Mkutano uliofanyika AICC Arusha |
Ndugu zanguni mtaniwia radhi kwa kusema haya najuwa ni kipindi kirefu sana nimekaa kimya ni kutokana na hali tu na mambo kuwa mengi, Ila nikaona sio vyema napopata nafasi yakushirikiana nanyi katika mambo kadhaa hasa ya maisha ni vyema.Hivi Hii Serikali yetu haina ya kufanya inawaza namna ya kuwaibia wananchi wake kila siku bila kuwaboreshea maisha wananchi wake.Hebu tujiulizeni kodi wanazokatwa wafanyakazi zinawasaidia nini hao wafanyakazi na bado pia bado Nchi inaenda kukopa nchi za nje, Bado haitoshi inakopa kwenye mifuko ya jamii kama NSSF na mingineyo na bado hairudishi.Hivi tunakwenda wapi,Ikaona haitoshi sasa inataka kuzui wafanyakazi hao wanaokatwa kodi na pia kuchangia mifuko ya jamii wasipate hela zao hadi miaka 55 wakati kwa mtanzania wa kawaida anaishi miaka 47 hadi 49 sasa hiyo miaka 55 mfanyakazi huyo atachukuwa mafao yake akiwa kaburini kama sio uwizi ni nini tena sio uwizi ni ujambazi mkubwa. Hii imenitoka akili baada Mbunge wa Kigoma Mh Zitto nae kutaka mfuko huo uchukuliwe akipingana na sera ya Mbunge mwenzie toka Chama cha Demokrasia na maendeleo Mh John Mnyika kutaka watu wawewanapata fedha zao kila waachapo kazi au kusimamishwa.Kutoka na hiyo imenijenga kwamba wanasiasa wote ni sawa hakuna anatoka chama gani wala ni nani.Kuna jambo limenitoa imani kabisa na viongozi wetu, hebu tuchukue hii kama changa moto wote najuwa tunalijuwa kundi la wasanii wa bongo flavor linalojulikana kama leka tutigite kutoka Kigoma likiwa chini ya Mh huyo, Kama mheshimiwa huyu haja pata kitu kidogo kuwakandamiza wananchi ni nini.Kapata nafasi hiyo na kaliambia kundi lake hilo lifanye wimbo kwa ajiri ya mifuko ya jamii hapa wewe unakuwa na imani na viongozi hao,Sijatoa hewani ni mambo yanayoendelea ndani ya serikali yetu na sio kama wanataka kufunga kwa makubaliano bali inaonekana ni kwa lazima.
Mwenyewe husika na vidio au nyimbo hiyo maoni yako kuwakomboa wafanyakazi na wananchi na nchi kwa ujumla
No comments:
Post a Comment