BIBLIA :
YESU AKASEMA » KWA NINI KUNIITA MWEMA ?
HAKUNA ALIYE MWEMA ILA MMOJA, NDIE MUNGU. WAZIJUA AMRI, USIUE, USIZINI, USIIBE, USISHUHUDIE UONGO, USIDANGANYE, WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO. AKAMWAMBIA, MWALIMU HAYA YOTE NIMEYASHIKA TANGU UTOTONI MWANGU. YESU AKAMKAZIA MACHO, AKAMPENDA, AKAMWAMBIA, UMEPUNGUKIWA NA NENO MOJA. NENDA , UKAUZE ULIVYO NAVYO VYOTE, UWAPE MASIKINI, NAWE UTAKUWA NA HAZINA MBINGUNI ; KISHA NJOO UNIFUATE. WALAKINI YEYE AKAKUNJA USO KWA NENO HILO, AKAENDA ZAKE KWA HUZUNI ; KWASABABU ALIKUWA NA MALI NYINGI. »
(MARKO MTAKATIFU 10 :17…..22)
YESU AMEANZA KUTUONESHA KWAMBA MWENYEZI MUNGU NDIE MWENYE UTUKUFU NA MWENYE SIFA ZAIDI YA KIUMBE CHOCHOTE. NA NDIO MAANA KAMWAMBIA TAJIRI HUYU, KWAMBA USINIITE MWEMA ALIYEKUWA MWEMA NI MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE. AMBAE UFALME WA MBINGU NA ARDHI VIMO MKONONI MWAKE.
KISHA YESU AMETUNESHA KWAMBA ILI UWE MCHA MUNGU WA KWELI UNATAKIWA USIUE (VIFO VIMEZIDI, RWANDA, KENYA, KONGO, VIFO VYA WALEMAVU WA NGOZI VIMEKUWA CHAMBO CHA MATAJIRI, SUDANI, SOMALIA, AFGHANISTAN, IRAQ, ANGOLA, PHILIPINE……….N.K.),USIZINI (WANAUME KWA WANAUME, WATOTO WA ZINAA KIBAO NA VYOMBO VYENYE KUHAMASISHA ZINAA VINAONGEZEKA KILA KUKICHA, HADI KWA SASA NYUMBA ZA WAGENI NDIO MAKAO MAKUU YA KUSALITI NDOA NA UJIRANI), USIIBE( WIZI WA MABENKI NA MAJUMBANI UMEKUWA KAMA LIGI KUU, ROBA ZIMEZIDI MTAANI HADI WATU WANAOGOPANA NA KUOGOPA KULIZA MWENYEJI NJIA KWA KUKHOFIA KUITWA MWIZI NA KUCHOMWA MOTO KATIKA JINA LA MTU MBAYA), USISHUHUDI UONGO (CHANZO CHA VITA VYA IRAQ AMBAVYO VIMEANGAMIZA MAMILIONI YA WATU MPAKA SASA NI KUWA IRAQ ILIKUWA IKIMILIKI SILAHA ZA MAANGAMIZI, LAKINI SASA TUNAAMBIWA BAADA YAKUNYONGWA ADUI, KWAMBA VIONGOZI WA NCHI ZILIZO VAMIA WALIONGEA UONGO, ILI WAPITISHE AU KUFIKIA LENGO LA MAUWAJI YA WATU WASIOKUWA NA HATIA), USIDANGANYE (KUDANGANYA KUMNEKUWA NJIA MOJAWAPO YAKUTAFUTIA RIZIKI, UTAPELI WA CHENI NA FEDHA BANDIA, UHAKIKA WA KUJUWA CHANZO NA MAANA YA UGAIDI MPAKA SASA NI KIZA KISICHO NA UKWELI WA USHAHIDI KATIKA KILA KUNDI HUSIKA KATIKA VITA VYA UGAIDI ? NA MARANYINGINE TUNASHINDWA KUJUWA TAFAUTI YA UISLAMU NA UGAIDI NI NINI ? AU AU VITA VYA WAISLAMU NA WALE WASIOKUWA WAISLAMU VILIANZA LINI NA NI NINI SABABU ?), MHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO(BAADHI YA WAZAZI WALIOWENGI WANAHANGAIKA KILA KUKICHA ILI WAWEZE KUWATULIZA WATOTO WAO KATIKA TABIA NJEMA NA MUELEKEO WA KUJIANDAA NA NDO LAKINI MWISHO WAYOTE VIJANA HUONA WAZAZI WAO NI WATU WAKUWAPOTEZEA MDA, NA MARANYINGINE WATOTO HUWAPA WAZAZI WAO MAJINA YA DINGI AU MZUSHI AU MNENE……………..WAKINA MAMA WAO HUKOSA KAULI YA KUZUIA MATOAKEO KAMA MIMBA NA WIZI).
• YOTE HAYA HUYO JAMAA TAJIRI ALIWEZA KUYAEPUKA NA KUYASHINDA, LAKINI ALISHINDWA KUFAULU, KATIKA MTIHANI WA FEDHA NA MALI.
IKIWA BAADHI YA BINAADAMU, HAWATAKI KUWA SAWA NA WATUMWA WAO AU WAFANYAKAZI WAO AU NDUGU ZAO AU MARAFIKI WAO AU JAMAAZAO, VIPI WAMFANYE MWENYEZI MUNGU SAWA NA WAJA(VIUMBE AU BINAADAMU, MAJINI NA MALAIKA) ?
HUWEZI KUFIKIA WEMA MPAKA UTOE UNACHOKIPENDA ZAIDI, KATIKA NJIA YA HALALI.
QURAN :
MWENYEZI MUNGU ANASEMA » NA MWENYEZI MUNGU AMEWAFADHILISHA BAADHI YENU KULIKO WENGINE KATIKA RIZIKI. NA WALE WALIOFADHILISHWA HAWARUDISHI (HAWAWAGAWII) RIZIKI ZAO KWA WALE ILIOWATAMALAKI MIKONO YAO YA KULIA (WATUMWA), ILI WAWE SAWA KATIKA RIZIKI HII ; (BASI VIPI NINYI MNAMFANYA MWENYEZI MUNGU SAWA NA WAJA WAKE, NA NYINYI HAMKUBALI KUWA SAWA NA WATUMWA WENU) ? BASI JE, WANAZIKATAA NEEMA ZA MWENYEZI MUNGU ? »
(16 :71)
LICHA YA WATU WENGI WENYE UWEZO WA KIFEDHA NA MALI, KUJIFANYA KWAMBA WAO NDIO WENYE KUGOMBANIA HAKI ZA BINAADAMU, NA KUTAKA USAWA WENYE MFUMO WA UADILIFU KATIKA UMILIKAJI, UTENDAJI NA MSINGI WA ELIMU KATIKA JAMII, MARANYINGINE HUSHINDWA KATIKA UTEKELEZAJI WA MATENDO NA KUSHINDA KATIKA MSINGI WA MANENO YENYE KUTA(WALL) ZA KUTIANA MOYO WA MAFANIKIO.
UTAWAKUTA WATU WENYE ELIMU NA NI MATAJIRI, WAKIJIGAMBA KWAMBA WAO NI WACHA MUNGU AU WANATETEA HAKI ZA WANYONGE AU NI WAADILIFU KATIKA MANENO YAO YA AHADI NA MATENDO YAO, LAKINI MWISHO WASIKU UDHAIFU WAO, UTAJITOKEZA AU UTAUTAMBUA KUPITIA ALAMA ZA MAPITO YAKE (JE ! ALIVYO ZUNGUMZA NDIVYO ATENDAVYO ?).
INAKUWAJE WEWE, UFIKIE CHEO CHA UTAJIRI NA KUITWA TAJIRI, PINDI AMBAPO HUJAFAURU KUARIDHISHA KIMAHITAJI WATU WAKO WA KARIBU.
BIBLIA
YESU AKAWATAZAMA WANAFUNZI WAKE, JINSI ITAKAVYOKUWA SHIDA WENYE MALI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU !
WANAFUNZI WAKASHANGAA KWA MANENO YAKE. YESU AKAJIBU TENA, AKAWAAMBIA, WATOTO, JINSI ILIVYO SHIDA WENYE KUTEGEMEA MALI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU! NI RAHISI NGAMIA KUPENYA KATIKA TUNDU YA SINDANO KULIKO TAJIRI KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU. NAO WAKASHANGAA MNO, WAKIMWAMBIA, NI NANI, BASI, AWEZAYE KUOKOKA? YESU AKAWAKAZIA MACHO AKASEMA, KWA WANADAMU HAIWEZEKANI, BALI KWA MUNGU SIVYO; MAANA YOTE YAWEZEKANA KWA MUNGU.
(MARKO MTAKATIFU 10:23………27)
KUNA WATU WENGI WENYE KUJIGAMBA KWAMBA NI MATAJIRI, LAKINI UKIANGALIA KHALI YA WAZAZI WAKE, MKE AU WAKE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI, UTASHANGAA KUHUSU MAANA YAJINA ALILOPEWA MTU HUYO. MTU ANAITWA TAJIRI ( PAPA AU PEDEJE…N.K) LAKINI ANASHINDWA KUDHAMINI CHAKULA CHA WIKI AU MWEZI AU MWAKA KATIKA KITUO FULANI CHA WATOTO YA TIMA AU KUWAPA MITAJI WAJANE AU MASIKINI, HILI NIJAMBO LAKUSHANGAZA KUHUSU UTAJIRI WENYE SIFA YA HEWA MAISHANI.
MARANYINGINE MTU ANAPEWA CHEO CHA UTAJIRI LAKINI KUMLIPA MFANYA KAZI WAKE WA NDANI MSHAHARA WENYE NAFUU YA MAISHA, ANAONA TABU SANA.
NA MARANYINGINE MTU HUSIKA HUITWA TAJIRI, LAKINI UKIANGALIA MAZINGIRA YA KULA NA KUNYWA NYUMBANI KWAKE, NIYENYE WASI WASI NA YENYE HESABU YA HALI YA JUU. UTAKUTA BABA NDIO MWENYE KURUHUSIWA KUNYWA CHAI YA MAZIWA AU KULA NYAMA MARA SABA KWA WIKI, NA WENGINE NI KUNYWA CHAI YA RANGI KATIKA MFUMO WENYE MPANGILIO WA HESABU YA VIJIKO VYA SUKARI NA MARANYINGINE HULA NYAMA KWA MAKADILIO YA VIPANDE.
MAVAZI YA MTUMBA NA UPATIKANAJI WAKE UPO KATIKA MSINGI WA MAOMBI YA HALI YA JUU, WASIWASI KATIKA KUTOA MAONI AU KUOMBA MSAADA, NA MARANYINGINE UTAMKUTA MFANYAKAZI WA NDANI AKIFANYWA WA MWISHO KULA, NA MARANYINGINE AKILISHWA CHAKULA KILICHOBAKI MEZANI. INA MAANA CHAKULA KIKIISHA MFANYA KAZI HUYO, HANA CHAKULA KWA WAKATI HUO, LICHA YA KUWA YEYE NDIE MPISHI.
MARANYINGINE MATAJIRI WA MWILI HUOGOPA KUSALIMIANA NA WATU MASIKINI, KWA KUOGOPA KUOMBWA (KUPIGWA MZINGA), NA MARANYINGINE WATU MATAJIRI HUJIJENGEA NIDHAMU YA KUOGOPWA NA WATU WENYE KHALI YA CHINI.
WATU MATAJIRI MARANYINGI HUJIJENGEA NGOME YA ULINZI KATIKA MFUMO WA DHARAU NA KIBURI, NA MSINGI WAO KATIKA UTENDAJI HUWA NA NJIA NYINGI ZA KUJIEPUSHA KUKAA KARIBU NA WATU WENYE UPUNGUFU WA PESA AU MALI.
MATAJIRI WALIO WENGI HUJIFANYA WAZURI KATIKA JAMII, PINDI WANAPOKUWA KATIKA MAZINGIRA YENYE KUONEKANA(TV NA VIKAO) NA KUSIKIKA(RADIO AU KATIKA MFUMO WA AHADI YENYE KUHITAJI NGUVU YA MASIKINI)SANA.
ASILIMIA KUBWA YA MATAJIRI, NI WATU WENYE KUOGOPA
(GHOFU)KUFIRISIKA, NA NI WENYE KUOGOPA UMASIKINI ZAIDI YA MWENYEZI MUNGU, NA NIWENYE KUOGOPA KUTOA (MALI, PESA, WAKATI AU MDA….N.K.), KUELEKEA KATIKA KAMBI YA MASIKINI NA MAFUKARA NA MAYATIMA NA WAJANE, LICHA YAKUWA NI WATU WENYE KUVAA KOFIA YENYE KIMVURI CHA UCHA MUNGU AU KUTEMBEA NA MBENDERA YA KUTETE HAKI ZA BINAADAMU.
MFANO HAI NI HUU WA SIERRA LEONE:
SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KUTETEA HAKI ZA BINAADAMU LA AMNESTY INTERNATIONAL, 23.09.09 LILISEMA MWANAMKE MMOJA KATI YA WANANE NCHINI SIERRA LEONE YUKO KATIKA HATARI YA KUFA WAKATI WA KUJIFUNGUA. HALI HII INAIFANYA SIERRA LEONE KUWA MOJA YA NCHI ZENYE KIWANGO KIKUBWA CHA VIFO VYA KINA MAMA WAJAWAZITO DUNIANI.
AMNESTY INTERNATIONAL ILISEMA MAELFU YA WANAWAKE NCHINI HUMO WANAPOTEZA DAMU NYINGI BAADA YA KUJIFUNGUA KWA SABABU HAWAWEZI KUGHARAMIA MATIBABU KUTOKANA NA UMASIKINI.
MKUU WA SHIRIKA HILO, IRENE KHAN, ALIISHUTUMU SERIKALI NA FAMILIA ZA WANAWAKE HAO KWA KUPUUZIA HALI HIYO.
IKIWA MANABII WA MWENYEZI MUNGU WALISEMA UONGO, KUHUSU UBAKHIRI WA MATAJIRI, BASI KWELI MATAJIRI WENGI WATAINGIA PEPONI.
NA IKIWA MANABII WA MWENYEZI MUNGU WANASEMA UKWELI, MOJA WAPO AKIWA NI YESU (NABII ISA KWA WAISLAMU), BASI KUNDI KUBWA LA MATAJIRI LITAANGAMIA SANA SIKU YAKIAMA (SIKU YENYE KUBEBA MALIPO YA KILA KIUMBE NA KUMALIZA UHAI AU MAISHA YA KILA KIUMBE HAI, HAPA DUNIANI).
UBAGUZI WA SALAMU BAINA YA MATAJIRI NA MASIKINI
SIKU ZOTE BAADHI YA MATAJIRI, WANATUMIA KURA YA MAISHA KATIKA MSINGI WENYE MAMLAKA YA PESA NA MALI, ZAIDI KULIKO KUTUMIA MFUMO NA ASILI YA MWANADAMU WA KAWAIDA.
MAMLAKA YA PESA NA MALI INAMFANYA MTU MWENYE MALI, AMUONE YULE MWENYE UPUNGUFU WA MALI NA PESA, KAMA MTU DHAIFU, HATAKAMA MDHARAULIWA (MASIKINI), ANA ELIMU NZURI AU UMRI MKUBWA ZAIDI YAKE(TAJIRI). MAMLAKA HAYO YA PESA NA MALI, YANAMFANYA TAJIRI KUHISI KWAMBA, HANA UPINZANI KATIKA MAONGEZI NA MATENDO.
KWA NJIA HII, THAMANI YA UKUBWA KATIKA NJIA YA UMRI, IMEKUWA DHAIFU NA INAPOTEA KABISA, KWASABABU, MZEE ANAMWITA MTOTO MDOGO BWANA MKUBWA, BABA, MHESHIMIWA, SIFA ZOTE HIZO HUWA NA MSINGI WA KUOMBA KATIKA UNYENYEKEVU WA HALI YA JUU. NA NJIA HII, YA WATOTO KUMILIKI PESA NA KUTOA KATIKA MFUMO WA SIFA, IMEWEZA AU KUFAULU KUVUNJA HESHIMA AU KUSHUSHA HADHI YA NAFSI YA BINAADAMU MWENYE UMRI NA HAKI WA KUHESHIMIWA NA YULE MWENYE UMRI MDOGO, BILA KUJALI MALI NA PESA.
NA ANAPOJITOKEZA MASIKINI KUPINGA MANENO YAKE(TAJIRI) AU VITENDO, HUPEWA (MASIKINI) ADHABU YA KUNYIMWA MSAADA AU KUTAFUTIWA SABABU YA KIFUNGO AU ADHABU NYINGINE YA KUMTIA ADABU (MTU MWENYE UPUNGUFU WA MALI NA PESA LAKINI ANAMKOSOA MTU AMBAE NI TAJIRI WA MALI NA PESA).AU MASIKINI AKINUSURIKA NA ADHABU HIZO, ATAPEWA JINA LA MASIKINI TAJIRI, AMBALO MAANA YAKE NI KUWA NA UTAJIRI NAFSINI
(UTAJIRI WA UADILIFU KATIKA MSINGI WA HAKI) NA KUWA MASIKINI WA MALI NA PESA.
MARANYINGINE, MATAJIRI HAWAPENDI KUWAPA WATU MASIKINI MKONO KATIKA MSINGI WA SALAMU, MATAJIRI HUOGOPA MARADHI KUTOKA KWENYE MIKONO YA WATU MASIKINI NA MAFUKARA NA MARANYINGINE, HUONA(MATAJIRI) KUPEANA MKONO NA MASIKINI, NI KUJISHUSHIA HADHI MBELE YA KUNDI LA MATAJIRI WENZAKE.
MARANYINGINE BAADHI YA WATU MATAJIRI HAWAPENDI KUWAKARIBISHA WATU MASIKINI, KATIKA NYUMBA ZAO AU SEHEMU YA KUKAA ( BARAZANI AU SEATING ROOM) KWASABABU, HUWA(MATAJIRI) NA DHANA YA KWAMBA MTU HUYO MASIKINI, ATAPUNGUZA THAMANI YA BARAZA KWA KUCHAFUA VITI AU KAPETI, AU MARANYINGINE BAADHI YA WATU WENYE UWEZO WANASHINDWA KUWAKARIBISHA WATU MASIKINI BARAZANI MWAO KWA KUGHOFIA KWAMBA MATAJIRI WENZAO WATAWAONA KWAMBA WAO NI MARAFIKI WA WATU WENYE KHALI YA CHINI KIUCHIMI AU KUSHINDWA KUWA KARIBISHA NDANI KWA SABABU BARAZANI MNA WAGENI MATAJIRI AU WATU FULANI MAARUFU.
YOTE HAYO NI MAPAMBANO AMBAYO MASIKINI WANAKABILIANA NAYO KATIKA MSINGI WA KUSAKA RIZIKI. NA NDIO MAANA MAKAO YA MASIKINI, HUITWA USWAHILINI AU USWAZI (YANI SEHEMU YENYE HADHI YA CHINI KATIKA KILA JAMBO)
MARANYINGINE NYUMBA ZA WATU MATAJIRI, ZINA VIKOMBE VYAKUNYWEA WATU WENYE GHADHI YA CHINI NA VIKOMBE NA MASAHANI VYA KUTUMIWA NA WATU WENYE GHADHI YA JUU.
NA MARANYINGINE WATU MATAJIRI WANA TABIA YA KUPEANA TAARIFA ZA SHEREHE KATIKA MSINGI WA UMWINYI NA KUPANGIANA KIASI KIKUBWA CHA MCHANGO. MARANYINGINE MASIKINI MWENYE KUJIPENDEKEZA ILI APEWE KADI YA HARUSI, INAMLAZIMU ACHANGIE HARUSI HUSIKA, KATIKA MFUMO WA KIASI KILICHOPANGIWA WATU WOTE, BILA KUJALI MASIKINI NA TAJIRI.
MCHANGO WA HARUSI HUSIKA UNAWEZA UKAWA KIASI FULANI CHA MTAJI WA MASIKINI.
YOTE HAYO YAMETUZUNGUUKA NA KILA MMOJA ANAUWEZO WA KUYASHUHUDIA AU KUYASIKA KWA WATU AU KWENYE VYOMBO VYA HABARI.
NDIO MAANA TUNAWASIKIA WAHENGA WAKISEMA HIVI « MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE »
JE ! IKIWA YOTE HAYO, YANATENDWA NA BAADHI YA BINADAMU KUWATENDEA BINADAMU WENZAO.
ITAKUWAJE WATU WAMFANANISHE MTU FULANI AU KIUMBE FULANI NA MWENYEZI MUNGU. MUNGU HANA TABIA YA DHULMA, DHARAU, CHUKI, LAWAMA……JUU YA VIUMBE WAKE. KWASABABU KILA JAMBO MAISHANI LIMEUMBWA KWA REHEMA NA UWEZO WAKE.
UTAKUTA KATIKA WAPINGAJI UBAGUZI WARANGI NA KIKABILA, WAMO MATAJIRI, LAKINI WENGI WETU NI WANAFIKI WENYE MSINGI WA KUHITAJI SIFA KATIKA JAMII. KUNA NDUGU ZETU WENYE ULEMAVU WA NGOZI(ALBINO), KWA SASA WANAWINDWA KAMA SWALA PORINI, JE NINANI WA KUWATETEA KATIKA MSINGI WA AMANI ?
NI MASIKINI WENZAO AU NIMATAJIRI WENYE KUHITAJI NYONGEZA YA MALI NA PESA KATIKA HARAKATI YAO YA KUNUNUA VIUNGO VYA BINAADAMU WENZAO KWA GHARAMA YA JUU KABISA.
KWASASA HATA WACHUNGAJI WAMEANZA KUINGIA KATIKA BIASHARA YA VIUNGO VYA BINADAMU. JE ! WATU WENYE ULEMAVU WATAWEZA KUMTAMBUA MUNGU NA KUHESHIMU AMRI ZAKE, KATIKA KHALI YA KUSAKWA NA WAKUU WAO WA IMANI ?
INAKUWAJE BABA AWEZE KUMUANGAMIZA MKE WAKE AU MWANAE KATIKA JINA LA KUSAKA MOTO WA UTAJIRI WA DUNIA HII ?
MFANO HAI WA MAUAJI YA ALBINO NI HUU :
WATATU KUNYONGWA KWA MAUAJI YA ALBINO ????!!!!!
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, LEO 23.09.09 IMEWAHUKUMU WATUHUMIWA WATATU WA NAUAJI YA ALBINO KUNYONGWA HADI KUFA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KUMUUA MTOTO MATATIZO DUNIA MWENYE UMRI WA MIAKA (13). WALIHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA NA MAHAKAMA HIYO MJINI KAHAMA, MKOANI SHINYANGA NI MASUMBUKO MATATA (32), MKAZI WA ITUNGA, EMANUEL MASANGWA (28), MKAZI WA BUNYIHUNA NA CHARLES KALAMUJI AU CHALES MASANGWA (42) MKAZI WA KIJIJI CHA NANDA WILAYANI BUKOMBE. WOTE WALIPATIKANA NA KOSA LA MAUAJI KINYUME CHA SHERIA YA JINAI YA MAKOSA NAMBA 196 SURA YA 16 ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO YA MWAKA 2002.
YOTE HAYO NI MABADILIKO YA KUMUACHA MUNGU KATIKA JINA LA UTANDAWAZI NA UKUTA WENYE MLANGO AMBAO UNA ALAMA ISEMAYO KWAMBA « YA MUNGU YALIISHAPITWA NA WAKATI. »
KWA UPANDE WA MATAJIRI WENYE KUMJUA MUNGU, WAO HUWA NA TABIA MBILI, AMBAZO NI KUTUMIA MFUMO WA ASILI. KUMJALI NA KUMHESHIMU MTU YOYOTE BILA KUJALI MALI, PESA, UMRI…………KATIKA MFUMO WA UADILIFU. NA HUWASAIDIA MASIKINI, MAYATIMA, MAFUKARA, WATUMWA……………..NA HUTOA ZAKA NA SADAKA KWA WAKATI WAKE. NA KATIKA MARAFIKIZAO UTAKUTA MNA MCHANGANYIKO WA MASIKINI NA MATAJIRI, WEUPE NA WEUSI AU WAFUPI NA WANENE AU WEMBAMBA NA WANENE. NA HAO MATAJIRI WENYE TABIA NJEMA KAMA HIZI, NDIO WATAKAORITHI UFALME WA MBINGU, NA MALIZAO ZITALINDWA DUNIANI NA WATAPATA MALIPO YA PEPO SIKU YA KIAMA. INSHALLAH (MUNGU AKIPENDA)
MTAYARISHAJI NI: ISMAIL MUSSA
No comments:
Post a Comment