NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, September 11, 2012

Somalia yapata Rais mpya

 
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Bunge la Somalia limemchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa Rais mpya wa nchi hiyo.
Kulikuwa na wagombea 22 kwenye uchaguzi huo, akiwemo Rais anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed na waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali.
Hassan Sheikh Mohamud alishinda kufuatia duru ya tatu ya upigaji kura, ambapo alikuwa anachuana na Rais anayeondoka Shariff Sheikh Ahmed.
Katika raundi ya kwanza Sheikh Ahmed alikuwa amepata ushindi mwembamba wa kura 64 dhidi ya 60 alizopata Sheikh Mohamud.
Kwa jumla wabunge 271 walipiga kura.
Katika duru ya mwisho wabunge wengi waliowaunga mkono wagombea waliochujwa walimuunga mkono Sheikh Mohamud , akapata kura 190 dhidi ya 70 alizopata Rais anayeondoka.
Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Rais kufanyika katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, tangu kuondolewa kwa serikali ya kijeshi mwaka 1991

Ethiopia kuwaachilia wandishi wa kigeni


Martin Schibbye na Johan Persson
Ethiopia imewasamehe waandishi habari wawili raia wa Sweden waliofungwa jela nchini humo mwaka jana kwa madai ya kuunga mkono vitendo vya kigaidi.
Wawili hao wanatarajiwa kuachiliwa baadaye wiki hii
Martin Schibbye na Johan Persson walikuwa wanahudumia kifungo cha miaka 11 baada ya kukamatwa mwaka jana mwezi wa saba na waasi mashariki mwa Ethiopia.
Duru za serikali zilisema kuwa waandishi hao walisamehewa na hayati Meles Zenawi kabla ya kifo chake mwezi jana.
Wamekuwa wakidai kuwa walikuwa tu nchini Ethiopia kikazi.
Schibbye na Persson, waliomba kuachiliwa baada ya hukumu yao mwaka jana kwa madai ya kuunga mkono kundi la wapiganaji la Ogaden (National Liberation Front (ONLF), ambalo Ethiopia inawaona kama kundi la kigaidi.
Afisaa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kujulikana, alisema kuwa waandishi hao wataachiliwa wiki hii pamoja na wafungwa wengine 1,900.
Mwaka mpya wa Ethiopia ambapo wafungwa huachiliwa, utasherehekewa siku ya Jumanne.
Meles,ambaye alikuwa mamlakani kwa miaka 21 alifariki mwezi jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Serikali imesema kuwa naibu wake Hailemariam Desalegn, ataapishwa kuhudumu hadi uchaguzi mpya utakapofanyika mwaka 2015.

Monday, September 10, 2012

Maadhimio ya Kamati kuu ya Chadema



1.Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri Emmanuel Nchimbi,IGP Mwema,Paul Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa FFU,na RPC IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na au wafukuzwe kazi

2.RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka

3.Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya kisiasa.1.ARUSHA vifo 3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU MASHARIKI,vifo 5, 4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.

4.Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli tata anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.

5.TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli na haki,kuisusia TBC

6.Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya hadhara ni lazima kwa mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni,pia kupata habari na taarifa

7.Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)

8.Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa mwanza Umevunjwa.
Imesomwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa

Hali mbaya ya wafungwa magerezani Chad

Ramani ya Chad
Wafungwa nchini Chad wanawekwa katika mazingira mabaya kiasi kuwa wanaotumikia kifungo wako katika hatari ya kufa jela.
Kulingana na shirika la Amnesty International, wafungwa wanawekwa katika magereza yaliyosongamana watu na kukosa hewa safi. Na yote hayo waliyashuhudia wakati walipotembelea magereza sita.
Ripoti ya shirika hilo imeelezea kisa kimoja ambapo wafungwa tisa walikufa gerezani baada ya kukosa hewa huku wengine saba wakiuawa kwa kupigwa risasi na walinzi.
Shirika hilo linasema kuwa wafungwa wanawake wanaishi katika hatari ya ubakaji na wengi wakiishi na watoto wao wenye hata miezi saba ndani ya magereza.
''Sio vyema wafungwa kuishi katika mazingira mabaya kama yale, mabaya sana kiasi cha mfungwa kuwa katika hatari ya kufia gerezani.'' alisema mtafiti mkuu wa shirika hilo Christian Mukosa.
"wafungwa wengi walikuwa na utapia mlo wakionekana wadhaifu sana. Baadhi walifungwa minyororo siku nzima wengi wakiugua maradhi ya ngozi, maradhi ya ngono, Malaria au Kifua kikuu" aliongeza Christian.
Shirika hilo limetoa wito kwa serikali kuchunguza madai hayo ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Serikali ya Chad bado haijajibu ripoti hiyo ya Amnesty.

Jeshi la Mali lauwa wasafiri

Jeshi la Mali linasema kuwa limewapiga risasi na kuwauwa watu 16 katika jimbo la Segou, katikati mwa nchi, baada ya gari la watu hao kutosimama kwenye kituo cha ukaguzi.
Rais Dioncounda Traore wa Mali (kulia) na Waziri Mkuu Midibo Diarra
Wakuu wanasema gari hilo liliendelea hata baada ya kuonywa kwa risasi.
Inaarifiwa kuwa baadhi ya wale waliouwawa ni wahubiri wa Kiislamu kutoka Mauritania, ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wa kidini nchini Mali.
Waandishi wa habari wanasema huenda kuwa jeshi liliwafikiria wasafiri hao kuwa wapiganaji wa Kiislamu ambao wanadhibiti eneo la kaskazini mwa Mali.

Somalia kupata rais Mpya

Wabunge wa Somalia
Wabunge 257 wa bunge jipya Somalia leo wanatarajiwa kumchagua rais wa nchi hiyo katika hatua ya hivi karibuni kuleta amani nchini humo.
Wabunge hao wapya wanakusanyika katika kituo cha mafunzo kwa polisi mjini Mogadishu kuanza kupiga kura.
Kamati ya uchaguzi imeidhinisha idadi ya wagombea 25 wa kiti hicho , akiwemo rais wa serikali ya mpito Sheikh Sharif sheikh Hassan na waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali.
Serikali ya mpito ambayo imedumu kwa muda wa miaka minane itakabidhi mamlaka kwa serikali mpya baada ya uchaguzi wa rais.
Rais wengi wa Somalia walilazimika kuikimbia nchi yao kufuatia hali mbaya ya usalama nchini Mwao.
Baadhi yao wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya wamekuwa na hisia mbali mbali kuhusu na mchakato wa kuleta amani na usalama pamoja na uthabiti unaoendelea nchini Somalia.
Mwandishi wa BBC mjini humo Daud Aweis anasema kuwa shughuli itachelewa kuhu wabunge wakipitia ukaguzi mkali kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi huo.
Ni Mara ya kwanza kwa miaka mingi kwa rais kuchaguliwa nchini Somalia ikiwa ni ishara ya usalama kuimarika.
Hata hivyo kundi la wapiganaji la al-Shabab, bado linadhibiti maeneo mengi ya kusini na katikati mwa Somalia.

Sunday, September 9, 2012

Wariri wa mambo ya Nje Mh.Bernard Membe ndani ya Mbamba Bey Mbinga

 Hivyo ndivyo anavyosema mwenyewe kupitia Tweeter Bado naendelea kuchati nae Nitakupa taarifa kulingana na sehemu alizopitia kutafuta ushahidi juu ya Ziwa Nyasa

Embedded image permalink
Mkutano wake  wa kwanza na Wazee wa Mbamba Bay unaofanyika pwani ya Ziwa Nyasa. Niko pamoja na Mbunge wa Mbinga na DC
Nimemaliza kuzungumza na Wazee wa Liuli, sasa naelekea Lituhi 

Waziri wa Kenya auziwa gari lililoibiwa

Waziri mmoja wa Kenya amekanusha kuwa amehusika na wizi wa gari moja la rais ambalo amekutwa nalo.
Rais Daniel Arap Moi
Waziri wa Serikali za Mitaa, Fred Gumo, alisema gari lake alikuwa amempa mfanya biashara alioko Mombasa na badala yake akakabidhiwa hilo gari, ambalo lilikuwa limeibiwa kutoka kwa rais wa zamani, Daniel Arap Moi, miaka mine iliyopita.
Bwana Gumo alisema hakujua kuwa gari hilo lilikuwa la kuibiwa.
Alisema hakulitumia sana kwa sababu hakupata nyaraka zote za gari hilo.

Wengi wauawa katika mapambano Sudan

Waasi wa Darfur wasema walivitimua vikosi vya serikali
Jeshi la Sudan na waasi wanasema wamekuwa katika mapambao tofauti mara mbili yaliyowaacha watu kadhaa kuuawa.
Jeshi linasema limewaua wapiganaji 32 walioshambulia kijiji magharibi mwa eneo la Darfur wakati waasi nao wakidai kuwa wamevitimua vikosi vya serikali kutoka eneo hilo.
Katika tukio tofauti Khartoum inasema kuwa waasi 45 wameuawa katika kijiji cha eneo la kusini la Kordofan, karibu na mpaka wa kusini wa Sudan.
Waasi wa Vuguvugu la Haki na Usawa (The Justice and Equality Movement-JEM) wamesema wamekiteka kijiji hicho huku wakiua askari mmoja.
Mwaka jana vikundi vya waasi katika majimbo mawili na pia katika jimbo la Blue Nile walianzisha muungano wenye lengo la kuiondoa serikali ya rais Omar al-Bashir.
Khartum inaishutumu Sudan Kusini kuwaunga mkono waasi hao.
Serikali mjini Juba inakanusha shutuma hizo ikiilaumu serikali ya Sudan kuyaunga mkono makundi ya waasi Sudan Kusini.
Mapigano ya hivi sasa yanakuja wakati Marekani ikiwa imetoa onyo kuhusu mgogoro unaoendelea wa mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Onyo hilo lilitolewa na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice kufuatia mkutano wa Baraza la Usalama kujadii mgogoro huo.
Sudan Kusini imekubali pendekezo la suluhu ya mpaka lililotolewa na Umoja wa Afrika, lakini Sudan inakataa pendekezo hilo.
Tarehe ya mwisho ya Agosti 2 ya kufikia muafaka iliyokuwa imewekwa na Umoja wa Mataifa imeshindwa kuzaa matunda.
Hata hivyo pande zote mbili zinashinikizwa kuwa zimefikia makubaliano kabla ya tarehe mpya iliyowekwa ya Septemba 22.
Sudan na Sudan Kusini zimekuwa katika mgogoro kuhusu mpaka kati ya nchi hizo mbili na mapato ya uchimbaji mafuta.
Sudan Kusini ilipata uhuru kutoka Sudan mwaka jana, ikimaliza miaka mingi ya mapigano kati ya eneo la kaskazini linalokaliwa na Waislamu wengi na lile la kusini lenye Wakristo wengi na dini nyingine.

Nigeria yaua wapiganaji wa Boko Haram

Ulinzi eneo la Maiduguri kaskazini mwa Nigeria
Jeshi la Nigeria linasema limewaua watu saba wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la wapiganaji wa Kiisalmu wenye msimamo mkali la Boko Haram katika mapambano kaskazini mwa nchi hiyo.
Msemaji wa jeshi hilo amesema watu wengine zaidi kumi na watatu wamekamatwa baada ya kushambulia kituo cha ukaguzi cha jeshi, katika mji wa Maiduguri.
Ghasia hizo zimetokea siku moja baada ya polisi wa Nigeria, kusema kuwa wataanza kulinda kutwa-kucha, milingoti ya simu za mkononi kufuatia milingoti kadhaa kama hiyo kushambuliwa mwezi uliopita, kaskazini mwa nchi.
Boko Haram ilisema ilifanya mashambulio hayo, kwa sababu milingoti hiyo inatumiwa kufuatilia mawasilino baina ya wafuasi wake.
Akitoa maelezo ya tukio hilo la Maiduguri, Luteni Kanali Sagir Musa amesema, ''Kundi la watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Boko Haram walishambulia kituo cha ukaguzi cha kijeshi sehemu ambayo wanajeshi walikuwa wameweka kizuizi na kufanya ukaguzi.
Ramani ya Nigeria ikionyesha eneo la Maiduguri
''Wanajeshi walijibu shambulio hilo kwa risasi. Watu saba wenye silaha waliuawa katika majibizano hayo ya ufyatulianaji risasi, na wengine kumi na watatu walikamatwa huku wengine wakikimbia. Hakuna majeruhi waliopatikana kwa upande wa wanajeshi.''
Boko Haram wanataka kuwekwa kwa utawala wa sheria ya Kiislamu nchini Nigeria.
Kundi hilo lilianzisha kampeni ya kijeshi mwaka 2009 kupigania kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu, likishambulia majengo ya serikali na makanisa na pia kuwaua wahubiri wa Kiislamu wenye msimamo wa kati.
Nchi hiyo imegawanyika kati ya eno la kaskazini lenye Waislamu wengi na lile la kusini linalokaliwa na Wakristo wengi na dini nyingine.

Saturday, September 8, 2012

Kanisa la Anglikana lataka kuwa na rais

Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana, Rowan Williams, amefichua kuwa kanisa hilo linaandaa mpango wa kumteua rais wa kanisa, ambaye atabeba sehemu ya jukumu la kuongoza kanisa duniani.
Askofu Rowan Williams

Alisema mtu atayechukua nafasi hiyo ataweza kusafiri kwa urahisi, na hivo kumuacha Askofu Mkuu kushughulika zaidi na kuongoza kanisa.
Doctor Williams, ambaye anastaafu mwezi wa Disemba baada ya uongozi wa miaka 10, alikiri kuwa hakuweza kufanya mengi kuzuwia mgawanyiko kanisani juu ya swala la uhusiano wa jinsia moja.

Hofu ya vita kuhusu mpaka wa Sudan na S. Kusini


Mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu mzozo wa Sudan mbili
Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice, amesema mzozo kuhusu mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini huenda ukasababisha vita kuzuka tena kati ya nchi hizo mbili.
Bi Rice ametoa matamshi yake katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu mzozo wa mpaka kati ya nchi hizo nchini Marekani.
Sudan Kusini imekubali mpango wa amani uliopendekezwa na Muungano wa nchi za Afrika ingawa Sudan imeukataa.
Nchi hizo mbili nusura zipigane mapema mwaka huu sababu kuu ikiwa mzozo wa mpaka na ugawanaji wa mapato ya mafuta .
Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka jana na kumaliza miaka mingi ya mapigano kati yake na Sudan.
Akiongea mjini New York, Bi Rice alisema kuwa hatua ya serikali ya Khartoum kukataa kusaini mpango wa amani inaweka nchi hizo katika hatari ya kurejelea vita.
Alisisitiza kuwa hatua ya kujikokota ya Khartoum inazua wasiwasi kuhusu kujitolea kwake kutatua mzozo huo.
Licha ya Sudan Kusini kukubali mpango wa amani, Bi Rice amekariri kuwa Marekani ina wasiwasi kwamba nchi hizo hazichukulii kwa uzito swala hilo kama ambalo linapaswa kushughulikiwa kwa dharura.
Muda wa mwisho uliowekwa na Umoja wa mataifa wa kuafikia makubaliano mwezi Agosti tarehe mbili, haukuweza kufikiwa na nchi hizo mbili.
Hata hivyo, pande hizo mbili zinashinikizwa kutia saini mpango huo wa amani ifikapo tarehe 22 mwezi Septemba.
Mwezi jana serikali za Khartoum na Juba zilifanya mkutano wa wiki tatu mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Kwenye mazungumzo hayo, mwafaka ulifikiwa wa kugawana mapato ya mauzo ya mafuta ingawa bado mazungumzo zaidi yanahitajika kuhusu usalama.
Mazungumzo hayo yataendelea mwishoni mwa mwezi Agosti.
Majeshi ya Sudan yamepigana mara kadhaa na yale ya Sudan kusini tangu Sudan kusini kujipatia uhuru mwaka jana.
Huenda baraza la usalama la umoja wa mataifa likaziwekea vikwazo nchi hizo iwapo zitashindwa kukubaliana kusitisha mzozo huo katika eneo la mpakani.

Wahamiaji haramu matatani Italia

Wahamiaji haramu waokolewa
Walinzi wa mwambao kutoka shirika la majeshi ya muungano ya NATO wanawatafuta manusura wa boti iliyozama ufuoni mwa kisiwa cha Lampedusa ambapo mtu mmoja alifariki na wengine wengi bado hawajulikani waliko.
Manusura wengine 56 wakiwemo wanawake wajawazito wameokolewa kutoka kwenye boti hiyo iliyozama mapema leo asubuhi.
Kisiwa cha Lampedusa ambacho kiko umbali wa kilomita 120 kutoka Tunisia, ni eneo ambalo hutumiwa na wahamiaji wengi haramu wa kiafrika kuingia barani Ulaya kwa sababu ya ukaribu wake kwa bara hilo.
Maafisa wanasema kuwa idadi ya watu waliokuwa kwenye boti hiyo heunda ikawa zaidi ya miamoja ikilinganishwa na idadi iliyokuwa imeripotiwa awali.
Baadhi ya manusura waliokolea kutoka baharini na wengine walikuwa kwenye sehemu ya kisiwa hicho ambako hakuishi watu.
Msemaji wa walinzi wa NATO, alinukuliwa akisema watu 56 wamepatikana wote raia wa Tunisia.
Mnamo siku ya Alhamisi, watu 56 walizama wengi wao wakiwa watoto baada ya boti yao kuzama Magharibi mwa pwani ya Uturuki.
Wengine 45 waliokuwa kwenye boti hiyo walinusurika.
Wahamiaji hao haramu walikuwa wairaqi, raia wa Syria na wapalestina wakikimbilia barani Ulaya.
Kulingana na shirika la kimataifa la Amnesty International, mnamo mwaka 2011, takriban watu 1,500 walizama katika bahari ya Mediterranea wakiwa njiani kuelekea barani Ulaya.
Wengi walikuwa wanatoroka vurugu nchini Tunisia na Libya,wakati wa harakati za mageuzi katika nchi za kiarabu.

Mashambulizi ya kulipiza kisasi Kenya

Ramani ya Kenya
Takriban watu kumi na moja wa kabila la Pokomo wameuawa katika mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi katika eneo la Tana River,Kusini Mashariki mwa Kenya.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema alisikia watu wakipiga mayowe wakati kijiji kimoja kilipokuwa kinashambuliwa na kisha wenyeji kuteketezwa.
Eneo hilo ambako zinaishi jamii za kuhamahama ni kitovu cha mizozo ya ardhi na maji kati ya jamii za Orma na Pokomo.
Watu wengine kumi walijeruhiwa kwenye uvamizi huo uliotokea usiku wa kuamkia leo.
Uvamizi huu umetokea baada ya mashambulizi mengine kutokea mwezi jana ambapo watu 52 kutoka jamii ya Orma wengi wakiwa watoto na wanawake kuuawa kwa kunyongwa na kuteketezwa kiasi cha kutotambulika.
Ni katika tukio ambalo lilitajwa kuwa ghasia mbaya za kikabila kutokea katika miaka ya hivi karibuni nchini Kenya. Polisi na viongozi wa kijamii walisaidia kutuliza hali na kurejesha usalama kati ya jamii hizo mbili lakini hali ya wasiwasi iimeendelea kutanda.
Licha ya kwamba polisi waliahidi kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo, viongozi wa eneo hilo wanasema vikosi vya usalama vimeshindwa kuzuia ghasia.
Mbunge wa eneo hilo, Danson Mungatana amewashtumu maafisa wa usalama kwa kushindwa kuchukua hatua za kuwalinda wananchi licha ya kufahamu mapema kwamba mashambulio yatatokea.
Jamii hizo mbili za Pokomo na Orma, zimekuwa zikizozana kuhusu matumizi ya ardhi na maji ambazo ni rasilimali adimu.
Wapokomo ni wakulima ambao hukuza chakula kando ya mto Tana wakati jamii ya Orma wakiwa wafugaji wa kuhamahama.

Friday, September 7, 2012

TANZANIA NCHI YANGU INAYOPOTEZA UHALISIA WAKE

Namshukuru Mungu kuzaliwa Tanzania, Nchi iliyobariliwa kila aina ya utajiri duniani, mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi kwa kila kitu ndiomana nchi kama za mashariki ya mbali ulaya na amerika zimetajirika kupitia maliasili za watanzania tuliolala usingizi bila kujua wapi tunaelekea na hii baiskeli yetu ya miti, kwanza napenda kutoa pole kwa ndugu zetu wote waliopoteza maisha kwenye matukio tofauti kama mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto,kuzama kwa meli ya MV BUKOBA,MV SPICE, MV SKAGIT, tumepoteza nguvu kazi kubwa ya taifa, lakini yote tisa sijui ni tatizo nini ukiuliza tumeunda tume tuwaachie tume wafanye kazi yao, yakitokea tena oooh nimakosa yakimaumbile sisi ni ngumu kuyazuia, wenzetu
wanazidi kuteketea, nchi inaingia gizani wawakilishi wetu wanakula rushwa wanaanza kurushia vijembe bungeni mambo yanapita hakuna hatua zilizochukuliwa, dah inaumiza sana, hivi napenda kuuliza tunaangalia maisha ya mjini tu au na watu wa kijijini tumewasahau, kwa sababu inasikitisha kuniambia uchumi umekuwa wakati watu zaidi ya milioni kumi hawajui watakula nini pale wanapofika muda husika kwa sababu hata shilingi mia moja hawana mfukoni. Mnamo mwaka 2010 nilibahatika kufanya utafiti katika mkoa wa Rukwa wilaya ya sumbawanga vijijini jimbo la kwela kuhusu kushuka kwa elimu katika mkoa wa Rukwa, ni masikitiko makubwa sana pale ukiipata hiyo taarifa nafikiri serikali ifike pahala iseme kuna maeneo tumeshindwa kufikia              malengo na watoe taarifa kwa nini wameshindwa hili hata wananchi watafute namna nyingine ya msaada hili wajikomboe na tatizo hili la uchumi.
Madini ya Tanzanite
Tatizo lingine vijana wakitanzania tuliowengi tunapenda mijadala ambayo haijengi nchi ni kubomoa nchi kwa sababu ya itikadi ya chama, na pili tumeshajiwekea katabia kakutofanya kazi sijui tunategemea nini, jamani hii nchi hawa jamaa wanaipeleka sehemu ambapo palipo tufanya tuwaone wakoloni wabaya, na watu wa kurekebisha hayo maswala ni sisi si wao, sasa tufike pahala jamani watanzania wenzangu tuangalie maisha haya na nchi yetu inapokwenda. ni mtazamo wangu
 
 Vijana wakiwa kijiweni na baada ya hapo ni kwenye pombe tu na mambo mengine sasa je tutaweza kujikwamuwa hapa tulipo na kwenda mbele licha tu ya kukosa ajira hata wenyewe kujishughulisha hatuwezi jamani.Hebu jamani tujufunze kutoka china,Watu wa China wanafanya kazi sana ndiomana hata nchi yao inakuwa kiuchumi si watu wakukaa tu kama hapa kwetu