NJOMBE

NJOMBE

Sunday, November 11, 2012

SABABU ZA KUMFANYA MTU AKAKOROMA NA JINSI YA KUZUIA

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?
Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:
• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.
• Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.
• Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.
• Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.
• Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.



Je, Dawa ya kukoroma ni nini?
Swali hilo limeulizwa sana na mimi katika kulijibu ningependa kusema kuwa, kujua sababu inayosababisha mtu akorome na kuitatua au kuiondoa sababu hiyo ndiko kunakotibu kukoroma. Sote tunajua adha inayotokana na kukoroma, na sauti hiyo inavyosumbua hasa iwapo anayekoroma ni mtu wako wa karibu kama vile mumeo, mwenzi wako au yoyote yule inayekubidi ulale naye karibu au katika kitanda kimojana hata chumba kimoja. Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde kadhaa ambapo usingizi pia hukatika. Wanaokoroma pia hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. Vilevile tunapaswa kujua kuwa kukoroma kuna athari za kiafya za muda mrefu kwa mtu anayekoroma hivyo si jambo la kufanyia mzaha na ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa.
Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:
1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.
2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.
3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.
4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.




Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, unashauriwa ujaribu yafuatayo: Punguza uzito Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa. Wacha kuvuta sigara. Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana. Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.

Wataalamu pia wanasema kwamba unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile
. Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.
. Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.
. Kutokunywa pombe kabla ya kulala.
. Kutotumia dawa aina ya antihistamines.
. Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na kurudisha ulimi nyuma kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa kulia na wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30. Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini.
Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofauti zilizoelezwa, usife moyo jaribu kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo. Madakatari wataalamu wa magonjwa ya pua, masikio na koo au ENT wanaweza kukusaidia zaidi kutatua tatizo hilo. Siku hizi kuna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa mahospitalini ili kuondoa kukoroma kama vile kifaa kinachowekwa kwenye meno, CPAP, kidude kinachowekwa mdomoni au hata kufanyiwa operesheni ili kuondoa tatizo hilo.

Je unajuwa kinachoweka nyumba nadhifu:Upangaji wa nyumba


arrange
Upangaji wa nyumba hasa sebule, jikoni na vyumbani ni jambo ambalo kila mwanamke anapenda alifanye kwa ukamilifu. Tatizo linakuja muda wa kufanya hivyo unakuwa hafifu sababu ya shughuli nyingi za ujenzi wa taifa na kazi ya Mungu pia.
Kuna njia nzuri ya kukuwezesha kufanya hivyo kwa muda huo kidogo ulio nao. Kwanza angalia zile sehemu ambazo zinahitaji muda mrefu ili ziwe nadhifu, kwa mfano jikoni, kabati languo, chumba cha watoto, shelfu la vitabu n.k.
Panga muda wa dakika 15 kila siku ambao utautumia kufanya shughuli hii. Anza na eneo moja kwanza hadi umalize ndio uende sehemu nyingine, ikiwezekana weka alarm ili usitumie zaidi ya dakika 15.
Mwanzo kazi itakuwa ngumu hasa kama hukuwa na utaratibu wa kupanga mara kwa mara ila baadaye utaona ilivyo rahisi kuweka nyumba yako nadhifu bila kutumia nguvu nyingi.
Inatosha kwa leo.

Mungu akubariki sana.
Happy Sunday

Saturday, November 10, 2012

MSHINDI WA MILIONI 50 WA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 NI WALTER CHILAMBO.

Walter ameandika kwenye profile yake kuwa.....Asante tena ndugu zangu, Nawashukuru ingawa hadi sasa inakuwa ngumu kuamini.
Samahani kwa kutojibu sms zenu kama kawaida yangu ni kwa sababu zimekuwa nyingi mnielewe. Nawashukuru sana. ASANTENI SANA tuendelee kuwa pamoja daima..
Walter Chilambo alionekana kutawala tukio la jana la kumtafuta star wa Bongo pale Diamond Jubilee ambapo kila alipomaliza kuimba, MC Vanessa Mdee alisema "hili tamasha limekuwa kama lako!" Walter alifanikiwa kuingia katika round zoote za mchujo na kufanikiwa kunyakua shilingi taslimu milioni 50.

TOP 5
 Jamaa kwenye profile yake ya facebook ameandika...."Hadi Ben Pol alinikubali!!

Salma na Walter wakiwa matumbo joto wakisubili kutajwa mshindi.
Hapa ni wakati wakitangaza matokeo ya mshindi wa BSS 2012.
 Hapa Walter akimkumbatia Madam Rita mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.

 Mshidi wa EBSS 2012 Walter Chilambo akikabidhiwa kitita cha milioni 50.


Umati wa watu ukishuhudia milioni 50 zikikabidhiwa kwa mshindi.

Na hatimae alimwaga mshiriki mwenzake wa kiume Wababa ambaye watanzania wengi walimpenda akiwa jukwaani lakini walisahau kumpigia kura. Hatahivyo mapambano ya Walter hayakuishia kwa mshiriki mwenzake Wababa bali yalihamia kwa mwanadada mrembo, mwenye mwanya na mtaalamu wa kucheza na gitaa "Salma Yusuf.

SALMA YUSUF - MSHINDI WA PILI
Huenda kosa alilofanya Salma, aliimba nyimbo za Kiingereza ambazo hazikuwasisimua wapigaji kura wa Epiq Bongo Star Search ya wakati wa mwisho mwisho, lakini Salma ni mtaalamu, nimkali na hata ukimsikiliza unasahau kama ni mgeni katika game la muziki.

Nafasi hiyo Walter aliituimia kisawa sawa kabisa kwani kutokana na kipaji chake cha muziki wa Bongo flava, alichagua nyimbo zinazopendwa na watanzania wengi. Wimbo wa Ben Pol ndio uliomtajirisha Walter na kumfanya star.... Ben Pol alikili kutendewa haki na msanii Walter pale alipokuwa akiimba wimbo wake kwa mara ya mwisho.... hivyo Ben Pol aliinuka kwenyekiti na kumtunza manoti ya fedha Walter.

TOP 5
VOCALIST - NSAMI NKWABI.... AMEFUNGUKA KUWA...
"Napenda sana kumshukuru Mungu kwa hatua niliyofikia, napenda pia kushukuru familia yangu na shukurani nyinyi kwa mashabiki wangu kwa kunipenda, kunipa nguvu na kunishauri nawapenda sana na samahani kwa kuwaangusha wapendwa sauti iliniharibia mwishoni lakini tupo pamoja sana. Nawapenda sana wapendwa mbarikiwe na wale wasabato wenzangu sabato njema!"
Madam Rita na Master J
NSHOMA
MC'S WA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012.
Hii ndio sehemu ya VIP ya shindano la Bongo star Search lilipofanyika pale Diamond Jubilee.
Washiriki wote walioingia top five, walikuwa ni wakali... so hongereni sana kwa kazi nzuri mliyoionyesha kwa wakati wote mliokuwa mkitizamwa na watanzania wenzenu, sehemu mbali mbali za dunia.Hongera sana Walter Chilambo mana hata mimi nimekiri kuwa jamaa anajuwa alistahiri pongezi kwako Walter.

Friday, November 9, 2012

VIJANA WAKIGOMBEA KWENDA KUFUKUA MAKABURI IRINGA

Vijana  wa Manispaa ya Iringa wakigombea  kuingia katika gari ya Manispaa ya Iringa kwa ajili ya kwenda  kufanya kazi ya  kufukua makaburi na kuchimba makaburi mapya  kwa ajili ya  kupisha mradi mkubwa wa umeme  kutoka Iringa kwenda Shinyanga leo     
Habari na Francis Godwin

Mbinu za kusoma na kuelewa


Tunapozungumzia uelewa wa wanafunzi darasani tunakuwa tumeingia katika msitu mpana zaidi wa majibu, lakini ukweli unabaki kuwa ndani ya darasa linalofundiswa na mwalimu mmoja hutokea wanafunzi wengine wakaelewa zaidi  na wengine wasielewe kabisa.

Kuna wanafunzi na baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kuna binadamu huzaliwa na uwezo mkubwa wa kuelewa zaidi ya wenzao, huu ni ukweli lakini si wa kuamini sana kwani kipimo cha kuhakikisha kuwa huyu ameumbwa hivyo hakuna zaidi ya kuangali tu yale ambayo yanatendwa na huyo anayeitwa ana akili za ziada au za kuzaliwa.

Lakini wakati huo huo kuangalia ayatendayo mtu au kuangalia uelewa wake darasani hakutoshi kumpa sifa za kuwa na sababu ya kuwazidi wenzake ambao wameamua tu kutokusoma, kutomsikiliza mwalimu, kutozingatia wanachoelekezwa au wameharibiwa na masumufu ya dunia yakiwemo masuala ya mapenzi.

Kwa maana hiyo, hawa ambao hawaelewi kwa sababu wanasoma huku wanawaza mambo ya kimapenzi au wanafikiria kwenda muziki au  kucheza, hawawezi kuwekwa kwenye kundi la watu ambao hawakuzaliwa na akili bali waliojiharibu kwa kukosa kuufahamu ukweli.

Hivyo basi, kuna kila sababu kwa mwanafunzi kupuuza fikra za kizembe zinazomfanya ajione kuwa anazidiwa na wenzake darasani kwa sababu yeye hakuzaliwa na akili nyingi. Kila binadamu mwenye akili timamu kwa mujibu wa tafiti za watalaamu wa masuala ya ufahamu ana uwezo mkubwa mara 1000 kuliko ule anaoutumia.

Hii ina maana kuwa kama kuna mwanafunzi anaongoza darasa lenye watu 100, uwezo huo wa kuongoza anaweza kusonga nao mpaka akafikia kwa watu 1,000 na akifika hapo anaongeza mara 1,000 tena na tena. Huu ni uwezo wa ajabu sana alionao mwanadamu. Lakini wengi kati yetu tumeshindwa kusonga mbele mara elfu toka tulipo kwa sababu tumeshindwa kutumia kipawa chetu na tumeamini uongo kuwa kuna waliopendelewa tangu wanaumbwa.

Ben Carson mwandishi mashuhuri na daktari bingwa wa magonjwa ya akili ambaye awali alikuwa akiburuza mkia darasani aliambiwa na mama yake aitwaye Sanya Carson maneno haya: �you can do anything they can do, only you can do it better� (Nukuu inapatikana ndani ya kitabu kiitwacho THINK BIG cha Ben Carson ukurasa wa 7) kwa tafsiri isiyo rasimi Ben aliambiwa na mama yake kuwa �unaweza kufanya wayafanyayo, lakini wewe unaweza kufanya zaidi yao�

Mwanamke huyu alidumu kumwambia mwanae kuwa ni bora zaidi ya wengine na kumtaka aongeze bidii kila siku ili afikie lengo. Ben aliaamini aliyokuwa akiambiwa na kwa makusudi aliamua kujibidisha na hatimaye kufikia  kiwango cha kuwa msomi mwenye kuheshimika ulimwenguni.

Kimsingi kuna watu wengi ambao walipuuza kauli za kujiona duni na kufanikiwa katika mambo waliyokusudia kuyafanya. Huu ni ushahidi kuwa hajaumbwa mwanadamu kuwa wa mwisho darasani bali matokeo ya kushindwa ni lazima yapewe kwanza sababu za uzembe na maumbile yawe ni ya mwisho kufikiriwa. Ufuatao ni muongozo wa kumuwezesha mwanafunzi kusoma na kuelewa vema.

-Kumzingatia mwalimu

Wanafunzi wengi wanashindwa kufikia uelewa wa juu kwenye masomo yao kwa sababu hawawi makini wanapofundishwa darasani na waalimu wao. Kitendo cha kuweka mawazo nusu darasani na nusu nje ni kujiwekea kizingiti cha kuelewa kinachofundishwa.

Ni muhimu kwa mwanafunzi kama nilivyosema awali kwamba ampende mwalimu wake na aone furaha kumsikiliza anapofundisha. Itakuwa vigumu kwa mwanafunzi kuelewa anachofundishwa kama anayemfundisha anamchukia eti tu kwa sababu jana alimwadhibu au alimfokea.

Ifahamike kuwa, msingi mkubwa kabisa wa mwanafunzi kuelewa somo lo lote ni kuelewa anachofundiswa moja kwa moja toka kwa mwalimu wake. Kitendo cha kutoka darasani bila kujua kilichofundishwa ni jambo la hatari kwa maendeleo ya mwanafunzi kimasomo.

Inashauri kuwa mwanafunzi anapoingia darasani anatakiwa kuwa makini na kufuata anachoongea mwalimu wake neno kwa neno, huku akinoti anachoelewa na asichoelewa, ili kama ni msaada wa kueleweshwa aombe muda mfupi baada ya mwalimu kumaliza kufundisha.

Kurudia notisi

Mara baada ya mwanafunzi kufundishwa na kuelewa, anatakiwa akifika nyumbani siku hiyo hiyo arudia yale aliyosoma kwa kujikumbusha alichosema mwalimu wake. Hii itamsaidia zaidi kuifanya akili itunze kumbukumbu ya somo alilofundishwa na hivyo kumfanya mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kujikumbusha au kukumbuka atakapokuwa akifanya mtihani.

Haifai kwa mwanafunzi kurejea nyumbani na kufunika madaftari bila kujikumbusha au kurudia siku mbili baada ya kufundishwa, kufanya hivyo kunaweza kutoa nafasi kwa akili kuyatupa aliyofundishwa kutokana na wingi wa masomo au mambo aliyoelekezwa kwa siku mbili au wiki nzima.

-Kufanya uchambuzi

Ni wajibu wa mwanafunzi kufanya uchambuzi wa notisi zake za shule kwa kuandika mchanganuo wenye maneno machache ya msingi kwenye daftari jingine au karatasi. Kufanya hivi kutamsaidia kupunguza wingi wa maneno ya kuhifadhi akilini hasa kwa wanafunzi wa ngazi za chini ambao wengi wao hutumia mbinu za kukariri ambazo ni hatari kwa kusahau haraka.

Kwa mfano, wanafunzi anapofundishwa kuhusu ubadhilifu wa pesa ndani ya Benki Kuu  ya Tanzania �BoT� kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje maarufu kama EPA na kupewa takwimu na mlolongo mzima ulivyokuwa, anachotakiwa kufanya yeye ni kunyambua mambo ya msingi ambayo yatamuongoza katika kujibu maswali, kama kuwajua wahusika, mwaka wa skendo, kiasi kilichoibwa na kilichorudiswa.

Mambo hayo machache akiyafahamu yatamfanya awe na uwezo wa kulielezea jambo hilo kwa kina mbele za watu na kuonekana mwenye ufahamu wa kutosha, lakini pia atajihakikishia uwezo wa kukabili jaribio au mtihani wo wote utakaokuja na swali la EPA.

-Kujipima uelewa

Kumsikiliza mwalimu, kurudia notisi na kufanya uchambuzi kunaweza kusitoe picha sahihi juu ya uelewa wa mwanafuzni katika yale anayosoma pamoja na uwezo wake wa kukumbuka aliyojifunza. Mwanafunzi ili ajipime kama akili yake imenakiri vema anatakiwa kutenga siku ndani ya wiki kwa kujitungia mitihani kutoka kwenye daftari zake, kuifanya na kujisahihisha mwenyewe.

Hii itampa mhusika ufahamu wa kujua ni eneo gani kaelewa zaidi ya jingine na hivyo kujituma zaidi sehemu ambayo hajaelewa kwa kuuliza tena kwa mwalimu au kwa wenzake ambao anadhani wana ufahamu mkubwa kuliko yeye. Ni vibaya kusoma bila kujipima uwezo. Itapendeza kama wanafunzi watakuwa wakifanya mitihani ya kujipima kwenye vikundi kila wiki.

 -Kukuza ufahamu
Ziko njia nyingi za mwanafunzi kukuza ufahamu wake lakini muhimu zaidi ni kusoma vitabu, kusikiliza habari kupitia vyombo vya mbalimbali na kushiriki katika mijadala ya wazi yenye kujadili masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Mwanafunzi hawezi kukuza ufahamu kama hajui masuala ya jamii yake, siasa za ulimwengu na hali ya uchumi wa ndani na nje na hayo yote yanapatikana kwa kusoma. Jambo jingine la msingi ni kwa mwanafunzi kuepukana na aibu ya kujieleza mbele za watu. Njia pekee ya kuhifadhi kumbukumbu ya kile alichosoma na kuwa na tabia ya kuwaeleza wengine.

Kwa mfano, kama mwanafunzi atakuwa amefungua mtandao wa inteneti na kusoma habari za kupanda kwa uchumi wa Marekani anatakiwa awaeleze wenzake alichojifunza, vivyo hivyo atakaposoma vitabu au kutazama filamu. Kujua jambo na kutokulitenda ni ujinga sawa na mtu ambaye hajui kabisa. Aibu ya kuzungumza mbele za watu haifai ni vema mwanafunzi akajiamini na kujizoeza kueleza anachokifahamu mbele za watu.

Wednesday, November 7, 2012

JE WAJUWA KUWA ASALI NA LIMAU ZINAPUNGUZA UNENE NA UZITO

KUPUNGUZA UNENE KWA KUTUMIA ASALI NA LIMAU/NDIMU

Asali na limau
Diet ya asali na Limau diet inasaidia kupunguza tatizo la uzito mkubwa/unene . Obesity ni hali ya mwili unapokuwa unamafuta mengi kupindukia na mafuta hujitokeza katika tishu za mwili, kwenye moyo, figo, ini na viungo kama vile nyonga, magoti na vifundoni na hivyo, watu wenye uzito mkubwa pia  ni rahisi kukabiliwa na magonjwa kadhaa kama kisukari, shinikizo la damu, arthritis, ini na nyongo ya kibofu cha mkojo kupata matatizo.

Asali ni njia nzuri ya asili ambayo unaweza kutumia kwa ajili ya Obesity na kupunguza kwa viwango vya cholesterol mwilini. 

Kufunga/Fasting kwa asali na lemon-juisi, chakula alkali, ina manufaa katika matibabu ya Obesity bila kupata hamu ya kula.

Kwa ajili ya tiba hii ya asili, changanya kijiko kimoja cha asali mbichi (unheated) na vijiko viwili vya maji ya limau au ndimu katika glasi ya joto au maji vuguvugu (si kuchemsha maji!).

Kunywa mchanganyiko huu wa asali na limau/ndimu kila unapoamka asubuhi tumbo likiwa tupu. Pia unatakiwa kunywa mchanganyiko huu mara baada ya mlo kubwa na vyakula vya mafuta, hii inarahisisha kwenye digestion .

Ukiendelea na tiba asili ya kupunguza uzito unatakiwa kuzingatia kanuni kama vile kutengeneza tabia katika milo unayokula pia kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.

Barack Obama aibuka mshindi

Rais Obama na wafuasi wake
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama ameshinda katika majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Mamilioni ya watu walijitokeza kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita

Tuesday, November 6, 2012

CAF: orodha fupi ya wachezaji bora soka

SPORTS/MICHEZO
 
CAF
Wachezaji bora zaidi wa soka barani Afrika watatangazwa na CAF tarehe 20 Desemba

CAF imetangaza orodha fupi ya majina ya wachezaji ambao wamo katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora zaidi barani Afrika.
Mshindi wa mwaka jana, Yaya Toure, anaongoza katika orodha hiyo yenye majina ya wachezaji 10, waliochaguliwa kutoka orodha ndefu ya wachezaji 34.

Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Manchester City, ni kati ya wachezaji wanne wanaozichezea timu za Uingereza ambao huenda wakapata tuzo hiyo ya mwaka 2012.

Kiungo cha kati wa Chelsea, John Obi Mikel, mshambulizi wa Arsenal, Gervinho, Demba Ba wa timu ya Newcastle, ni kati ya wachezaji wengine wa ligi kuu ya Premier ambao wanawania tuzo hiyo.

Katika orodha hiyo, kuna wachezaji wengine ambao waliwahi kucheza Uingereza mwaka 2012.

Wachezaji hao ni aliyekuwa kiungo cha kati wa Arsenal, Alexandre Song, na ambaye sasa huichezea Barcelona ya Uhispania, na mshambulizi wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, ambaye anaichezea klabu ya China, Shanghai Shenhua.

Chris Katongo ni mchezaji wa pekee kutoka timu ya Zambia iliyoibuka mshindi katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mchezaji wa Morocco, Younes Belhanda, yumo katika orodha hiyo, kwa juhudi zake mapema mwaka huu, katika timu ya Ufaransa ya daraja ya kwanza, Montpellier.

Wanaowania tuzo hiyo, watapunguzwa hadi kufikia watatu, katika wiki ya mwisho ya mwezi Novemba.

CAF vilevile ilitangaza orodha fupi ya wachezaji watano, ambao wana nafasi ya kupata tuzo la mchezaji bora barani Afrika, kwa wachezaji ambao hucheza kandanda yao barani Afrika.

Katika ordha hiyo ni pamoja na Mohamed Aboutrika, kiungo cha kati kutoka Misri, na aliyecheza katika mechi ya Al Ahly ya klabu bingwa dhidi ya Esperance ya Tunisia, mchezo uliokwishwa kwa sare ya 1-1 siku ya Jumapili.

Tuzo hizo, ambazo zitakuwa pia ni kumpa zawadi kocha bora zaidi wa mwaka, na klabu bora zaidi mwaka 2012, zitatolewa kwa washindi tarehe 20 mwezi Desemba, katika ukumbi wa Banquet, katika ikulu ya rais, katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Malawi yasitisha sheria ya ushoga

Rais wa Malawi Joyce Banda
Serikali ya Malawi imesitisha rasmi mswaada wa sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.
Polisi wameagizwa kutowakamata watu wanaojihusisha nayo, mpaka hapo uamuzi utakapotolewa wa kuendelea na sheria hiyo au la.
Mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi yamepigwa marufuku na kutolewa kifungo cha miaka hadi kumi na minne jela kwa wanaokamatwa kushiriki.
Baadhi ya viongozi wa kimagharibi wametishia kusitisha kuzipa msaada nchi za Afrika ambazo zinakataa kutambua haki za mashoga
Ushoga ni haramu katika nchi nyingi za Afrika na linasalia kuwa swala tete katika jamii nyingi za Afrika zenye kukumbatia maadili ya kiafrika.
Mmoja wa viongozi wa kijamii wenye ushawishi mkubwa, bwana Kaomba, amiomba serikali kutoruhusu bunge kubadili sheria zake kuhusu ushoga. ''Hii ni kinyume na maadili'' alisema kiongozi huyo.
Mwandishi wa BBC mjini Blantyre Raphael Tenthani, anasema kuwa kusitisha kwa muda sheria hiyo, itawaudhi sana watu wengi hasa viongozi wa kidini pamoja na watu kwa ujumla.
Mnamo mwaka 2010, wanaume wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu hadharani baada ya kusema kuwa wataoana.
Kesi hiyo ilivutia sana kero kutoka kwa jamii ya kimataifa na hata kusababisha baadhi ya wahisani kusitisha msaada kwa nchi hiyo, na ikawa pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.
Rais wakati huo akiwa , Bingu wa Mutharika - aliwasamehe wanaume hao kwa misingi ya kibininadamu ingawa alisisitiza kuwa ni kinyume na maadili ,na tamaduni za kiafrika na hata sheria za nchi.
Hata hivyo rais Joyce Banda, aliyemrithi Bingu aliwaambia wabunge kuwa anataka kubatilisha sheria hiyo na kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.

Uchaguzi waanza nchini Marekani

Wagombea Barack Obama na Mit Romney
Rais Barack Obama ametoa wito wake wa mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa hadhara mjini Iowa huku wamarekani wakijitokeza kupiga kura kuamua ikiwa atapata muhula wa pili au mpinzani wake Mitt Romney ndiye atachukua usukani katika ikulu ya White House.
Mwandishi wa BBC ambaye yuko kwenye kampeini ya Romney, anasema kuwa hizi dakika za mwisho ni kuhusu kuwashawishi wapiga kura katika uchaguzi huu wenye ushindani mkali
Kura za kwanza zimepigwa katika jimbo la New Hampshire, ambako inaarifiwa Obama na Romney wamepata kura tano kila mmoja kati ya kura kumi. Kura hizi hazitokani na wapiga kura kwa ujumla bali watu maalumu ambao huteuliwa kupiga kura katika kile kinachojulikana kama Electoral village.

Monday, November 5, 2012

Je wajuwa ufumbuzi wake Linalokuhuzunisha si tatizo kubwa, unajitesa bure!

Lord Byron mwanafalsafa na mshairi mahili wa Uingereza aliwahi kuandika maneno haya “The great art of life is sensation, to feel that weexist even in pain.” Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba Sanaa kubwa ya maisha ni maono, kuhisi mambo ni madogo hata katika maumivu. Kwangu mimi nimechukulia usemi huo kama somo la kuwafundisha watu wanaolia kwa matatizo ya aina mbalimbali.
Nafahamu kwamba katika maisha ya kila siku hayakosekani mambo ya kuumiza. Sina shaka kuugua, kufiwa, kukosa chakula, kusalitiwa katika mapenzi, kudhurumiwa, kufilisika na kufutwa kazi ni mambo ambayo huzaa huzuni na machozi miongoni mwa watu wengi. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba tunalia au kuhuzunika kwa sababu matatizo yetu ni makubwa au tumekosa kufahamu kanuni ya maisha aliyoitoa Lord!
 Hebu tujiulize ni wangapi tunahuzunikia mishahara midogo tunayolipwa makazini mwetu? Je katika huzuni hizo tulishawahi kuwaza kwamba kuna binadamu wengine hawana kazi na wanahangaika kutafuta shilingi mia tano kwa kuuza mihogo na karanga kwenye kona za mitaa huku wakiwa juani?. Kama hao wapo ukubwa wa tatizo la kukosa kazi unaotuliza kila siku uko wapi?
 
 Uko wapi ukubwa wa tatizo la kutokuzaa wakati kuna waliozaa na watoto wote wakafa. Kimsingi uwiano wa shida na uhimili wake unaopatikana baina ya mtu na mtu, kamwe sifa ya huzuni hailetwi na ukubwa wa tatizo, isipokuwa ni kukosekana kwa sanaa ya kuishi, yenye maono na hisia za kupunguza mambo makubwa kuwa madogo.
 Katika hisia, mwanadamu hawezi kuzuia machozi ya furaha au huzuni yasitoke, maana nilisoma katika Biblia kuwa hata Yesu alilia pale alipopata habari kwamba rafiki yake Lazaro amekufa. Lakini pamoja na kilio hicho hakusita kuita maono na kuona kwamba tatizo lililokuwa mbele yake lilikuwa dogo, akaamua kuchukua hatua ya kuwaagiza wanakijijini waliondoe jiwe na yeye kutajwa kumfufua kwa kutumia uwezo wake (Haya ni ya kidini siyajadili sana katika mada hii).
 Ifahamike kwamba kila mwanadamu ana uwezo wake wa kufanya, zaidi ya tatizo analokutana nalo, lakini uwezo huo hauji kama sanaa ya maono na ‘udogoshaji’ matatizo hayajapewa kipaumbele. Kuna watu wanalia kila siku kwa kuhitaji utajiri, lakini hawafikii malengo kwa sababu wanaona umasikini ni jambo kubwa na kuufikia utajiri ni jambo kubwa pia.
 Kwa mujibu wa utafiti wa William Frey mkemia na Mkurugenzi wa Kituo cha Dry Eye and Tear Reseach cha Minneapolis, watu hulia katika makundi matano tofauti ambayo ni: Wenye kujawa na huzuni  zinazosababishwa na matatizo ya kimaisha 49%.
Wanaolia kwa furaha ni alisilimia 21, hasira 10% na huruma 7%, huku wenye wasiwasi wakilia kwa kiwango cha asilimi 5 juu ya wenye hofu wanaolia kwa asilimia 4%.
Lakini, pamoja na kuwepo kwa makundi hayo sita, mwanadamu mwenyewe anatajwa kuwa na uwezo wa kuyabadili maono yake kwa kila kundi na kupata matokeo tofauti kabisa, kwani hasira ikipunguzwa kwa kuona kichocheo kilichojaza hasira ni kidogo pumzi hushuka na mtu hujiona mwenye utulivu tofauti na mwanzo.
Vivyo hivyo, kwa anayelia kwa huzuni, huruma, wasiwasi na hofu! Kwa mantiki ile ile hakuna haja ya kuhuzunika kwa kiwango cha juu, wakati kuna kiwango cha chini cha kujiweka huru, nacho ni cha kutazama mambo makubwa kama madogo yasiyodumu na kwamba saa, siku, miaka michache  ijayo yatapita. Jiulize hapo ulipo msomaji wangu ni kitu gani kinakuliza? Fahamu kwamba hulii au kuhuzunika kwa sababu matatizo ni makubwa, bali umekosa ufahamu wa maono.
Hebu chukua jukumu la kudharau shida zako kwa kujilinganisha na wengine ambao bila shaka wanakuzidi matatizo. Fanya hivyo kila unapokabiliwa na tatizo, usilione tatizo ni kubwa kwa takwimu, lichukulie kuwa ni dogo kisha uanze kulishughulikia, utaona linamalizika kwa ushindi mkubwa. Kamwe usijaribu kulitatua ndani ya maono yanayolikuza, hutapata matokeo mazuri.
Ukiwa ni umasikini uone ni mdogo, kutokuzaa, kukosa kazi, kuteswa na mume au mke na matatizo yote yatakayokukuta katika maisha yako yaone ni madogo kisha tumia nguvu zako zote kuyakabili nina hakika utayashinda kirahisi.
 Lord Byron aligundua kanuni aliyoipa jina la Byronic Hero, ambayo ilikuwa na misingi ya kuishi kwa maono na  kupunguza ukubwa wa mambo kwa kutumia fikra. Wengi walipata mafanikio ya kutisha. Jaribu kupunguza matatizo, badala ya kuyakuza kwa kuona hayawezekani kutatuliwa, utaona maajabu. Tambua kuwa tatizo lako si kubwa bali unalikuza katika mawazo yako, kwa kuwa wapo wenye matatizo makubwa zaidi yako na hawalii kama wewe.

Sunday, November 4, 2012

BRIGITTE ALFRED NDIE REDDS MISS TANZANIA 2012

HATIMAYE kile kitendawili cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds Miss Tanzania 2012, kimeteguliwa usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya Mrembo kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Brigitte Alfred kutwaa taji hilo.

Brigitte ambaye nyota yake katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza kung’aa tangu Kitongoji cha Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza na Baade kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni amedhihirisha ukali wake baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo kutoka Kanda mbambali.

Mpinzani mkubwa wa Brigitte katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda ya Ziwa ambaye nae alianza kuwika baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa Mara na baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa, Eugene Fabian.

Enagene alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo Brigitte ameondoka akiendesha gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi Milioni 8.

Nafasi ya tatu ilikwende kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss Temeke 2012, Edda Sylvesta huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza, Happyness Daniel.
 Brigitte Alfred akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi na kuwabwaga washiriki wenzake 29.
Brigitte Alfred (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael
Mshindi wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili, Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo. Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene anatoka Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa huku Edda ni Miss Kigamboni na Kanda ya Temeke.
 
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatu5 bora ya Redds Miss Tanzania 2012, kutoka kushoto ni Brigitte Alfred, Eugen Fabian, Happyness Daniel, Edda Sylvester na Magdalene Roy wakipozi kwa picha.

Washiriki wakicheza show ya ufunguzi wakati wa kuanza kwa shindano hilo.
Wageni mbalimbali na wadau wa tasnia ya Urembo nchini Tanzania wakifuatilia shindano hilo kwa umakini ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la Ngoma za Asili la Wanne Stars likitoa burudani kwa wageni.
Balozi wa Tanga Beach Resort, Happyness Rweyemamu akijinadi jukwaani na vazi lake la ubunifu.
Mshiriki Flavian Maeda kutoka Kitongoji cha Kurasini na Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam akipozi jukwaani na vazi la ubunifu.
Fina Recatus akipita jukwaani na vazi la ubunifu. Fina ni Balozi wa Tanga Beach Resort 2012.
Naomi Jones nae akipita jukwaani na vazi la ubunifu
Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Kudra Lupato nae alikatiza jukwaani na kunaswa na Camera ya Father Kidevu Blog.
 Brigitte akipozi na vazi lake la Ubunifu
 Msanii kutoka THT Rachel nae alipata fursa ya kuonesha kipaji chake na kudhihirisha wazi kuwa yeye ni Mrithi wa Ray C kwa sauti na kiuno Bila mfupa.


 
Japokuwa ni ufukweni lakini chini walivaa hivi, maana shindano la Dunia ndivyo inavyokuwa
 Warembo mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la ufukweni.
Warembo mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la ufukweni.
 Warembo mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la ufukweni.
 Warembo mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la ufukweni.
Mdau Kabula nae hakukosa na haopa akiwajuza waliobaki nyumbani kinachojiri. Siunajua tena mambo ya Tanesco baadhi ya mitaa na mikoa ilikuwa giza tu.
 Juma Pinto kutoka Jambo Concerpt (kulia) na William Malecela 'Lemutuz'  nao walikuwepo.
Waongoza Show nzima ya Redds Miss Tanzania 2012, Jocate Mwegelo 'Kidot' na Taji Liundi wakiwajibika.
Picha na Clever