Friday, December 9, 2011
Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na
viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya
uhuru wa Tanzania yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
mchana huu hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mhshimiwa Hifikepunye Pohamba.
FULLSHANGWE inakumuvuzishia moja kwa moja matukio ya maadhimisho hayo kutoka
kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ili kukujuza mambo mbalimbali
yaliyojiri katika sherehe hizo.
Rais Jakaya Kikwete akielekea Jukwaa kuu
mara baada ya kukagua gwaride katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwa ameongoza na na Mkuu wa Majeshi nchini
Jenerari Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya
ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi
hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanawake
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya
ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi
hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanaume.
Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati
mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.
Hiki ni kikosi cha Jeshi la wananchi
wanamaji kikiwa tayari kutoa heshima kwa amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tamnzania Dk. Jakaya Kikwete.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono
wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe
za miaka 50 ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment