Wenyewe hawajui lakini, mwanamke anaweza kunusa
hasira, naam ikiwe mumewe ana hasira hata akikaa kimya , mkewe atakuwa
wakwanza kujua kwamba mmmh! leo kumeharibika.
Mwanamke pia anaweza kunusa uogoa wa mumewe.
Dr Gün Semin wa Utrecht University, Ujerumani anasema hii ni kutokana na jasho la mwanamume!
Utafiti unaonyesha kuwa jasho analotoka
mwanamume linatuma ujumbe katika kiwili wili cha mwanamke na
kumuambukiza hali unayosikia bila ya wewe kumuambia kitu.. Jasho lako
linatuma ujumbe kwa mkeo au kwa mchumba wako.
Ukiwa wewe mwanamume umeshutshwa na kitu au
umebabaika au umeogopa au ana hasira. Jasho lako litasema. Na System ya
mama itapokea ujumbe!
Dr Gün Semin wa Ujerumani anasema mwanamume
akikasiria anatoa jasho lenye kemikali aina fulani. Akiwa na uoga
anatokwa na jasho aina tofauti.
Ndio maana mkeo au mchumba wako atakuuliza kuna
nini lakini? Hata ukikataa mwili wake unamuashiria kwamba lazima kuna
kitu. Sio ati wao ni wajanja sana lakini jasho lako limetoa chembechembe
fulani kulinagani na hali yao na hivyo kutuma ujumbe wa siri kwa system
ya mama.
Ni majaliwa ya wanawake hayo.
....

Kipepeo aweza kunusa mpenzi wake akiwa mbali
Vipepeo wanawake pia wanamajaliwa ya kuweza kunusa vitu.
Wanasayasi wanasema kipepeo ana uwezo wa kunusu kipepeo mchumba wake au anayemfaa hata akiwa maili 7 au nani hivi.
Kipepeo atanusa nakujua kiboko yangu anakuja japo yuko kilomita nyingi.
Nani mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kunusa? Kwa wanyama ni Dubu, yaani bear, sio teddy bear.
Baharini ni papa. Papa anaweza kunusa hata damu amboyo bado ingali ndani ya samaki mwengine. Ni papa huyo.
..............
Wanasayansi wanasema kuwa wanawake ni viumbe wa ajabu!
Katika mahusiano ya kawaida, urafiki tu wa
kimapenzi, boy friend na girl friend wanawake bila ya wao kujua huvutiwa
na watu wakaidi, watukutu watu wenye miguvu kuvu, misuli misulu, watu
wenye vimo virefu kwa kiingereza hao wabajulikana kama Alfa men.
wabasayansi wanasema watu wenye vurugu vurugu , watundu wanauwezo mkubwa wa kutongoza.
Pengine hii nikutokana na sababu ya kutoogopa kukataliwa.
........
Lakini katika ndoa wanawake bila ya wao hata
kujijua huvutiwa na watu wadhaifu , watu waungwana, wastaarabu, wenye
hekima watu wenye vimo vya wastani.

Wanawake wanapenda Alpha men kama wapenzi tu
Hata enzi za adamu na hawa mambo yalikuwa vivyo hivyo.
......
Watafiti wa maswala ya kijamii na mahusiano
wanasema kuwa kwa akina dada wengi katika ndoa huvutiwa na watu wasio na
misuli, wenye vimo vya wastani au hata wafupi - hawa kimombo
wanajulikana kama Beta men- B-E-T-A, Beta, baada ya Alfa , kuna Beta
katika alphabeti za kirumi.
Kwanini ieve hivyo.
Sayanmsi ya mahusiana inasema kuwa watu
wasiokuwa nguvu, vimo vya kutisha au misulu eti, eti wanajali sana
familkia zao na wake zao.
Maelezo ni kwamba
kwa kuwa hawaezi kushindana katika ulimwerngu wa
mahaba kwa kutumia nguvu na kifua basi mwenyezi mungu amewapa sifa za
kuwa wakarimu, wenye kutoa, kujali wapenzi wao , na kama njia ya kutinza
ndo zao Mungu amewapa watu sampuli hiyo uwezo wa kuwa waaminifu. Wasipo
kuwa hivyo kuna hofu ya kutorokwa!
Ni sayansi ya mahusiano!
.........
Jee unajua kuwa kufanya kazi usiku ni hatari kwa akina mama? Na inaweza kusababisha kifo?
Utafiti uliofanywa na madaktari nchini Uingereza
umegundua kuwa wanawake wanaopendelea kufanya kazi usiku wanahatari ya
kupatikana na sartani ya matiti- breast cancer.
Katika kichwa cha Kazi za usiku zinasababisha
vifo 500 kila mwaka nchini Uingereza utafiti hunasema shift za usiku ni
hatari kwa akina amma.
Dr Lesley Rushton, wa Imperial College Mjini
London anasema Mawanamke akifanya kazi ya usiku kwa wastani ya siku tatu
kwa wiki kwa miaka sita - anakaribisha kansa ya matiti.
Kufanya kazi usiku au kukosa usingizi kwa akina
mama kunatatiza utengenezaji wa homoni ya ya MELATONI, hii ni
chembechembe inayosaidia usingizi na hii inasadikiwa kuwa na uwezo wa
zuia kansa.
................
Wanasayansi wana mambo!

Dawa ya kuzuia nyumba ndogo
Sasa kumegunduliwa dawa aina ya homoni inayoweza kuwazuia wanaume kwenda nje, au kuwa na uhusiano wa pembeni,
Dawa hii iliyovumbuliwa Ujerumani inaitwa
FIDELITY HORMON. Dawa ya uaminifu! Au kampuni hiyo ya ujereumani imeipa
dawa hiyo jina la CUDDLE DRUG! Dawa ya kukumbatiana.
Dr René Hurlemann, of Bonn University nchini
Ujerumani anasema mwanamume akipewa dawa hii ya kumeza huyeyuka na
kuingia katika damu, hivyo mwanamke mrembo akipita karibu, basi mume
analazimika kukaa umbali wa inchi sita . Mume bila kujua damu yake
itakuwa haipatani na mwanamke mwengine mbali na mkewe.
Mwanamke huyo akiwa mrembo zaidi , ndio dawa inafanya kazi vizuri zaidi. Ni FIDELITY HORMON. Tembe za uaminifu.
.....

iPad inaweza kusababisha maradhi ya moyo
The iPad ni komputa ndogo ya mkoni hii
inatengezwa na kampuni ya Apple Ipad yakanzwa ilinza kuuzwa tarehe 3
April mwaka 2010 NA iPada ya kisasa zaidi imetolewa tarehe 2 novemba
mwaka huu wa 2012.
Ipada inaweza kupiga picha ya video, picha ya kawaida , kucheza muziki , kuzuru mtandao na mambo mewngi tu.
Lakini ujajua kwamba ukiwa na tabia ya kutumia
Ipad usiku usiku huenda ukapatikana na matatizo ya moyo au msongo au
kudorora kwa afya, yaani depression?
Utafiti pia unasema kuwa ukiwa na tabia ya
kuangali televisheni hadi usiku mpevu kila mara basi unakaribisha
maradhi ya moyo au depression.-kudorora kwa afya.
Profesa Samer Hattar anasema wa Marekani anasema
utafiti umegundua kuwa televisheni na komputa ya iPad inatoa mwanga
usistahili wakati mwili unahitajika kulala.
Hivyo kutumia iPad na televisheni usiku sana
inaweza kusababisha maradhi ya moyo au mtu kukosa raha maishani au
kutompenda starehe au mkuwa mtu pweke, kutumia iPad au televsiheni kila
mara usiku sana kunasababisha upweke.