i) Kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalum la Katiba
No comments:
Post a Comment