Sifa Za Mke Mwema
Kitabu cha mithali 31 kuanzia msitari wa 10 hadi 31
kimeelezea sifa mbalimbali za mke mwema, tuangalie kwa uchache sifa hizo kwa
kuzichambua katika maeneo tofauti.
1. Imani
Mithali 31:26, 29, 30
Mke mwema anayashika na kuyafanyia kazi maneno ya
Mungu na ni mtu ambaye anamtumikia Mungu kwa moyo wake wote na akili yake yote.
Anatafuta makusudi ya Mungu katika maisha yake na kuyafuata. Zaburi
119;15
2. Ndoa
Mithali 31:11-12, 23, 28
Mke mwema humuheshimu mume wake na anahakikisha
anamtendea mambo mema siku zote za maisha yake. Ni wa kuaminika na msaidizi kwa
mume wake. Efeso 5:22-24, 1Petro 3
3. Malezi
Mithali 31: 26, 28
Mke mwema anawafundisha watoto wake njia za Mungu na
pia anawatunza kwa upendo. Huwafundisha kwa hekima na kuwaelekeza njia iwapasayo
kuiendea. Mithali 22:6
4. Huduma
Mithali 31:12-15, 17, 20
Mke mwema anamhudumia mume wake na familia yake yote
kwa ukarimu na upendo. Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora na chenye
afya. Ni mtu mwenye huruma na ukarimu.
5. Mali
Mithali 31:14, 16, 18
Mke mwema anatafuta kwanza ushauri wa mumewe kabla ya
kutumia fedha na pia anafanya manunuzi kwa hekima. Ni muangalifu kununua bidhaa
zenye ubora kulingana na mahitaji ya familia yake.Efeso 5:23
6. Nyumba
Mithali 31:15, 20-22, 27
Mke mwema ni mtu anayeifanya nyumba iwe mahali pa
kuishi. Anatengeneza mazingira ya kuvutia kwa familia yake na wageni wote na
anawahudumia watu wake wote kwa ukarimu. 1pet 4:9, Ebrania 13:2
7. Muda
Mithali 31:13, 19, 27
Hutumia muda wake vizuri na kuhakikisha anakamilisha
kazi zake za kila siku. Kamwe hapotezi muda katika kufanya mambo ambayo
hayampendezi Mungu na yasiyo na faida.
8. Uzuri / Urembo
Mithali 31:10, 21-22, 24
Ni mrembo na mwenye thamani, ana uzuri wa ndani
unatoka kwa Yesu Kristo. Anatumia ubunifu wake na utanashati wake kuleta uzuri
katika maisha yake na ya watu wake.
Mungu atusaidie ili maisha yetu yaonyeshe kweli
tunamjua na kumwamini yeye.
Ubarikiwe na Bwana Yesu!
Sifa za Mume mwema
1. Aliyesimama katika imani na tayari kuitetea katika familia:
1 Wakorintho
11:3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila
mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha
Kristo. Waefeso 5:23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke
kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe
ni Mwokozi wa kanisa. Ikumbukwe huyu ndiye ana uamuzi wa mwisho katika familia
akiamua kuukana ukristo, kurudi nyuma inakuwa na athari kubwa sana katika
familia. Hivyo hii ndio nguzo ya ndoa ya Kikristo.
2. Ampende mkewe:Waefeso
5:33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda
nafsi yake. Upendo ni nguzo ya Pili na pia ni moja ya tunda la Roho katika ndoa.
Hapa naomba nieleze hii ndoa inayoongelewa ni ya Kikristo hivyo upendo huu
hauwezi kuutenga na upendo wa Kristo kwa ujumla, je upendo unaelezwaje katika
Biblia:
a. Huleteana heshima Warumi
12:10
Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine kuliko mnavyojiheshimu wenyewe.
Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine kuliko mnavyojiheshimu wenyewe.
b. Hufadhiliana:
Atakupa mahitaji yako bila kujali nani anazalisha zaidi, hatajali cheo au elimu
yako. Maana katika ndoa mwingine anaweza panda zaidi ya mwingine lakini sio
sababu ya kumwacha kwa kujiona utaonekana duni. (kuwa na kiburi) 1
Wakorintho 13:4-8 4Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo
hauna wivu au majivuno.
c. Hauna ubinafsi;
husameheana: Hatatunza makosa yake moyoni atasamehe na kusahau,
haujihesabii haki 1 Wakorintho 13:4-8 5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na
adabu. Upendo hautafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya
mabaya.
d. Huonyana: atakwambia
kama unakosea na siyo kukuacha upotee na marafiki wabaya 1
Wakorintho 13:4-8 6Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia
kweli,
e. Hustahimiliana: hata
uwe mgumba, mlemavu, unakasoro gani atakuvumilia. 1 Wakorintho
13:4-8 7Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote,
hustahimili yote,
f. Hauna ukomo au
mipaka: Atakupenda hadi kifo sio siku anaamka ‘mimi na wewe
basi” 1 Wakorintho 13:4-8 8Upendo hauna mwisho. Lakini
penye unabii, utakoma; zikiwepo lugha zitakoma; yakiwepo maarifa yatakwisha.
3. Heshima na
huruma:
Heshima humfanya mtu ajione unamjali, wanaume wengine atasema anapenda lakini anamwita mwenzie hajasoma, ametoka familia duni, hafanani na hali yangu, kwakweli huku ni kumdhalilisha mwenzio 1 Petro 3: 7 – 9 7Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.
Heshima humfanya mtu ajione unamjali, wanaume wengine atasema anapenda lakini anamwita mwenzie hajasoma, ametoka familia duni, hafanani na hali yangu, kwakweli huku ni kumdhalilisha mwenzio 1 Petro 3: 7 – 9 7Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.
4. Amtimizie haja zake za
kimwili:1 Korintho 7: 3-5: 3 Mume atimize wajibu
wake wa ndoa kwa mkewe; na hali kadhalika mke kwa mumewe. 4Kwa maana mke
hatawali mwili wake mwenyewe, bali mume wake ndiye autawalaye. Vivyo hivyo, mume
hatawali mwili wake mwenyewe, bali mkewe ndiye anayeutawala. 5Msinyimane,
isipokuwa kama mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda mfupi ili muwe na nafasi
nzuri ya maombi. Lakini baada ya muda huo rudianeni tena shetani asije akapata
nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kushindwa kujizuia.
5. Ajue kulea
watoto:Mume ndiye baba pia hivyo asiishie kupenda mke tu
watoto hajui wanasoma vipi, wanaishi vipi, anaacha malezi na makuzi yote kwa
mama, siku watoto wakiharibika anaanza kumlaumu mama. Watoto wanahitaji wazazi
wote wawili ili kukua katika mwenendo mzuri wa maadili ya Kikristo.
1 Timotheo3: 4 4Aweze kuisimamia nyumba yake vizuri
akiwafanya watoto wake kuwa wanyenyekevu na wenye heshima katika hali zote.
(Hata kama imetajwa kuwa ni sifa ya Askof ila imebainishwa ni moja ya sifa za
mume)
6. Aiheshimu ndoa / asiwe
mzinzi:Kuna wanaume ambao anaweza kukupatia mahitaji yote
muhimu, lakini ni mzinzi tena wala hafichi, hii kwakweli ndio sababu kubwa ya
kuvunjika ndoa nyingi sasa hivi. Ulipoapa mbele za Mungu utampenda mwenzio hadi
kifo iweje uchangie upendo huu na wengine, hapa ni kama umesema “nilikupenda
lakini sasa nimepata mwingine hivyo unamruhusu aondoke katika ndoa yenu” wengine
hawaishii hapa anafukuza na kuoa mwingine kabisa. Mwanamke anahitaji kuona kuwa
yeye ndiye pekee anayepewa upendo huu na mumewe na sio kuchangia na msururu wa
wenza. Waebrania 13:4 Ndoa iheshimiwe na watu wote, na
wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na
waasherati. Mathayo 19:9-11 9Nami nawaambieni, mtu ye
yote anayemwacha mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, akaoa mke mwingine,
anazini.” [``Na mtu anayemwoa mwanamke aliyepewa talaka pia anazini.'']
7. Anayejitegemea kwa kimawazo na
mali:Kuna waume ambao pamoja na umri wa kuoa bado anategemea
baba, mama, kaka, dada kwa mahitaji yake na pia hata mawazo afanye nini. Sio
vibaya kukaa na ndugu hasa kama ni wema na wanatabia nzuri pia wasioingilia ndoa
yako. Na ni vizuri pia kupata ushauri wa waliotuzidi katika mambo mbalimbali
unayotaka kufanya lakini isiwe ni kikwazo cha upendo, heshima na uhuru wa ndoa
yenu. Mume awe anajitegemea awe mbunifu akimshirikisha mkewe ili pamoja waweze
kujitegemea na sio kutegemea wazazi hadi kutawaliwa hapa hata uimara wa Imani
yake unaegemea huko anakofadhiliwa.
Marko 10:7 Na kwa
sababu hii mume atamwacha baba yake na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili
mmoja. Hapa ina maana aweze kumtunza mkewe na familia pamoja na kumwezesha, ila
wanawake tuwe na kiasi katika kutumia hiki kifungu hususan mavazi yatupasayo:
1 Petro 2: 3 – 6 3Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje,
yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. 4Bali
kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa
roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu.
5Maana ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu
na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao. 1Timotheo 2: 9 –
10: 9Kadhalika, nataka wanawake wajipambe kwa heshima na kwa
busara. Mavazi yao yawe nadhifu, si kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu,
lulu na mavazi ya gharama kubwa, 10bali kwa matendo mema kama iwapasavyo
wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu.
Ninaomba wengine zaidi wachangie na kurekebisha
maana bado ninajifunza Neno, Mungu mwenye nguvu azidi kutupa roho ya hekima na
maarifa katika safari yetu hii.
No comments:
Post a Comment