Rais Barack
Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa
hadhara mjini Iowa huku wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa
atapata muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua
usukani katika ikulu ya White House.
Mwandishi wa BBC ambaye yuko kwenye kampeini ya
Romney, anasema kuwa hizi dakika za mwisho ni kuhusu kuwashawishi
wapiga kura katika uchaguzi huu wenye ushindani mkaliKura za kwanza zimepigwa katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa Obama na Romney wamepata kura tano kila mmoja kati ya kura kumi. Kura hizi hazitokani na wapiga kura kwa ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga kura katika kile kinachojulikana kama Electoral village.
No comments:
Post a Comment