NJOMBE

NJOMBE

Thursday, March 29, 2012

VODACOM FOUNDATION YAKINUFAISHA KIJIJI CHA INYUMBU MKOANI DODOMA KWA VISIMA



Mkuu wa Mfuko wa kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule (kwenye picha ya juu),akimsaidia kumweka ndoo kichwani  mama mmoja kati ya wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma, baada ya kukabidhi msaada wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 40 katika kijiji hicho.

DUNIANI KUNA MAMBO: MATATANI KWA KULEWESHA MBWA

Bwana mmoja nchini Marekani amekamatwa na polisi baada ya kumpa pombe mbwa wake na kumlewesha kiasi cha mbwa huyo kushindwa hata kutembea.

Bwana huyo Todd Harold Schreiner, anashtakiwa kwa kosa la kutesa wanyama. Polisi wa mji wa East Helena walikuta mbwa huyo akiwa amelewa chakari, mara nne zaidi ya kipimo cha wanadamu kinachoruhusu kuendesha gari.

Taarifa zinasema mbwa huyo aitwaye Arly II wakuweza kusimama au kutembea vyema wakati alipokutwa na polisi ndani ya baa moja saa tano na nusu usiku.

Mbwa huyo alichukuliwa na kupelekwa katika zahanati ya wanyama ambapo vipimo vilionesha ana ulevi wa asilimia sifuri nukta tatu nne nane katika damu yake.

Kisheria kipimo cha mwisho cha ulevi wanaadamu wanaruhusiwa kuwa nacho na kuendesha gari ni asilimia sifuri nukta sifuri nane. Muuzaji katka baa aliyokutwa mbwa huyo amesema mwenye mbwa alimpa mbwa wake kilevi aina ya vodka.

Monday, March 26, 2012

HILO NI VUMBI LINAENDA KWENYE MAKAZI YA WATU KUTOKA KIWANDA CHA SARUJI MBEYA, TAFAKARI? JE NEMC MPO?

PAKA MREFU DUNIANI KWA SASA


Guinness World Records has officially recognized cat named Trouble largest cat in the world.
 Representatives of the Guinness Book of Records measured the cat and veterinarians Savannah breed (a cross between an African wild cats (serval) and domestic non-pedigreed cats) from the clutches of up to shoulder height (height of 48 cm) and stated that this cat is a leopard - the world's longest cat.
Despite this remarkable growth, Trouble weighs a little - only about 9 pounds, because they do not like to eat a lot and has a very active life, constantly running around like a real wild cat.
The owner of a cat-American champion Debbie Maraspina from Sacramento, Calif., said she was proud of his pet, which is 3 years, and despite the fact that it belongs to the breed, the cats that are considered the largest in the world, her cat Trouble even walked the length of the bodies of their relatives. 

JE WAJUA NGE ANA VITAMIN C, MATE YA PAKA YANASAFISHA MAJI MBADALA WA WATER GUARD



Saturday, March 24, 2012

Kikwete awashukia wabunge, madiwan


Rais Jakaya Kikwete
Iringa
RAIS Jakaya Kikwete amewataka viongozi na wanasiasa wakiwamo wabunge na madiwani kuacha kusababisha migogoro kwa maslahi yao binafsi katika kusimamia maji ya Bonde la Mto Rufiji kwa lengo la kulinusuru bonde hilo.Pia Rais Kikwete ameagiza Mto  Ruaha usimamiwe vizuri kwa sababu maji yamekauka na kuhatarisha uchumi wa taifa kwa kuwa unatumika kuzalisha umeme na chakula.

Rais Kikwete alitoa rai hiyo baada ya kufanya ziara katika maeneo mbali mbali ikiwamo Pawaga unakopita Mto Ruaha na kuona jinsi maji yalivyopungua kwenye mto huo.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Iringa, Rais Kikwete alisema hakuna njia ya mkato kunusuru bonde hilo isipokuwa  viongozi wa serikali kusimamia kiukamilifu.

 “Wakati Serikali inapoamua kusimamia mazingira ikiwamo kuwaondoa watu kwenye vyanzo vya maji, wabunge na madiwani  acheni kusababisha migogoro kwa maslahi yenu binafsi, acheni tamaa ya kuomba kura kwa kutumia bonde hili  badala yake angalieni maslahi ya Taifa.

 “Kama itatokea vita kuu ya tatu ya Dunia, basi itakuwa vita ya kupigania maji, hali imekuwa mbaya sana na hakuna njia ya kujinusuru zaidi ya kufanya mabadiliko tena haraka,” alisema Kikwete.

Alisema ikiwa maji yataendelea kupungua kwa kasi, uchumi wa taifa utayumba kwa kuwa Taifa linategemea bonde hilo kujiendesha kiuchumi na kuzalisha umeme katika mabwawa ya Mtera na Kidatu sambamba na chakula kinachozalishwa kwenye mabonde Usangu, Kilombero na Rufiji.

“Itafika wakati chakula kitakuwa tabu, umeme shida na asilimia 80 mpaka 90 ya umeme na chakula nchini, kinapatikana  katika  Bonde la Ruaha, lazima tuchukue hatua za kulinusuru haraka bonde hilo,” alisema.

Kutokana na hali hiyo aliziagiza wizara zinazohusika kutafakari hatua za haraka ili kunusuru maji katika mabonde hayo.
Rais Kikwete alisema maji yamepungua nchini kwa sababu baadhi ya watu wamekuwa wakiharibu mazingira kama vile kukata miti, kuchoma moto hovyo na kuishi karibu na vyanzo vya maji.

Alisema uharibifu huo umesababisha kuwapo kwa  vipindi virefu vya tatizo la ukame na mafuriko.
Alisema kwa nchi zilizoendelea, suala la viwanda limekuwa likihatarisha amani ya nchi kutokana na kuwapo kwa mabadiliko makubwa ya tabia nchi.

 “Wakubwa wanaochafua mazingira wamekuwa wabishi kuchukua hatua kunusuru mazingira, hali hii itaendelea kuwa mbaya zaidi kwa sababu tayari kina cha bahari kimepanda, joto limeongezeka na kipindi cha ukame kimeongezeka,” alisema Kikwete.
Alisema ipo haja kwa viongozi kusimamia kwa ukaribu suala la mazingira na upatikanaji wa maji ili kuweza kufikia malengo ya millennia ikiwemo suala la wananchi wote kufikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Rais Kikwete alizindua miradi mikubwa ya maji miwili Mkoani Iringa wa kwanza ukiwa wa maji safi na taka wa manispaa ambao umegharimu zaidi y ash Bil 73 na kuweza kufikisha asilimia 96 ya wananchi wote wanaopata huduma ya maji safi.
Mradi mwingine ni wa Pawaga ambao umefadhiliwa na kanisa la Aglikan na kughalimu zaidi ya sh Bil mbili, ambao umewafikia zaidi ya wananchi 20,500 wa maeneo hayo.

Aliwataka wananchi kutunza miradi hiyo ambayo imefadhiliwa na Jumuiya ya Watu wa Ulaya na Ujerumani ili kuepuka tatizo la upatikanaji wa maji ambalo lilidumu kwa muda mrefu.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dr Christine Ishengoma alisema mkoa huo umeanza kuhifadhi vyanzo vyake vya maji.
Habari na Mwananchi

Thursday, March 22, 2012

Raia wa Zambia wazua vurugu mpakani Tunduma

Vurugu zimeibuka katika mji mdogo wa Tunduma mpaka wa Tanzania na Zambia kufuatia wananchi wa Zambia kudaiwa kuwazuia wafanyabiashara kutoka Tanzania kuvuka mpaka kwenda kufanyia biashara zao nchini humo.
Kutokana na hatua hiyo, Watanzania nao walijibu mapigo kwa kuwatimua raia wa Zambia waliokuwa wakifanya biashara zao upande wa Tanzania na hivyo kusababisha kuibuka kwa vurugu katika mpaka huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo, akizungumza na NIPASHE jana mjini Vwawa alisema baada ya kujulishwa kutokea kwa vurugu hizo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya imekwenda mjini Tunduma ambako walijadiliana kwa pamoja na hatimaye vurugu hizo kudhibitiwa.
“Ni kweli nimejulishwa kuwapo kwa tukio hilo. Lakini kimsingi hazikuwa vurugu kubwa. Kamati ya Ulinzi na Usalama imeweza kulishughulikia suala hilo na sasa hali imetulia katika mji huo,” alisema Kimolo.
Hata hivyo, alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimechukua hatua ya kuimarisha ulinzi katika kila kona ya mji huo ili kusitokee machafuko zaidi yatakayoleta athari kwa wananchi wa Tunduma na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji wa Tunduma, Aidan Mwashiga, alisema vurugu hizo ziliibuka baada ya wananchi wa mji wa Nakonde Zambia kuendesha operesheni ya kuwatimua Watanzania wanaofanya biashara zisizokuwa za halali katika mji huo.
Alisema kufuatia hali hiyo, Watanzania nao walichukua hatua ya kuanza kuwatimua wafanyabiashara wa Zambia wanaofanya biashara zao katika mji wa Tunduma na kusababisha kutokea kwa vurugu.
Hata hivyo, alisema vurugu hizo zimedhibitiwa na vyombo vya  ulinzi na usalama na kwamba askari wamewekwa tayari katika mji wa Tunduma ili kama kutaibuka vurugu ziweze kudhibitiwa.
Mji wa Tunduma umekuwa mara kadhaa ukikumbwa na vurugu zinazosababishwa na wafanyabiashara wa pande mbili.
Mwaka 2005, mfanyabiashara wa Tanzania aliuawa na askari polisi wa nchini Zambia na hivyo kusababisha mpaka wa Tanzania kufungwa kwa siku tatu hadi serikali ilipomaliza tatizo hilo kwa kukaa na serikali ya Zambia.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, alipofanya ziara wilayani Mbozi, aliagiza Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kuimarisha ulinzi katika mji wa Tunduma kufuatia kutokea kwa matukio ya vurugu mara kwa mara katika mji huo.
CHANZO: NIPASHE

Tembelea hifadhi za Taifa wakati wa Pasaka



Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na makampuni ya usafirishaji watalii ya PongoSafaris, Burco safaris na Cordial Tours kwa pamoja wamekutayarishia wewe mwananchi ofa kabambe ya Pasaka ya kutembelea Hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi na mji wa kihistoria wa Bagamoyo kama ifuatavyo.
SAFARI YA RUAHA/MIKUMI
Kuondoka Dar: (Asubuhi) 3/4/2010
Kuondoka Ruaha: (Asubuhi) 5/4/2010
Gharama: 250,000/= (Mtu mzima)
SAFARI YA MIKUMI
Kuondoka Dar: (Asubuhi) 5/4/2010
Kurudi (Jioni): 5/4/2010
Gharama: 40,000/= (Mtu mzima)
SAFARI YA KULALA MIKUMI
Kuondoka Dar (Asubuhi): 4/4/2010
Kurudi (Asubuhi): 5/4/2010
Gharama : 90,000/= (Mtu mzima)
SAFARI YA BAGAMOYO
Kuondoka Dar (Asubuhi): 4/4/2010
Kurudi Dar (Jioni): 4/4/2010
Gharama: 25,000/=( mtu mzima)
  • Gharama za watoto kwa safari zote zitakuwa kama ifuatavyo: Miaka 0-3 (Bure); Miaka 4-10 (50% ya gharama ya mtu mzima)
  • Gharama zote zinajumuisha: Usafiri, Ada za viingilio, Malazi, Uongozaji, Chakula na vinywaji baridi. Makampuni hayatahusika na ghara nyinginezo kama vile vileo, sigara n.k.
  • Kiwango cha chini cha idadi ya watu wanaohitajika kwa kila safari ni 15
Wahi sasa nafasi yako na kulipia kabla ya tarehe 2/4/2010 katika ofisi zao kama ifuatavyo;
PONGO SAFARIS & TOURS LIMITED
NIC Life house, 3rd floor, Sokoine Drive/Ohio Street, DSM
Tel: +255-22-2135728 Mob: +255 714354444
Email: info@pongosafaris.com
BURCO SAFARIS
Ground floor, NSSF Water front house,
Sokoine Drive, DSM
Tel: +255-22-2128010/2125408
Email: safaris@burco.co.tz

CORDIAL TOURS
Tel: +255-22-2136259 Mob: +255 754 270784
Email: info@cordialtours.com

Wednesday, March 21, 2012

Taswira Toka Kisiwa cha Mbudya

Mbudya ni Moja ya visiwa vilivyopo katika pwani ya Kaskazini mwa jiji la Dar Es Saalam, Maeneo ya Kunduchi. Ni eneo ambalo ni tengwa kwa lengo la kulinda na kuhifadhi viumbe wa baharini wanaopatikana eneo hilo. Hii haizuii wageni kwenda na kupumzika kisiwani hapo. Wadau wengi hivi sasa wamekuwa wakikitumia kisiwa hiki kama eneo la mpumziko ya weekend na siku nyingine za wiki huku wengine wakienda mbali hadi kupiga kambi ndani ya kisiwa - tented camping. Kipo chini ya Wizara ya Uvuvi (Sio Utalii na Maliasili). Kimsingi kuna njia moja kuu ya kuweza kufika hapo ambayo ni kwa njia ya Boti. Unaweza kwenda kwa boti binafsi au kwa kutumia boti 'za umma' ambazo zinafanya safari mara kwa mara katika siku tokea katika hoteli mbalimbali zilizopo kwenye pwani ya kunduchi. Huduma ya boti hizi ipo ktk hoteli za white sands na Jangwani Sea breeze. Ubao juu unakupa taarifa kadhaa za kuzingatia kama mgeni uwapo katika kisiwa cha mbudya.
Kuwa ktk eneo la kina kirefu kunamhakikishia mgeni wa kisiwa hiki fursa ya kupata maji ya kina kirefu muda wowote kwa yule ambae kuogelea ni sehemu ya starehe na mapumziko yake awapo ufukweni. Kina pWani nzuri yenye mchanga mweupe.

Maji yanapokuwa yamekupwa, pwani za kisiwa cha mbudya hutoa fursa kwa wageni kuafanya michezo kadha wa kadha kwenye mchanga. licha ya hili, maji yenye kina cha kutosha huwepo pia hata wakati wa maji kupwa (kina kifupi), tofauti na maeneo mengine ambako maji huwa yanakuwa kama hayapo kipindi hiki
huu ni upande mwingine unaojulikana kama Campsite. Kuna mwekezaji alipewa fursa ya kuanzisha na kuendesha campsite pembezoni mwa hapa, lakini inaelekea mipango haikuwa sawia na mategemeo hali iliyopelekea baadhi ya vitu kuachwa kama havina mwenyewe. Sasa hivi anayekuja hapa kisiwani yupo huru kupunga upepo upande huu. Pwani ya upande huu nayo ina mchanga mweupe na sehemu nzuri ya kuogelea pia. Kitu kimoja cha nyongeza kwa kisiwa cha Mbudya ni kwamba mgeni una uwezo wa kuleta vyakula na hata vinywaji vyako kama utapenda. Japo vinywaji baridi na hata vya moto vinapatikana.
huu ndio usafiri tulioutumia siku hii. Unafanya safari zake kati ya kisiwa cha Mbudya na Hotel ya White sands. Hapo nahodha alikuwa anauweka sawa tuanze kupanda na kurudi Mjini mida ya jioni.
Abiria wakijivuta kwenda kupanda boti tayari kwa safari ya kurudi. Wengi wetu tulikuwa tumeanzia safari ktk hoteli ya white sands. Unaweza kuwasiliana na Mdau Omary kupitia 0713202946 ili akupe mpango mzima wa jinsi ya kufika huko na gharama husika. hata hapa, wazawa tuna punguzo la bei kwenye kiingilio cha kisiwani.

Ni ruksa kwenda kisiwa cha Mbudya kwa boti Binafsi. Siku hii kulikuwa na familia kadhaa ambazo zilikuwa zimekuja kupumzika kisiwa cha Mbudya kwa kutumia namna hii ya usafiri.

Wapo walioamua kucheza michezo mbalimbali ya majini kwa kutumia boti zao.



Tuesday, March 20, 2012

EBWANA DA MWANADASHOST LINA AKIWA MBEFELE MAREKANI

  Mapic ya kufa mtu






Linar Sanga mwanamuziki wa kizazi kipya sasa yupo marekani kwa muda wa miezi mitatu katika tua inayoitwa "NATAMANI TOUR

Dar kukosa maji siku mbili

Baadhi ya vitongoji vya jiji la Dar es Salaam vinatarajia kukosa huduma ya maji kwa siku mbili kutokana na kupasuka kwa bomba kubwa linalosambaza huduma hiyo katika eneo la gereji Wilaya ya Bagamoyo.

Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Maji safi na Maji taka (Dawasco), Teddy Mlengu, alisema baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam yanatarajiwa kutopata huduma ya maji kutokana na kupasuka kwa bomba kubwa linalosambaza huduma hiyo katikati ya jiji
Maeneo yatakayoathirika na huduma hiyo, kuwa ni Mbezi Beach, Kawe, Tegeta, Sinza, Mwenge, Ilala, Mwananyamala na Bunju.
Alisema mafundi wanashughulikia tatizo hilo kwa juhudi kubwa na wanatarajia kulifunga kesho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kutumia maji kwa uangalifu kwa kujiwekea akiba ya kutosha.
Mlengu alisema Jumamosi walilazimika kuzima mtambo unaosambaza huduma ya maji katika maeneo hayo kutokana na hitilafu ya umeme. 


Chanzo:Nipashe

Wanajeshi waua raia watano kwa risasi

Watu watano wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kuzuka tafrani baina ya wananchi na wanajeshi waliokuwa wakishirikiana na mgambo kuendesha operesheni maalum ya kuwaondoa waliovamia eneo la hifadhi katika kijiji cha Maguba, kata ya Igawa, tarafa ya Malinyi wilayani Ulanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo saa Jumamosi iliyopita saa 8:00 mchana.
Waliouawa ni Sanyiwa Ndaya (34), Lutaya Ndala (48), Nchambi Bujiku (28), Kulwa Luhende (48) na Shija Msheshiwa (35), ambaye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Ulanga. Wote wakazi wa Kijiji cha Mguba, kata ya Igawa.
Waliojeruhiwa na kulazwa  Hospitali ya Wilaya ya Ulanga ni Nkama Jisonge (35), Zina Msheshiwa (30), Msheshiwa Taiya (60) na MT 70328 Koplo Paulo Lawrent ambao hali zao zimeelezwa kuendelea vizuri.
Akifafanua kuhusiana na tukio hilo, Kamanda Chialo alisema kuwa siku ya tukio askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Job Edward (54) Ofisa Mteule wa daraja la pili, ambaye ni mshauri wa mgambo wilaya ya Mahenge akiongoza timu ya watu 15 akiwemo askari mwingine wa jeshi hilo, MT 70328 Koplo Paulo Lawrent na mgambo, walikwenda katika eneo hilo kwa ajili ya operesheni maalum ya kuwaondoa watu waliovamia hifadhi hiyo.
Kwa mujibu wa Kamanda Chialo, watu hao baada ya kufika walivamiwa na wananchi waliokuwa na silaha za kijadi na walipojaribu kujitetea, Koplo Lawrent aliyekuwa na bunduki aina ya SMG alifyatua risasi hewani ili kuwatawanya wananchi hao ambao waliendelea kupambana nao.
“Na yeye huenda katika kunusuru silaha ile isiporwe na wananchi, alirusha risasi hewani zilizopoteza maisha ya wananchi wanne pale pale katika eneo la tukio, huku mwananchi mmoja akifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mahenge,” alisema Kamanda Chialo.
Kufuatia tukio hilo, Chialo alisema watu wanane wamekamatwa na wanahojiwa na polisi ili hatua zaidi za kisheria dhidi yao zikuchukuliwe na kuongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Awali, ilidaiwa kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro ilikwenda katika eneo hilo na kuwazuia wananchi kuendelea na shughuli za kilimo na uharibifu wa mazingira katika eneo hilo la hifadhi, lakini walikataa kwa madai kuwa hawafahamu mipaka kati ya eneo lao na eneo la hifadhi.
Inadaiwa kuwa mipaka hiyo iliwekwa na Serikali na wananchi hao kutakiwa kutii mamlaka ya Serikali kwa kuacha kufanya uharibifu ndani ya hifadhi bila mafanikio, hadi ilipofanyika operesheni hiyo katika eneo hilo ambalo ni hifadhi ya wanyamapori linalomilikiwa na wizara ya Maliasili na Utalii.
Habari kamili na Nipashe

Hii ndio Tanzania tembea ujionee

Hii ilikuwa Oktoba 2011 - Mto Rufiji


Mto Rufiji ulivyo Sasa hivi...


Pembezoni mwa Mto Rufiji hivi karibuni na taswira hizi za hali ya Mto Rufiji ulivyo sasa hivi.

Uwanja mdogo wa ndege wa Mtemere - Selous GR

Ni Uwanja mdogo wa ndege wa Mtemere uliopo pembezoni mwa geti la Mtemere, geti la kuingilia kwenye pori la akiba la Selous huko Mloka Rufiji. Ni uwanja ambao unatumika zaidi na ndege ndogo ambazo huleta wageni ukanda wa Mtemere. Selous kuna viwanja kama hivi kadha wa kadha vingiwe vikiwa chini ya usimamizi wa hotel ambazo ndio watumiaji wakuu. Picha hizi zilipigwa wakati wa kumalizia game walk ambapo tulikuwa tunarudi kwenye geti la mtemere ili tuendelee na mambo mengine. unayoiona kwenye picha ya juu ni njia ya kurukia na kutua ndege - runway - ya uwanja huu.

Mashirika kadhaa ya ndege ndogo yana safari za kila mara (scheduled) kwenda Selous kupitia kiwanja hiki. Coastal Air ni mojawapo.

Eneo la maegesho ya ndege wakati wa kushusha na kupakia abira.

Magari ya hoteli na makampuni mengine yakiwa pembe ya uwanja yakisubiri ndege ya coastal ili wapokee wageni wao. Coastal hupeleka ndege mara mbili kwa siku ktk kiwanja cha Mtemere. Ya kwanza hutua saa nne asubuhi na ya pili (mwisho) hufika majira ya saa kumi jioni.

Taswira toka Selous GR


Mama na mwana

Wababe wa majini wakiwa ndani ya moja ya maziwa ndani ya pori la akiba la Selous.
Inaelezwa ya kwamba Viboko ndio wanaongoza kwa kujeruhi na kuua watu barani Afrika (kusini mwa Sahara) kushinda mnyama mwingine yeyote yule wa porini.

Mtaani tunasema ukiona manyoya ujue kaliwa..
Porini wanasema ukiwaona hawa jamaa wapo chini ujue kaliwa pia

Shughuli ya sharubu ni usiku, mchana ni siesta kwa kwenda mbele

Kipanga