NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, January 29, 2013

BONANZA LA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA LAMALIZIKA SALAMA NA LAPENDEZA SANA

MGENI RASMI MKUU WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMANDA DIWANI AKIFUNGUA BONANZA HILO
MWENYEKITI WA MICHEZO HOSPITALI YA RUFAA MBEYA CHRISTOPHER MWAKUBOMBAKI AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KUFUNGUA BONANZA HILO AMBALO LIMESHIRIKISHA WATUMISHI WA SERIKALI  TOKA KATIKA OFISI MBALI MBALI MKOANI HAPA
TIMU MBALI MBALI ZA SERIKALI ZILISHIRIKI BONANZA HILI HAPA WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI
MGENI RASMI AKISALIMIANA NA TIMU YA DAMU SALAMA
HAPA AKISALIMIANA NA TIMU YA OFISI YA MKUU WA MKOA  MBEYA
TIMU YA OFISI YA MKUU WA MKOA MBEYA
TIMU YA DAMU SALAMA MBEYA
MASHINDANO YA KUKUNA NAZI KWA WANAUME YALIKUWEPO
MASHINDANO YA KUNYWA SODA KWA CHAPATI
KAMANDA DIWANI AKIFURAHIA MICHEZO MBALI MBALI KATIKA BONANZA HILO
DUU HII KALI MZEE ANAONYESHA UMAHILI WAKE WA KUCHEZA SEBENE
WATOTO NAO WALIKUWEPO HAPA NI KIDUKU TU
JAMAA BAADA YA KUSHINDWA KATIKA SHINDANO LA KUKUNA NAZI AKAAMUA BORA ALE MACHICHA YA NAZI HII KALI
MASINDANO YA KUVUTA KAMBA KWA WANAWAKE
MASHINDANO YA KUVUTA KAMBA KWA WANAUME
KIDUKU KWA WATOTO KINAENDELEA
MPIRA WA MIGUU
NYAMA CHOMA ILIKUWEPO UWANJANI HAPO
MASHINDANO YA KUKIMBIA NA GUNIA
TBL NAO WALIKUWEPO UWANJANI HAPO
WATOTO NAO WAKIVUTANA KWA KAMBA
MGENI RASMI TOKA OFISI YA MKUU WA MKOA MBEYA COSTANTINE MUSHI AKIFUNGA BONANZA HILO
PICHA NA MBEYA YETU

FLAVIANA MATATA ATWAA TUZO YA MWANAMITINDO BORA WA AFRIKA 2012

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ambaye ameng’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super Model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).
Tuzo aliyojishindia mwanamitindo Flaviana Matata.

NI MFANO WAKUIGWA:UMOJA WA BAJAJI MBEYA WATEMBELEA WATOTO YATIMA SIMIKE NA KUTOA MSAADA

Umoja wa Vijana  waendesha Pikipiki za magurudumu matatu Mkoani Mbeya umeamua kuzindua mpango wa  kutembelea  watoto yatima  na kutoa misaada  kutokana na faida wanayoipata baada ya kusaijili umoja  wao na kuchana  na kutumisha  kwenye maandamano ya kisiasa  na kusababisha vurugu Jijini . Hapa umoja huo ukitoa msaada wa sukari mchele chumvi na madaftari kwa watoto yatima wa simike mbeya
Hapa wanaumoja huo wa bajaji mkoani mbeya wakimkabidhi kijana Frank Musa ada ya awamu ya kwanza kwani kijana huyo amefauru kwenda shule ya sekondari itigi lakini alikosa ada ya kwenda shule hivyo umoja huo umetoa kiasi cha shilingi 40,000/ za kuanzia ili aanze masomo
kulia nia mama janeth Njenga yeye amejitole kumsaidia mtoto Franki kwa ada na matumizi yote ya shule mpaka atakapomalisha elimu hiyo ya sekondari 
Wanaumoja hao wa bajaji wametoa msaada kwa watoto hao yatima wenye dhamani ya shilingi 250,000/
Hapa watoto hao wakiushukuru umoja wa babaji mkoa wa Mbeya kwa kuwakumbuka na kuwajali katika chakula
Mama Anna Kasile yeye ndiyo anaewalea watoto hao akiwashukuru wanaumoja hao kuja kuwaona na kutoa msaada kwa watoto hao


“sisi ni vijana ambao tumeamua kuwa wajasiliamali  ambapo tumejipanga kwa ajili ya kuinuana kiuchumi  lakini kutokana na faida tunayoipata  tumeamua kuwa tutakuwa tunaitumia kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima  katika vituo vilivyopo Mbeya  na tutazindua mpango huu mwishoni mwa mwezi.”walisema wanaumoja hao wa Bajaji mkoani Mbeya.
Picha na Mbeya yetu

Sunday, January 27, 2013

Uwanja wa ndege wa Gao wakombolewa

Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa inasema kuwa jeshi linaloongozwa na Wafaransa limeuteka uwanja wa ndege wa mji wa Gao, ngome ya wapiganaji ya Kiislamu kaskazini mwa Mali.
Wanajeshi wa Ufaransa wakikaribia Gao, Mali
Daraja muhimu piya wameiteka.
Mapigano yanaendelea.
Gao ni mmoja kati ya miji mikuu mitatu ya kaskazini mwa Mali iliyotekwa na wapiganaji mwaka jana.
Siku ya Ijumaa wanajeshi wa Mali na Ufaransa waliukomboa mji wa Hombor kilomita 160 kutoka Gao.
Umoja wa Afrika umesema unataka kuzidisha idadi ya wanajeshi wa kuweka amani nchini Mali, na imeomba nchi zanachama kujitolea kwa wanajeshi zaidi katika wiki zijazo.
Piya umeuomba Umoja wa Mataifa usaidie kuwasafirisha wanajeshi hao hadi Mali.

Mateka waachiliwa huru Niger Delta

Mabaharia watano wa India waliotekwa nyara mwezi uliopita nje ya mwambao wa Nigeria wameachiliwa huru, kwa mujibu wa kampuni yao.
Jeshi la Nigeria likipiga doria katika Niger Delta

Mabaharia hao wa meli ya mafuta walitekwa wakati watu waliojihami na silaha tele walipoingia kwa nguvu ndani ya meli yao, SP Brussels, katika eneo la mafuta la Niger Delta kusini mwa Nigeria.
Taarifa ya kampuni ya meli hiyo, Medallion Marine, ilieleza kuwa mabaharia hao ni wazima lakini haikueleza iwapo ililipa kikombozi.

Friday, January 25, 2013

Jaji wa mahakama kuu Kenya atekwa nyara [video]

nzioka1 150x150 Jaji wa mahakama kuu Kenya atekwa nyara [video]
Jaji wa mahakama kuu Grace Nzioki, anayeongoza jopo linalochunguza mauaji ya Tana Delta alitekwa nyara jana usiku na ripoti ya uchunguzi wake iliotarajiwa kutolewa hapo kesho kuibiwa.
Majambazi hao walimteka nyara jaji huyo nyumbani kwake na kisha kumpora vifaa kadhaa ikiwemo kipakatalishi, au ukipenda laptop iliokuwa na ripoti ya uchunguzi wa mauaji ya tana.


Je, tunashughughulikia ufumbuzi wa tatizo la elimu nchini?

Shughuli za  kila siku, kwa namna moja au nyingine, zinakupa taswira ya “maendeleo” (neno sahihi katika kipindi hiki ni “mmomonyoko”) wa sekta ya elimu Tanzania. Nadhani wale ambao wako kwenye michakato ya usaili na shughuli kadha wa kadha za kutafuta na kuajiri vijana ambao wamehitimu hatua fulani ya elimu, wako katika nafasi nzuri kujua kama elimu aliyopata mhusika imempa nyenzo za kukabiliana na changamoto za taaluma au kazi fulani na maisha kwa ujumla.
Bahati mbaya sio wote tuna ndugu, jamaa na marafiki ambao kazi zao zinawapa mwanya wa kuona kinachozalishwa na mfumo wa elimu nchini. Hata hivyo, wakati tunaanza kuelewa kinachoendelea kupitia kwao tunakuwa tumechelewa. Tumechelewa sana. Kwa sababu tunakuwa tayari tumeshapoteza kizazi; tunakuwa tunaangalia matokeo ya makosa yaliyokuwa yakifanywa kwa kipindi kifefu.
Juhudi za asasi kama Twaweza/Uwezo na Tamasha Vijana, kufanya tafiti za kina na kuonesha wapi mapungufu yalipo hasa, ni nzuri na zinahitaji heko badala ya kuzikebehi kwa ‘majibu ya kisiasa’. Zinapaswa kutumiwa katika uundaji na mabadiliko ya mitaala na mfumo mpya wa elimu unaoakisi mwelekeo wa ulimwengu huu wa leo.
Pia, napenda kuchukua fursa hii kuhoji: Kwa nini hatukuwa na vigezo vya kutuambia mwelekeo wa elimu katika ngazi mbalimbali? Yaani, hizi ripoti zingetakiwa ziwe zinatoka angalau kila baada ya miaka kadhaa tangu siku sekta ya elimu na wizara husika zilipotengemaa. Hakuna mtu aliyewahi kufikiria hilo? Kama nilivyosema awali, ni dhahiri kuwa mapungufu tunayoyaona sasa hivi ni matokeo ya mapungufu na makosa ya muda mrefu.
Au bado tunaamini ya kwamba mitihani ya mwisho pekee ndio kipimo thabiti cha elimu?
Kwa upande mwingine, wengi wetu — mtu mmoja mmoja — hatuna hulka ya kufuatilia maendeleo ya wadogo zetu, ndugu zetu na watoto wetu mara kwa mara. Wengi tunasikia malalamiko kutoka kwa wengine, lakini hatushtuki hadi pale watoto wetu wanapopata madaraja ya chini kabisa kwenye mitihani ya mwisho (hasa ya kidato cha nne na sita).
Kama umefanya utafiti au umesoma ripoti za tafiti mbalimbali, utakubaliana nami kuwa hatuwatendei haki vijana ambao wapo mashuleni sasa hivi. Sehemu kubwa hawaandaliwi kukabiliana changamoto za dunia ya sasa.
Wapo wenye mawazo tofauti, kuwa tunapiga hatua; vijana wengi zaidi sasa hivi “wanapata elimu”. Bahati mbaya ulimwengu wa leo hauna mipaka. Nchi yetu sio kisiwa. Vijana wa leo hii wanashindana na vijana kutoka kona mbalimbali za dunia. Kwa mantiki hiyo, kama wengine wanaendelea kwa kasi kubwa kuliko sisi, basi sisi tunarudi nyuma!
Mapungufu tunayoyaona ni mengi, lakini wakati waliopo kwenye sekta ya elimu wakijaribu kuyatambua na kuondokana nayo, ni wajibu wetu — mtu mmoja mmoja — kujaribu kufanya kila tunachoweza kuokoa wengi kadri tunavyoweza, kwa kuwa mabadiliko yanayotakikana yatachukua miaka mingi.
Kwa mtazamo wangu, donda ndugu ni sisi kama jamii kwa ujumla kutoheshimu taaluma ya ualimu. Hatujaweza kuwavutia wengi wanaofanya vizuri mashuleni kuingia kwenye fani ya ualimu. Zaidi ya hayo, walimu wachache tulionao hawapewi motisha ya aina yoyote ile.
Ukiacha upungufu wa zana za kufundishia, n.k., kuna mdahalo mzito wa muda mrefu wa lugha ipi itumiwe (sekondari na vyuoni): Kiswahili au Kiingereza?
Tukumbuke kuwa kwenye taaluma yoyote ile, kitu muhimu ni ujenzi wa “msingi”. Hapa namaanisha, kwa mfano kwenye sayansi, “msingi” ni tabia ya udadisi, jinsi mtu anavyofikiri na anavyokabili tatizo fulani. Katika hatua ya ujenzi wa tabia ya udadisi, awali ya yote mwanafunzi anapaswa kuwa na ufahamu wa mambo yanayomzunguka. Na udadisi au ufahamu huambatana na ujenzi wa taswira fulani kichwani.
Je, elimu inamsaidia mwanafunzi kuwa mdadisi? Lugha inayotumiwa inarahisisha zoezi la kujenga msingi, au tabia ya udadisi?

Unapomfundisha mwanafunzi wa kidato cha kwanza kuhusu mwendo kasi, atakuelewa vizuri ukitumia mifano ya gololi, ndulele au billiards? Ukitumia mfano ya billiards pekee, mwanafunzi atatumia nguvu nyingi kukariri (kwa kuwa hajui billiards ni nini) badala ya kuanza kujenga taswira na uelewa wa mwendo kasi.
Mabadiliko ya matumizi ya lugha kwenye masomo kutoka darasa la saba hadi kidato cha kwanza huathiri wanafunzi wengi mno. Wapo wachache wanaouruka hiki kihunzi bila matatizo, ila wengi hupata msaada kwa namna moja au nyingine. Wenye bahati tulikuwa na walimu wenye uwezo wa kutuelezea vizuri kwa Kiswahili rahisi kila palipohitajika. Wenye bahati zaidi tulikuwa tuna wazazi ambao waliweza kutusaidia kujenga taswira ya vitu kama electron kwa kutumia Kiswahili.
Bahati mbaya wengi hawana hizo bahati, hivyo sehemu kubwa ya juhudi zao huelekezwa kwenye kukariri maelezo ya Kiingereza bila kuelewa. Hii ni moja ya vyanzo vya misingi mibovu ambayo huja kuanza kuota nyufa wanafunzi wanapofika ngazi za juu.
Kama moja ya njia ya kutatua tatizo la matumizi ya lugha ya Kiingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao bado hawajakimudu vizuri, kuna kitabu kipya kinachoitwa “Enjoy Chemistry, Furahia Kemia” kilichochapwa hivi karibuni. Kitabu hiki kimeandikwa maalumu kwa ajili ya wanafunzi wanaozungumza lugha ya Kiswahili wanaotaka kujifunza Kemia,
na wakati huohuo wapate kumudu lugha ya Kiingereza ili kufanya majaribio na mitihani ya kufuzu elimu ya sekondari.

Kwa upande wa uhaba wa vifaa vya maabara, kitabu hiki kina maelezo ya kufanya majaribio ya Kemia ambayo yatamwezesha mwanafunzi kujifunza mwenyewe. Maelezo ya kitabu yanasema: “Kwa kuwa shule nyingi za sekondari zina uhaba mkubwa wa vifaa vya maabara maalumu kwa ajili ya somo la sayansi lenye majaribio mengi kama ilivyo Kemia, kitabu hiki pia kinaweka mkazo kwenye mbinu ya fanya-mwenyewe. Mbinu hii itawasaida wanafunzi kuelewa Kemia kwa kina na wakati huohuo kulifurahia somo. Njia hii itawapatia wanafunzi walio kwenye shule zisizo na vifaa vya kutosha fursa sawa ya kufanya majaribio ya Kemia kama waliyonayo wanafunzi walio na bahati ya kuwa katika shule yenye vifaa vingi vya maabara.”
Ni muhimu kusisitiza kuwa kitabu hiki hakibadilishi wala kupindisha mitaala ya Kemia nchini.
Wakati wadau wa elimu wakiendelea kufanya midahalo na mijadala ya mabadiliko katika sekta ya elimu na mitaala, juhudi kama hizi zinatia moyo kwa kuwa naamini zitasaidia kuokoa vijana kadhaa.
Tafadhali, pitia kitabu hiki kisha tupe maoni yako hapo chini. Pia, wataarifu na wengine na wakaribishe kupiga kura juu ya lugha gani itumiwe kufundisha wanafunzi wa ngazi ya sekondari.
Imetolewa na Mzumbe

Je unajuwa nini kinaendelea katika Tume ya Katiba:Jijuze sasa




Karibu Tume ya Mabadiliko ya Katiba 
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83. Tume ina Wajumbe 32 ikiongozwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti. Tume ina Sekretarieti inayoongozwa na Katibu na Naibu Katibu.
 Kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, jukumu kuu la Tume ni kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, jukumu la Sekretarieti ni kuiwezesha Tume kufanya kazi zake.

  Kuhusu Tume

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83. Jukumu kuu la Tume ni kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu kupatikana Katiba Mpya.
Tume pia inatekeleza majukumu mengine yafuatayo:-
a)           Kuandaa na kuendesha programu za kuelimisha umma;
b)           Kuitisha na kusimamia mikutano na mabaraza ya katiba;
c)           Kutathmini na kuchambua maoni ya wananchi;
d)           Kupitia na kuchambua michango, mawazo, maoni, taarifa na mapendekezo yaliyokusanywa na
              kufanyiwa tathmini siku za nyuma;
e)           Kupitia na kutafiti usahihi na ulinganifu wa masharti ya kikatiba yanayohusu mamlaka ya wananchi,
              mifumo ya kisiasa, demokrasia, utawala wa sheria na utawala bora;
f)            Kumuomba mtu yeyote kufanya majadiliano na Tume au kuwasilisha nyaraka kuhusu mabadilioko ya Katiba;
g)           Kuchapisha Rasimu ya Katiba katika Gazeti la Serikali na magazeti mengine ili kutoa fursa kwa wananchi kusoma
              na kutoa maoni zaidi kwa Tume kupitia mabaraza ya Katiba;
h)           Kutayarisha na kuwasilisha ripoti kwa kila hadidu ya rejea; na
i)            Kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalum la Katiba