MWIGIZAJI
Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Yvonne Cherryl Monalisa
amewashutumu wasanii wenzake kwa kusema uongo katika jamii kuhusu maisha
yao halisi pamoja na malipo wanayopata.
Binti huyo amedai kwa kufanya hivyo wasanii wengi wemejikuta katika maisha ya kuunga unga kutokana uongo huo.
Baadhi ya wasanii wa filamu wanadanganya sana kuhusu hali halisi ya
maisha yao, mtu akipata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari kuhusu
malipo na maisha yake halisi utakuta akisema kuwa yeye bila kulipwa
milioni tano hawezi kushiriki katika filamu, lakini ukweli hakuna msanii
wa kawaida anayelipwa fedha kama hizo katika tasnia ya filamu Bongo
mimi mwenyewe ni mtayarishaji, anasema Monalisa.
Anaendelea kudai kuwa kutokana na udanganyifu huo Serikali kupitia
Bodi ya Filamu iliamua kuongeza gharama za kibali cha kurekodi filamu
hadi kufikia Shilingi 500,000 jambo lilofanya wasanii walalamike kama ni
fedha kubwa sana kulingana na malipo ya filamu, lakini ilitokana na
udanganyifu kutoka kwa baadhi ya wasanii wa filamu kudanganya, mwanadada
huyo anasema hali ya soko la filamu ni mbaya kwa sasa.
No comments:
Post a Comment