NJOMBE

NJOMBE

Thursday, August 23, 2012

Mzozo wa Mali kutatuliwa kijeshi mazungumzo yasipofaulu

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ameonya kuwa hapatakuwa na chaguo jingine ila kuingilia kijeshi mzozo uliopo nchini Mali iwapo hakutakuwa na mwafaka na makundi ya kiislamu yaliyojihami.
Wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Ansar Dine Kaskazini mwa Mali

Makundi hayo yanayothibiti eneo la kaskazini mwa Mali.
Akizungumza katika ziara yake nchini Senegal, rais huyo amesema kuwa wanajeshi 3000 kutoka Jumuiya ya mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS, watatumwa nchini humo lakini azimio la Umoja wa Mataifa pamoja na msaada utahitajika.
Alisema kuwa wajumbe watatumwa Bamako kukutana na serikali mpya kufuatia malalamishi kwamba maeneo mbali mbali ya Mali hayajawakilishwa kwenye serikali.
Kulingana na Rais Jonathan, hilo litakapoafikiwa, basi watakuwa radhi kuzungumzia mzozo wa Kaskazini mwa nchi hiyo.
Alisema mzozo wa Mali unapaswa kusuluhishwa kwa mazungumzo, lakini iwapo hayatafaulu basi hakutakuwa na budi ila kutumia nguvu za kijeshi, "njia za kidiplomasia na mashauriano ndio zitakazopowa kipaumbele. Na iwapo mashauriano hayatafaulu, basi tutatumia jeshi kusuluhisha mzozo huu. Jumuiya ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, itatumia majeshi kuingilia kati kwenye mzozo huu lakini hata kabla ya kufanyika hivyo lazima Umoja wa Mataifa ikubali kwa sababu tuko chini ya sheria sawa na mikataba sawa.''
Rais Jonathan alikiri kuwa mataifa ya Magharibi mwa Afrika pekee hayawezi kuingilia kati mzozo wa Kaskazini mwa Mali.
Ecowas inasema kuna kikosi cha wanajeshi 3000 ambacho kiko tayari kupelekwa Mali.
Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, majeshi hayo bado hayajakusanywa na mradi wapate msaada wa kifedha kutoka kwa mataifa ya Magharibi kabla ya kuelekea Mali.
Mali kwa upande wake imepinga mzozo huo kuingiliwa na mataifa ya kigeni huku ikishikilia kuwa jeshi yake ikipata msaada wa kifedha itaweza kukabiliana na mzozo huo.

Mwili wa Zenawi umewasili Adis Ababa

Mwili wa Zenawi ukiwasili Adis Ababa
Mwili wa Zenawi ukiwasili Adis Ababa
Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Melez Zenawi, uliwasili jana usiku katika mji mkuu wa nchi hiyo Adis Ababa na kwa sasa umehifadhiwa katika Ikulu hadi mazishi yake yatakapofanyika.
Maelfu ya raia wa nchi hiyo walimiminika katika barabara za mji huo jana jioni wakati mwili wake ulipowasili kutoka mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.
Meles, ambaye alikuwa na umri wa miaka 57, aliaga dunia ghafla kutokana na maambukizi wakati alipokuwa akitibiwa.
Kifo cha Bwana Zenawi kimezua hofu ya kugombea madaraka hali ambayo ingeweza kuathiri amani ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn ataliongoza taifa hilo hadi mwaka 2015 wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Utawala wa Bwana Zenawi ulishutumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuna hofu kuwa Waziri Mkuu mpya huenda asiwe na uzoevu wa kushughulikia na kutatua uhasama wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
Zenawi amesifika kwa kuiongoza Ethiopia kufikia mafanikio makubwa ya maendeleo na uchumi, lakini wakosoaji wake wanasema licha ya hayo yote utawala wake haukuruhusu uhuru wa siasa za vyama vingi na kuwa viwango vya ukiukwaji wa haki za binadam bado viko juu.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia madarakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.

Wednesday, August 22, 2012

Kifo cha Zenawi amani kuendelea Ethiopia

Meles Zenawi
Meles Zenawi
Serikali ya Ethiopia imesisitiza kuwa nchi hiyo ni tulivu licha ya kifo cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo Meles Zenawi aliyekuwa na umri wa miaka 57.
Zenawi alifariki katika hosipitali katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, siku ya Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwili wake unasafirishwa kuelekea mako makuu ya Ethiopia Addis Ababa, na kipindi cha maombolezo ya kitaifa kimetangazwa nchini humo.
Vyombo vya serikali vimeripoti kuwa Makamu Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn ndiye atakayeshika madaraka hadi wakati wa uchaguzi mwaka 2015.
Kifo cha Bwana Zenawi kimezua hofu ya kugombania madaraka ambayo ingeweza kuathiri amani ya nchi hiyo.
Ellen Johnson Sirleaf rais wa Liberia amemsifu Bwana Zenawi kuwa alikuwa kiongozi mahiri wa kurekebisha uchumi na pia kiongozi msomi na imara mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika.
Naye waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga awali aliiambia BBC kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles Zenawi kutokana na vita vya kikabila kuendelea kuwa tishio.
Licha ya kuwa kama mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, lakini utawala wake ulikumbwa na utata barani humo.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa kabla ya kifo chake ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu alichokuwa akiugua hasa.
Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa akipokea matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa hospitalini. Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo, alifariki siku ya Jumatatu usiku majira ya saa tano na nusu usiku.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.

''Kaa kando'' Todd Akins aambiwa

Mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican , Mitt Romney, amemtaka mwanasiasa mwenzake wa chama hicho kujiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa kiti cha Useneta baada ya kutoa matamshi yaliyozua utata kuhusu ubakaji.
Mwanasiasa wa bunge la Congress, Todd Akin
Todd Akin, ambaye ni mwanasiasa wa bunge la Congress alizua manung'uniko kwa kudai kuwa mwili wa mwanamke una uwezo wa kuzuia mimba katika baadhi ya matukio ya ubakaji.
Matamshi ya Todd Kin anayegombea kiti cha seneta nchini Marekani yalitolewa wakati wa mahojiano. Alikuwa akitetea msimamo wake dhidi ya utoaji mimba.
Alipoulizwa kuhusu kutoa mimba iwapo mwanamke atabakwa, Todd Kin alieleza kuwa katika ubakaji halali au kile alichokitaja kuwa 'legitimate rape' kuna uwezekano kwamba kibiolioia, mwili wa mwanamke utamzuia kupata mimba anapobakwa.
Matamshi yake yamezua hisia kali.
Mpinzani wake Mitt Romney amesema, ''Matamshi yake kuhusu ubakaji yanaudhi sana na siwezi nikatetea msimao wake au nikamtetea yeye''
Baadhi ya wenzake Todd Akin kutoka chama cha Republican wamemtaka kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha useneta.
Hiki ni kipindi kigumu kwa wana Republican ambao walikuwa wamejiandaa kuendeleza kampeni yao kwa kumshambulia rais Obama kwa jinsi uchumi ulivyozorota wakati wa uongozi wake. Badala yake sasa wamejikuta wakirushiana maneno kuhusu sera za kijamii.
Chama cha Democrats kimechukua fursa hiyo kushambulia Republicans kwa kuwataja kama watu ambao hawazingatii maslahi na hisia za wanawake.
Todd Akin ameomba msamaha kufuatia matamshi yake.
"Nilitumia maneno yasiofaa na ninaomba msamaha. Nina watoto wawili wa kike na nataka haki kutendeka, nina roho ya huruma kwa waathiriwa wa ubakaji na nawaombea. Ukweli ni kuwa, mtu anaweza akapata mimba kutokana na ubakaji. Ukweli ni kwamba, kuna waathiriwa wengi wa ubakaji. Makosa yangu ni kutumia maneno yasiofaa. Naomba msamaha wako. ''
Hata hivyo halitakuwa jambo la kushangaza iwapo atalazimika kujiondoa kwenye mbio za kuwania kiti cha useneta kwa sababu ya matamshi hayo.

Rais wa Liberia amsimamisha kazi mwanae


Ellen Johnson Sirleaf anashutumiwa kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu
Ellen Johnson Sirleaf anashutumiwa kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, amemsimamisha kazi mmoja wa watoto wake wa kiume kutoka ngazi ya unaibu gavana wa benki kuu ya nchi hiyo kwa kushindwa kuorodhesha mali zake katika tume ya kuzuia rushwa nchini humo.
Charles Sirleaf, ni miongoni mwa maafisa 46 waliosimamishwa kazi kwa kosa hilo.
Ni mmoja wa watoto wake watatu wa kiume aliowateua kushika vyeo vya juu kabisa baada ya kushinda muhula wa pili wa uchaguzi mwaka jana.
Wapinzani wa Bi Sirleaf wanamshutumu kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu.
Rais huyo amemteua mtoto wake wa kiume Fumba kuwa mkuu idara ya usalama wa taifa, na kijana mwingine Robert kuwa mshauri mkuu na mwenyekiti wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali-NOCAL.

Utawala bora

Robert Sirleaf anayashitaki magazeti mawili nchini humo ya Independent na Analyst, na mwanasiasa wa upinzani Jefferson Kogie kwa kumkashifu kuwa amejinufaisha kifedha kutokana na vyeo alivyopewa.
Taarifa kutoka ofisi ya Bi Sirleaf imesema Charles Sirleaf na maafisa wengine 45 wataendelea kuwa wamesimamishwa kazi hadi hapo watakapoorodhesha mali zao kwa Tume ya Kuzuia Rushwa.
Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na mkuu wa itifaki ya rais, David Anderson, Wakili mkuu na naibu waziri wa sheria Micah Wilkins Wright na naibu mkurugenzi mkuu wa utangazaji Ledgerhood Rennie.
Liberia
Liberia
Bi Sirleaf aliyeingia madarakani mwaka 2005 mwishoni mwa mgogoro wa vita Uliodumu miaka 14, amekuwa akiahidi mara kwa mara kupambana na rushwa na kustawisha utawala bora nchini Liberia.
Alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka jana, muda mfupi baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine katika uchaguzi ulioghubikwa na tuhuma za udanganyifu katika zoezi la upigaji kura.
Rushwa bado inabakia kuwa kikwazo kikubwa nchini Liberia huku idadi kubwa ya watu wakiishi katika umasikini licha ya utajiri mkubwa wa madini nchini humo.
Mwezi Juni taasisi ya kimataifa ya Maafa-ICG, ilitoa ripoti kutahadharisha kuwa rushwa na upendeleo wa kindugu katika sekta mbalimbali vinaweza kuhatarisha demokrasia nchini humo.

Tuesday, August 21, 2012

Kazi yakoma mgodi wa Lonmin


Wafanyikazi wa Lonmin
Wachimba migodi waliofika kazini lakini pasipo kufanya kazi
Wafanyikazi wa migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurudi mmoja mmoja katika migodi ya dhahabu nyeupe, platinum, ambako polisi waliwafyatulia risasi wenzao na kusababisha vifo vya watu 34 Alhamisi iliyopita.
Hata hivyo idadi ya wachimba migodi hao haijatosha kiasi cha shughuli za uchimbaji migodi kuendelea kikamilifu.
Kampuni ya Lonmin ilitangaza kwamba imeanza tena shughuli zake, lakini ukweli ni kwamba ni chini ya theluthi moja tu ya wafanyakazi waliofika katika migodi, na kazi haijaanza.
Kampuni pia ilitangaza kwamba imetenga muda wa wafanyakazi wote kurudi kazini, na kuongezea muda huo hadi Jumanne.
Imetisha kwamba watakaoshindwa kufanya hivyo, basi watafutwa kazi.
Rais Jacob Zuma alitangaza wiki nzima ya maombolezi kufuatia vifo hivyo vya wachimba migodi.
Vile vile alitaka uchunguzi kamili kufanyika.

Mbowe asema Tuchagueni ila kwa mashariti

Mbowe: Tupeni madaraka kwa masharti
 
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka Watanzania kukiweka kando Chama cha Mapinduzi (CCM) na badala yake wakichague CHADEMA kwa masharti kwamba kikishindwa kusimamia masilahi yao nacho kiondolewe.
Alisema ni makosa makubwa kwa wananchi kufikiria kuwa CCM ndicho baba na mama yao, hivyo kuwataka wakinyime kura katika chaguzi mbalimbali kwa kuwa kimeshindwa kuwaondolea kero zao.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, alitoa kauli hiyo juzi jioni katika Kata ya Hembeti, jimboni Mvomero, mkoani Morogoro, alipozuiliwa kwa muda na wananchi wakitaka awahutubie.
Alisema kuwa kwa sasa wananchi wanapaswa kuachana na CCM badala yake wakichague CHADEMA lakini akaweka bayana kuwa endapo nacho kitashindwa kusimamia masilahi yao, kiwekwe pembeni.
“Mimi Mbowe leo nikiona CHADEMA haiendani na mahitaji ya wananchi na kushindwa kuongoza, sitakuwa na sababu ya kuendelea kuwa mwana-CHADEMA, sasa ninyi mnang’anga’nia CCM kwa nini?” alihoji huku akishangiliwa na wakazi hao.
Mbowe alipita eneo hilo akitokea mjini Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge, akielekea Kata ya Mtibwa mkoani humo, kuungana na viongozi wenzake katika operesheni  ya vuguvugu la mabadiliko ( M4C) ndipo akazuiliwa kwa muda katika Kata ya Hembeti ambako kulikuwa na mkutano wa chama hicho.
Mkutano huo ambao ulikuwa ukihutubiwa na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Hamad Yusuph, ulisimama kwa muda huku wananchi wakizuia gari la Mbowe lisiendelee na safari wakitaka awahutubie.
Hali hiyo ilimlazimu kada wa chama hicho, Arcado Ntagazwa, aliyekuwa akihutubia kumpa kipaza sauti Mbowe kwa ajili ya kusalimia umati huo.
Akihutubia mkutano huo, Mbowe alisema kuwa dhamira ya CHADEMA kuwapo mkoani Morogoro ni kuwaondoa wananachi wa mkoa huo katika wimbi la usingizi wa kuishabikia serikali ya CCM aliyodai imeshindwa kutatua matatizo ya msingi ya nchi.
“Tunapita kila kata ya Mkoa wa Morogoro kujenga mtandao wa chama bila kujali dini, kabila wala rangi, ujumbe wangu kwa wana-Hembeti ni kujua wajibu wa chama cha siasa ni kupata viongozi na sera mbadala zitakazowezesha nchi kusonga mbele,” alisema Mbowe.
Mbowe aliongeza kuwa serikali ya CCM imeshindwa kuwatoa watu katika  matatizo na kuwapeleka katika neema huku akiwataka wakazi hao kutafakari miaka 50 ya Uhuru imewafikisha wapi.
Alisema kuwa Mkoa wa Morogoro umefunga ndoa na CCM, hali inayowafanya wasiwe na sauti ya moja kwa moja hadi matatizo yao yaongelewe na wabunge wa vyama vya upinzani kutoka maeneo mengine.
“Tunawaunganisha wana CCM,  CUF na vyama vingine na wengine katika kuikomboa Tanzania, tunawaomba msiwacheleweshe wakazi wa mikoa mingine katika kusonga mbele kwa kuwa ninyi  mmefunga ndoa na Chama cha Mapinduzi,” aliongeza.
Naye Ntagazwa, akihutubia katika vijiji vya Kambala, Hembeti na Mkindo kunakokaliwa na jamii ya wafugaji na wakulima, alisema migogoro ya ardhi nchini inakuzwa kwa makusudi na watawala kwa vile wana masilahi nayo.
Alisema watendaji na watawala wa serikali ya CCM badala ya kuwakutanisha wakulima na wafugaji kwa ajili ya kuondoa tofauti zao wao hutumia fursa hiyo kuchukua fedha kwa mmoja wao na kisha kuacha uhasama miongoni mwa wafugaji na wakulima.
“Msidhani matatizo yenu yanashindwa kutatuliwa ila huo ni mradi wa watu kwa maana leo ng’ombe wa mfugaji akiingia katika shamba la mkulima na akapelekwa kwa mtendaji kwa ajili ya kulipwa fidia, mtendaji anachukua fedha kwa mfugaji na mkulima, hali inayomfanya mfugaji aendelee kuwa na kiburi cha fedha na mkulima awe na uchungu wa kuharibiwa mali yake,” alisema Ntagazwa

Bunge la Somalia lakutana Mogadishu

Wabunge wa Somalia
Wabunge wa Somalia
Bunge la kwanza la Somalia lililochaguliwa ndani ya nchi hiyo limeapishwa rasmi katika mji mkuu Mogadishu na kuashiria kumalizika kwa muda wa serikali ya mpito iliyodumu kwa muda wa miaka minane iliyopita.
Wabunge hao wamefanya kikao chao cha kwanza katika uwanja mkuu wa ndege, moja ya maeneo yenye ulinzi mkubwa mjini humo.
Jukumu kuu la wabunge hao sasa ni kumchagua rais mya wa nchi hiyo na shughuli hiyo inatarajiwa kukamilika katika muda wa wiki mbili zijazo.
Rais anayeondoka ambaye ni Muislamu mwenye siasa za wastani, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, amekuwa madarakani tangu mwaka wa 2009 na anatarajiwa na wengi kuibuka mshindi.
Wagombeaji wengine wanaopigiwa kumpa rais wa sasa upinzani mkali, ni pamoja na waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali na aliyekuwa spika wa bunge la nchi hiyo Sharif Hassan Sheikg Aden.
Zoezi hilo ni muhimu katika historia ya taifa hilo na hasa tangu kupinduliwa kwa serikali ya Siad Bare mwaka wa 1991.
Tangu wakati huo Somalia imekuwa chini ya wababe wa kivita, wanamgambo wa Kiislamu na serikali za nchi jirani zimekuwa zikishughulikia masuala ya taifa hilo.
Kwa ushirikiano na usaidizi wa wanajeshi wa Muungano wa Afrika, serikali ya mpito ya Somalia imefanikiwa kudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, lakini kundi la wapiganaji wa Al Shabaab, ambalo lilijiunga na kundi la Al Qaeda bado linadhibiti maeneo kadhaa ya kati na kusini mwa nchi hiyo.
Wabunge hao wapya walifanya kikao chao cha kwanza leo asubuhi, katika uwanja wa ndege ambao kwa sasa unalindwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika.
Bunge hilo wawakilishi litakuwa na wabunge 275 ili hali bunge la Senate litaluwa na takriban wabunge 54.
Kufikia sasa jumla ya wabunge 211 wameapishwa idadi ambayo inazidi idadi inayohitajika kwa bunge kukutana na kufanya vikao vyake.

Gu Kailai ahukumiwa kifo Uchina

Gu mke wa Bo Xilai, mwanasiasa wa Uchina
Mke wa mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa nchini Uchina Bo Xilai amepatiwa hukumu ya kifo ambayo badala yake atatumikia kifungo gerezani kwa mauaji ya mfanyabiashara wa Uingereza Neil Heywood.
Gu Kailai hakupinga mashitaka dhidi yake katika kesi hiyo iliyochukua siku moja ya kumuua kwa kutumia sumu Bwana Heywood mwezi Novemba mwaka 2011.
Hukumu za kifo mara nyingi huwa ni kifungo cha maisha nchini Uchina.
Bwana Bo, kiongozi mkuu wa zamani wa chama mjini Chongqing, alikuwa akitegemewa kugombea nafasi ya uongozi wa juu kabisa baadaye mwaka huu.
Lakini hajaonekana hadharani tokea kuanza kwa uchunguzi dhidi ya mkewe Gu kutangazwa kuanza.
Msaidizi wa Gu, Zhang Xiaojun, alihukumiwa kifungo cha miaka tisa kwa ushiriki wake katika mauaji hayo.

Heshima ya kipekee

Hukumu hii kwa mtu mashuhuri kuwahi kutokea kwa miaka mingi nchini Uchina, imetolewa siku ya Jumatatu huku kukiwa na ulinzi mkali mahakamani.
Vyombo vya habari nchini Uchina vimeripoti kuwa, wakati wa kesi hiyo tarehe tisa Agosti, Gu alikiri kuwa alimlisha sumu Neil Heywood katika chumba cha hotel mjini Chongqing, akisaidiwa na msaidizi wake.
Alisema alikuwa akiathiriwa na matatizo ya kisaikolojia na kwamba Bwana Heywood alimtishia kijana wake wa kiume katika mvutano wa kibiashara kuhusu nyumba. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.
Picha zilizoonyeshwa kupitia televisheni ya taifa ya Uchina zimemuonyesha Gu akiitikia hukumu hiyo. ''Hukumu hii ni haki. Inaonyesha heshima maalum kwa sheria, uhalisia na uhai,'' ameongeza.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo kusomwa, msemaji wa mahakama Tang Yigan amesema mahakama inaamini Bwana Heywood alimtishia mtoto wa Gu lakini hakutekeleza vitisho hivyo. Imegundua pia Gu alikuwa akiathiriwa na matatizo ya kisaikolojia'', alisema.
Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema Uingereza iliweka bayana kwa Beijing kuwa kesi hiyo ni lazima ichunguzwe ipasavyo, lakini matokeo yalikuwa ni ''juu ya mamlaka za Uchina".
Ulinzi mkali wakati wa kesi hiyo ya Gu Kailai
Mwanasheria wa familia ya Heywood amesema wanaheshimu uamuzi wa mahakama.
Hukumu ya kifo iliyoahirishwa kwa muda wa miaka miwili inamaanisha kuwa, iwapo Gu hatafanya kosa la jinai akiwa gerezani, hukumu yake itaanza baada ya miaka miwili kutumikia kifungo cha maisha, na inaweza kupunguzwa zaidi iwapo ataonyesha tabia nzuri. Mtaalamu wa masuala ya sheria Profesa Donald Clarke anaandika katika blogu yake.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Uchina walianza kutoa maoni yao mara moja kuhusu hukumu hiyo kupitia mitandao kijamii hususani ule wa Twitter.
Wengi wameonyesha kutoridhika wakisema kuwa wauaji wengi nchini Uchina hunyongwa wakilinganisha na kesi hii ya Gu. Wengine wametoa wasiwasi wao kuwa Gu huenda akaachiliwa kwa kutumia kipengele cha msamaha kwa misingi ya kiafya.

Mabadiliko ya uongozi

Katika siku tofauti ya kesi hiyo mnamo tarehe 10 Agosti, maafisa wa ngazi ya juu wa polisi mjini Chongqing walikiri mashitaka ya kuficha ushahidi dhidi ya kesi ya Gu. Afisa wa mahakama amesema walipewa hukumu ya kifungo cha kati ya miaka mitano na kumi na moja gerezani. Shirika la habari la AFP limeripoti.
Chanzo cha kifo cha Bwana Heywood awali kilirekodiwa kuwa ni shinikizo la moyo.
Kesi hiyo ilikuja hadharani baada ya makamu wa Bo Xilai, mkuu wa polisi Wang Lijun, alipokimbilia ubalozi wa Marekani mwezi Februari akiwa na vielelezo vinavyohusiana na kesi ya Gu.
Hajawahi kuonekana hadharani toka wakati huo na vyombo vya habari vya serikali vinasema nafanyiwa uchunguzi.
Haijulikani ni kwanamna gani chama cha kikomunisti kinapanga kushughulika na Bwana Bo, anayeonekana mwenye ushawishi mkubwa.
Wachambuzi wengi wanatarajia kuona akipandishwa cheo katika kamati maalum ya watu tisa baadaye mwaka huu.
Wajumbe saba wa kamati hiyo wanatarajiwa kustaafu kukiwa na kizazi kipya cha viongozi wanaotarajiwa kuchukua nafasi zao katika mkutano wa chama hicho baadaye mwaka huu.
Bwana Bo amevuliwa vyeo vyake vya uongozi akiwa nachunguzwa kwa utovu wa nidhamu,'' vyombo vya habari vya serikali vinasema.
Kufichuliwa kwa kesi ya Gu Kailai's katika uhalifu huo kumesambaratisha nyota ya mumewe Bo Xilai katika siasa na kusababisha mgawanyiko mkubwa katika chama cha Kikomunisti wakati kikijiandaa kubadili uongozi.

Monday, August 20, 2012

Zuma atangaza maombolezo Afrika Kusini

Baadhi ya miili ya wachimba migodi waliouawa na polisi Afrika Kusini
Baadhi ya miili ya wachimba migodi waliouawa na polisi Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kipindi cha maombolezo nchini humo kufuatia mauaji ya wachimba madini thelathini na wanne yaliyofanywa na polisi,
wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi.
Bwana Zuma pia ametaka tume ya uchunguzi ya kisheria ichunguze mauaji hayo katika mgodi wa madini meupe yaani PLATINUM eneo la Marikana.
Wakati huohuo wachimba madini wameamriwa kurejea kazini siku ya Jumatatu la sivyo watafukuzwa kazi.
Lakini wengi wamesema kumaliza mgomo wao sasa ni sawa na kuwadhalilisha wenzao waliouawa.
Wanasema watarejea kugoma katika eneo la mgodi huo na wataendelea kushinikiza malipo bora zaidi ya kazi.
Hata hivyo chama cha wafanyakazi wa migodi cha NUM ambacho kina uhusiano wa karibu na chama tawala cha ANC - kinasema wanachama wake wamekubali kurejea kazini.
Mmoja wa wachimba madini hao Vuyisile Mchiza, amesema atarejea kazini iwapo idadi kubwa ya wenzake watakubaliana kusitisha mgomo.
''Iwapo idadi kubwa watarejea kazini kesho, basi na mimi nitakwenda''. Anasema. ''Iwapo wengi hawatakwenda kazini, nami pia sitakwenda, kwasababu sitaweza kufanya kazi wakati wengine wakiwa bado wanaomboleza''. Ameongeza.

Ajali ya ndege yamuuwa waziri Sudan


Wazir Ghazial Sadiq Abdelrahim aliuwawa ajalini
Waziri wa dini wa Sudan Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim ni miongoni mwa watu 31 waliouwawa katika jali ya ndege.
Shirika la habari la Sudan limesema kuwa mawaziri wengine wawili na pia viongozi wa chama kinachotawala la Omar el-Bashir pia waliuwawa.
Ndege hiyo ya ki-raia ambayo pia ilikuwa imebeba wakuu kadhaa wa kijeshi ilianguka katika eneo la milama ya Nuba
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea eneo la South Kordofan kwa sherehe za Eid al-Fitr ili kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mbali na waziri huyo wa maswala ya kidini Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim wegine waliofariki katika jali hiyo ni Justice mwenyekiti wa chama Makki Ali Balayil, Waziri wa vijana na michezo na Issa Daifallah, waziri wa utalii na wanyma pori.
Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Talodi huko South Kordofan, ikiwa imetoka mji mkuu Khartoum
Mji huo wa Talodi, uko kilomita 50 kutoka mpaka wa Sudan Kusini.
Taarifa za runinga ya taifa zinasema kuwa hali mbaya ya anga iliizuia ndege hiyo kutoa na ilipojaribu mara ya pili iligonga mlima.
Afisa mmoja wa shughuli za ndege alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ya iana ya Antonov.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ajali kadhaa mbaya za ndege. Na maafisa wa Sudan wamekuwa wakilalamika kuwa imekuwa vigumu wao kupata vipuri kwa sababu ya vikwazo vya Marekani.

Sunday, August 19, 2012

Watu wa Assam India warudi kwao

Wanafunzi na wafanyakazi kutoka kaskazini-mashariki mwa India, ambao wakiishi miji ya kusini, wanaendelea kurudi nyumbani, ingawa wakuu wameomba watu wawe tulivu.
Wafanyakazi wanasubiri treni kuondoka Bangalore

Wengi walihama miji mikuu kutokana na maneno kwenye mitandao ya jamii, kwamba kutafanywa ghasia dhidi ya watu kutoka Assam na maeneo mengine ya kaskazini-mashariki mwa India, ili kulipiza kisasi kwa mapambano yanayoendelea baina ya makabila tofauti ya Assam.
Treni mbili zimefika Assam, zikibeba abiria kutoka mji wa Bangalore.

Ebola yaibuka DRC piya

Ugonjwa wa Ebola umezuka kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Virusi cya Ebola

Wagonjwa wawili wamethibitishwa kuwa na virusi, mmoja wao amefariki.
Shirika la matibabu la MSF, lenye watu wake Isiro, linasema hatua zinachukuliwa ili kumtafuta na kumtenga mtu yeyote ambaye aliwakaribia wale walioambukizwa.
MSF inasema aina ya virusi vya Ebola ya Congo ni tofauti na ile ya Uganda, ambayo iliuwa watu 16 mwezi uliopita.

Saturday, August 18, 2012

Zuma ataka tume ichunguze mauaji

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amesema kuwa atabuni tume ya uchunguzi baada ya polisi kuwafyatulia risasi maelfu ya wafanyikazi wa migodi waliogoma siku ya Alhamisi.
Wanawake na watoto wakienda kutafuta habari za waume zao kwenye mgomo huko Rustenburg, Afrika Kusini
Rais wa chama cha wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa Association of Mineworkers and Construction Union, aliiambia BBC kuwa wanataka tume huru ya kimataifa kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari kinalaumiwa kwa ghasia hizo.
Kampuni inayomiliki migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za walioathirika, lakini inashikilia kuwa mgomo huo haukuwa halali.
Chama hicho kinataka nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi.
Watu kumi wakiwemo polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.

AIBU: AGNESS MASOGANGE ATOA "VIDEO YA UTUPU"


Hawa ndio wanajiita vioo vya jamii hivi dada zetu mnafikiria nini 

BAADA ya kuandamwa na skendo kibao za kutoka na vigogo kisura wa video za wasanii wa bongo, Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange, ameonekana kwenye mkanda wa picha ya ngono ambao umesambaa mtaani huku ikiwa dili kwa watu wanaotaka kuona umbo la mwanadada huyo.

Mkanda huo unaomuonesha mwanadada huyo akiwa mtupu, huku utata mkubwa ukizunguka kujua ni kitu gani kilichosababisha hadi kusambazwa kwa video hiyo.



  Mwandishi mmoja wa mtandao wa udaku hapa nchini
alifanikiwa kupata video hiyo ambayo mwanadada huyo ameonekana na kijana mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake.

Baada ya kupatikana kwa video hiyo mtandao huo ulijaribu kumsaka Agnes ili kufafanua uwepo wake ndani ya video hiyo lakini hakuweza kupatikana kwenye simu yake.

                                                  HII NDIO VIDEO YAKE HIYO.