NJOMBE

NJOMBE

Saturday, April 7, 2012

BREAKING NEWS: STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA HATUNAE TENA DUNIANI

 


Msanii wa kuigiza Steven Kanumba afariki dunia usiku wa kuamkia leo.Maiti bado ipo muhimbili na kwa habari zilizotufikia hivi punde.Steven Kanumba alianguka ghafla usiku wa kuamkia leo na kukimbizwa hospital ya Muhimbili ambako mauti yalimkuta.Msiba utakuwa Sinza Vaticani wewe fika Vaticani Hotel basi utakuwa umefika msibani kwa habari nyingine zaidi basi endelea kuwa nasi.
Mwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.Mungu ailaze roho ya Kanumba mahala pema peponi Amen.

Friday, April 6, 2012

The Truth About Long Distance Relationships


Unatongozwa hovyo na wanaume? Dawa hii hapa!


Leo nimeona nizungumze juu ya tabia ya baadhi ya wanawake kutongozwa hovyo. Kiukweli ni tabia ambayo inakera. Kila ukipita huku unaitwa, ukienda kule unaitwa, hili tatizo lipo kwa wanawake wengi hasa wa mijini.

Nimeamua kuandika mada hii hasa kutokana na wasomaji wengi kunitumia meseji wakilalamikia tabia hii. Kati ya meseji hizo, ipo inayosomeka; “Shikamoo kaka . Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21, naishi Mtwara. Tatizo linalonisumbua na kunikosesha raha ni kuitwa-itwa hovyo na wanaume, nikienda, naishia kutongozwa!

“Yaani hata sijui nifanye nini? Mimi kwa mwonekano ni binti mrembo tu ambaye naweza kumvutia mwanaume yeyote kimapenzi, najipenda na nahakikisha napendeza muda wote. Nimejaribu kufikiria hilo na kuliona kama pengine linaweza kuchangia tatizo hilo, lakini sioni kama ni sababu.

“Naamini wewe ni mtaalamu wa mambo ya uhusiano na katika hili utanisaidia. Ahsante sana, naamini utanipa msaada wa kunifaa. Naomba sana usiandike jina wala namba yangu ya simu gazetini. Ahsate sana.”

Ujumbe wa msomaji wetu huyo, ndiyo hasa ulionisukuma niandike mada hii leo, naamini wapo wengine wana tatizo hilo, lakini hawakuweza kuniandikia sms au kunipigia. Huyu atakuwa mwakilishi wa wote.

Ukiacha msomaji wangu huyo aliyenitumia ujumbe mfupi, wengine walionipigia simu wameeleza wazi jinsi wanavyosumbuliwa na wanaume, wengine wakidai wanataka kuwaoa, wengine wakieleza wazi kuwa wanataka kufanya nao mapenzi tu tena kwa ahadi ya malipo manono.

Kiukweli hili ni tatizo sugu ambalo linaepukika lakini kuna ugumu kidogo katika kuliepuka moja kwa moja. Mitaani tunapoishi wapo wanaume ambao wasione msichana mrembo akipita, lazima wataanza kumsumbua kwa kumuita na wengine kufikia hatua ya kuwatomasa tomasa sehemu zao nyeti bila ridhaa yao. Mbaya zaidi ni kwamba wanaume hao hufanya hivyo hata kwa wanawake ambao ni wake za watu au wenye wapenzi wao.

Tabia hii huwakera sana baadhi ya wanawake hasa wale wanaojiheshimu na kuziheshimu ndoa na uhusiano wao. Hata hivyo, ili kuwaepuka wanaume wakware wakati mwingine huwa ngumu kwa kuwa wengi wao hawana akili timamu, muda mwingi wao huwaza kufanya ngono tena na kila mtu watakayemuona bila kufikiria madhara wanayoweza kuyapata baadaye.

Niseme tu kwamba, wanaume wa aina hii wapo wengi ila kwa mwanamke anayeiheshimu ndoa yake au uhusiano wake na akaweka nia ya kuwaepuka, inawezekana! Hizi hapa chini baadhi ya njia muhimu za kukabiliana na tatizo hilo la kusumbuliwa hivyo na wanaume.

MAVAZI YAKO YAKOJE?
Wanawake wengi sana hukosea katika suala zima la uvaaji. Baadhi yao hupendelea kuvaa mavazi yanayoonesha maungo yao kiasi cha baadhi ya wanaume kuwachukulia kuwa ni machangudoa.

Ni kweli kwamba mavazi ya mtu hayawezi kumfanya akaingizwa katika kundi la watu fulani na pia kila mtu anao uhuru wa kuchagua avaeje lakini, kwa uhalisia mwanamke asiyeujali mwili wake kwa kuvaa nguo zisizokuwa na heshima, asitarajie kuuepuka usumbufu wa wanaume wapenda ngono. Ni lazima watamtongoza na wakati mwingine kumfanyia vitendo vya kumdhalilisha.

Hivi mwanamke kuvaa ‘kitop’ na suruali inayobana huku ikionesha shepu ya sehemu zako nyeti kisha kukatiza mbele za wanaume kutakuwa kunamaanisha nini kama siyo kujitangaza kwao? Hivi kwa mavazi hayo utakuwa na tofauti gani na wale wanaoijiuza kule Ohio?

Ifike wakati uondokane na ulimbukeni wa kwenda na wakati hasa kwa wewe mwanamke ambaye umeolewa ama una mpenzi wako. Vaa mavazi ya heshima kila unapokwenda.

Mavazi yanayoonesha maungo yako yavae ukiwa na mpenzi wako chumbani. Naamini kwa kuvaa hivyo, kidogo utakuwa unapunguza ile kasi ya wanaume wakware kukusumbua.

TABIA ZAKO VIPI?
Baadhi ya wanawake acha wasumbuliwe kwani tabia zao huwafanya wasiheshimike mbele ya jamii na kuonekana kwamba ni jalala. Unakuta mwanamke anapita mbele za wanaume kisha anatembea kwa kujishebedua huku akitingisha maungo yake makusudi, hapo unatarajia nini?

Achilia mbali hilo, wapo baadhi ya wanawake ambao ni rahisi kuchukuliwa na wanaume. Yaani hawawezi kusema hapana! Ukiwa na tabia hiyo tambua kuwa, kila mwanaume mkware atataka kuweka mhuri wake mwilini mwako.

USITANIANE NA WANAUME!
Wanawake wengine ni wa ajabu sana. Unamkuta anajenga ukaribu sana na baadhi ya wanaume na kufikia hatua ya kutaniana nao katika mambo ambayo mwishowe huwa kutongozana.

Mwanamke aliyeolewa ama mwenye mpenzi wake hatakiwi kujenga ukaribu sana na wanaume wa pembeni. Unapopita maskani wamekaa wavulana, wasalimie kisha chukua hamsini zako, utani wa kijinga epukana nao kwani mwishoni watakutongoza na ukionesha kuchukia watadai walikuwa wanakutania kumbe wako ‘sirias’.

MWAMBIE MPENZI WAKO
Sishauri kila mwanaume atakayekuchomekea umwambie mpenzi wako. Nasema hivyo kwa kuwa, natambua itageuka kero kwa mwenza wako. Ila sasa wapo wanaume ambao ni ving’ang’anizi. Unamweleza kuwa una mpenzi wako lakini hakuelewi ni vema ukamtaarifu mumeo ili akae akijua.

Hiyo itasaidia sana kwani mumeo anaweza kuchukua hatua zinazostahili dhidi yake na hatimaye kuweza kupunguza kasi ya usumbufu huo. Kamwe usithubutu kukaa kimya. Mbaya zaidi ni kwamba unaweza kukuta shemeji yako ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wako ama mwanaume anayemfahamu vilivyo mumeo akakutongoza!

Huyu ni hatari sana na wala usisubiri akutongoze mara mbili. Siku ya kwanza tu atakayokutamkia maneno yake ya kipuuzi, kwanza geuka mbogo, mkaripie kwa ukali kisha mpe taarifa mpenzi wako.

Wanaume wa siku hizi wametawaliwa na tamaa zisizokuwa na msingi. Ukitaka wakusumbue watakusumbua kweli na wakati mwingine wanaweza kukushawishi ukamsaliti mpenzio wako.

Kikubwa ni mwanamke kuwa na msimamo. Kutokukubali kugeuzwa kiti cha daladala, kwamba kila mtu anaweza kumchezea. Naamini msimamo huo pamoja na mambo hayo niliyoyataja hapo juu unaweza kuepukana na usumbufu huo kutoka kwa wanaume.

Thursday, April 5, 2012

KUZUIA MIMBA KWA KUTUMIA KALENDA



Kwanza nataka niwaeleze wadau juu ya athari za vidonge vya kuzuia mimba:

Wanawake wengi hujikuta wanakumbwa na machafuko ya tumbo au kutapika wakati wa asubuhi, kuvimba matiti kama siyo kukumbwa na dalili za ujauzito mara wanapoanza kutumia vidonge kwa mara ya kwanza!Hii husababishwa na vidonge hivyo ambavyo vina hormones zile zile ambazo mwanamke huzitia kwenye damu wakati akiwa na mimba. Hata hivyo wataalam wanasema kuwa dalili hizi hufikia kikomo baada ya miezi kati ya 2 hadi 3.

Sambamba na hilo watumiaji wengine wavidonge hutokwa na damu nyingi wakati wakiwa kwenye siku zao.

Athari kubwa anayoweza kuzipata mtumiaji wa vidonge vya kuzuia mimba ni kuganda kwa damu kwenye moyo, mapafu au ubongo!

Wadau naomba muelewe kuwa kwa wanawake wengine mimba pamoja na kutumia vidonge vya kuzuia mimba vina hatari kubwa zaidi kwao. Hivyo basi wanawake hawa ni lazima watumie njia zingine za kuzuia mimba!

Baada ya kutanabaisha hayo naomba sasa nimjibu dada yangu jinsi yakutumia kalenda kujikinga na mimba!

Njia hii haina uhakika sana wa kuzuia mimba, lakini ni nzuri kwa sababu haigharimu chochote.Njia hii huwafaa zaidi wanawake ambao taratibu za siku zao za kwenda mwezini ni kawaida mara moja kila baada ya siku 28, na ili iweze kuzaa matunda, njii hii huhitaji mtumiaji awe tayari kukaa bila kukutana kimwili kwa muda wa wiki moja kila mwezi!

Kwa kawaida kuna siku 8 tu kila mwezi ambazo mwanamke anaweza kupata mimba ambapo siku hizi zipo katikati ya siku zake za kwenda mwezini, na huanza siku 10 baada ya siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi. Hivyo basi ikiwa mwanamke yoyote hataki kupata mimba ni lazima aache kukutana na mwanaume kwenye siku hizi 8! Naamini hili linawezekana kwani siku nyingine zilizobakia wapendanao wanaweza kujiachia kama kawaida kwani hakuna uwezekano wa mwanamke kushika mimba!

Ili kuepukana na kutatanikiwa, ni lazima mwanamke aonyeshe kwenye kalenda zile siku ambazo hatakiwi kukutana na mwanaume. Hapa inaweza kuwa ngumu kuchora kalenda ya ukutani kwa kuwa inatumiwa na wengi lakini ni rahisi kutekeleza hili kwa kutafuta pocket kalenda [kijikalenda ambacho waweza kiweka kwenye pochi yako]

Kwa mfano: Unaingia kwenye siku zako tarehe 5 Desemba, weka alama kwenye tarehe hiyo kisha hesabu siku 10 na baada ya hapo pigia msitari siku 8 zinazofuata!

Angalia mfano huu:-

Kumbuka siku hizo nane utakazozipigia msitari ni hatari kwani ukikutana na kidume tu na kushiriki ngono bila kutumia kondom utashika mimba, hivyo ni vema usikutane na mwanaume hata kidogo, yani epuka hata akikubembeleza na lugha laini kuwa nitapizia nje sweetie, sijui nini na nini kama hataki tumia kondom kataa kwani kupizia nje ni bahati nasibu hasa pale mwanamke anapoamua kumpa mwanaume maujuzi ya kabatini ambayo ni adimu, yaani mwanaume hupewa kwa sababu maalum tu hali inayomfanya apagawe kwa huba na hivyo huweza msababisha ashindwe kupiziza nje!

Nimalize kwa kusema kuwa, mwanamke anapaswa kuendelea na utaratibu huu kila mwezi lakini akumbuke kuwa, njii haina uhakika sana mbaka itumiwe sambamba na njia nyingine kama vile kondom.

Chezea mama Mziray ana marafiki wa kweli wasomi, warembo kufa,umetisha mama mziray





Wednesday, April 4, 2012

Polisi aliyetinga disko na bangi afukuzwa kazi

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limemfukuza kazi askari wake, Deogratius Chang’a, kwa kosa la kuingia ukumbi wa disco wa Pub Alberto wa mjini hapa na kufanya vurugu, kuumiza watu na kukutwa na misokoto mitatu na nusu ya bangi.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, alithibitisha jana kufukuzwa kazi kwa askari huyo na kueleza kuwa ni baada ya Mahakama ya kijeshi kumkuta na hatia na kuamuru afukuzwe kazi kwa fedheha.
Alisema kuwa kosa la kwanza la askari huyo ni kufanya fujo katika ukumbi huo na kumjeruhi mmoja wa wafanyakazi wa ukumbi huo kwa kumng’ata meno na kosa la pili ni kukutwa na misokoto ya bangi mfukoni.
“Mnamo Machi 24, mwaka huu, saa 6:05 usiku, katika kituo cha Polisi Kati Moshi Mjini, askari huyo alipekuliwa na kukutwa na bangi, kitendo ambacho ni kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi
Tanzania. Amepatikana na hatia kwa makosa yote mawili, Kamati ya Maadili ya Polisi ilipendekeza afukuzwe kazi kwa fedheha, hivyo tumemfukuza kazi kuanzia Aprili 3, mwaka huu,” alisema.
Askari huyo alimjeruhi mlinzi wa pub hiyo, Rajab Hamad, kwa kumng’ata meno mkononi, kutoa matusi na kuwapiga ngumi watu mbalimbali bila sababu, kitendo ambacho ni kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi nchini.
Baada ya tukio hilo, Jeshi hilo lilieleza kuwa  askari huyo akiwa amevalia kiraia alifika katika ukumbi huo kwa lengo la kucheza miziki na kwamba alikuwa akinywa pombe, lakini baada ya muda alianza kufanya vurugu.
Walinzi wa ukumbi huo walipojulishwa juu ya vurugu hizo, walifika na kuanza kukabiliana naye na ndipo alipomjeruhi mmoja kwenye mkono na mmiliki wa ukumbi huo, Christopher Shayo, alipoingilia kusuluhosha, alipigwa ngumi ya usoni.
CHANZO: NIPASHE

Tuesday, April 3, 2012

AIRTEL YALA RAHA NA WATOTO WA WATEJA WAO JIJINI DAR ES SALAAM

 Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania wakijumuika kwa pamoja
na  watoto  wa wafanyakazi wa Airtel kukakata keki iliyoandaliwa na
kampuni ya Airtel Tanzania katika shamra shamra za tamasha maalum
kuelekea sikukuu ya pasaka ambapo watoto hao walipata nafasi ya
kucheza  michezo mbali mbali kwa pamoja  ambayo imefanyika katika
kituo cha michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport  ndani ya jengo la
Qualty center Jijini Dar-es-salaam.

 Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania wakijumuika kwa pamoja
na  watoto  wa wafanyakazi wa Airtel katika shamra shamra tamasha
maalum la watoto kuelekea kusheherekea sikukuu ya pasaka kwa michezo
mbali mbali kwa pamoja  ambayo imefanyika katika kituo cha michezo ya
watoto kiitwacho Fun Sport  ndani ya jengo la Qualty center Jijini
Dar-es-salaam kwa hisani ya Airtel.

 Meneja mauzo wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi.Hilda Nakajumo akikata
keki kwa  pamoja na Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania na
watoto  wa wafanyakazi wa Airtel katika shamra shamra za  kuelekea
sikukuu ya pasaka ambapo watoto hao walipata nafasi ya  kucheza
michezo mbali mbali kwa pamoja  ambayo imefanyika katika kituo cha
michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport  ndani ya jengo la Qualty center
Jijini Dar-es-salaam.

 Mkurugenzi wa Biashara  wa kampuni ya Airtel Tanzania Bw.Irene  Madeje
akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe ya michezo kwa
Watoto wa wateja wa kampuni ya Airtel Tanzania na  watoto  wa
wafanyakazi wa kampuni hiyo katika shamra shamra za  kusheherekea
sikukuu ya pasaka na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya wateja
wa Airtel na wafanyakazi wa Airtel ambapo watoto hao walipata nafasi
ya  kucheza  michezo mbali mbali kwa pamoja  ambayo imefanyika katika
kituo cha michezo ya watoto kiitwacho Fun Sport  ndani ya jengo la
Qualty center Jijini Dar-es-salaam.

Watoto wakicheza mchezo wa kuendesha magari wakati wa tamasha maalum
la michezo kwa watoto lilioandaliwa na Airtel ili  kutoa nafasi kwa
watoto  wafanyakazi wa Airtel pamoja na watoto wa wateja wa Airtel
jijini Dar esa salaam kukutana na kucheza  michezo mbali mbali kwa
pamoja , tamasha hilo  lililofanyika katika kituo cha michezo ya
watoto kiitwacho Fun Sport  ndani ya jengo la Qualty center Jijini
Dar-es-salaam kwa udhamini wa  Airtel 

Airtel yaanza shamra shamra za sikukuu kwa kushereheka na watoto
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel yaanza shamrashamra za sikukuu
kwa kujumuika na watoto wa wateja wao jijini Dar es saalam ambapo
watoto zaidi ya 150 walipata nafasi ya kukutana pamoja jumamosi
mwishoni mwa wiki hii  katika ukumbi wa Quality Center - Fun sports na
kufurahi kwa pamoja.
.
Huu ni mkakati ambao Airtel imejiwekea  kusherehekea pamoja na watoto
wa wateja wao wa makapuni ( corporate customer)  wiki moja kabla ya
sikukuu za pasaka huku lengo likiwa ni kuwa karibu na wateja wao na
kusambaza upendo wa kampuni hiyo kwa wateja wake na familia zao.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Bi Irene Madege

alisema" leo tunajisikia furaha kuwa na watoto wa wateja wetu na
kujumuika nao pamoja, Tumekuwa tukifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni
katika kuwazawadia wateja wetu, lakini leo tunatumia muda huu kuwapa
burudani watoto ambao ndio wateja wetu wa kesho".

Kwa muda wa takribani masaa 4 watoto zaidi ya 150 walipata burudani

mbalimbali ikiwa pamoja na michezo mbalimbali ya watoto kama  face
painting, mashindano ya kucheza music, na pia kupata nafasi ya
kukutana na wafanyakazi wa Airtel,  kumzungumza pamoja na kuwasisitiza
watoto kuwa wasikivu shuleni ili  kufanya vizuri kwenye masomo yao,
tunaamini watoto hawa wamekuwa na wakati mzuri pamoja nasi. Aliongeza
Bi Irene
.

Monday, April 2, 2012

Mbunge Arumeru Mashariki ni Joshua Nassari wa CHADEMA


MGOMBEA Ubenge Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amewashinda wagombea wenzake saba kutoka vyama vya CCM, AFP, DP, NRA, SAU, UPDP na TLP katika uchaguzi mdogo wa Ubunge uliofanyika Aprili 1, 2012.

Kwa Mujibu wa Matokeo ya liyotangazwa asubuhi hii yanaonesha kuwa Mgombea Ubunge wa Joshua Nassari CHADEMA amepata kura  32,972, na kumshinda Mgombea mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo, Sioi Sumari wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 26,757.

Kwamatokeo hayo inafanya kuwa idadi ya Kura zilizompa ushindi  Nassari wa Chadema kuwa kura 6,215 dhidi ya Sioi Sumari CCM.

Msimamizi wa huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi.

Gagenzi pia ametangaza matokeo ya wagombea wengine ambao walitoka vyama vya Siasa nchini kuwa kama yafuatavyo:-
AFP – 139, DP -77, NRA – 35, SAU – 22, UPDB – 18 na TLP – 18.

Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.

Aidha CHADEMA pia jana katika Uchaguzi wa Udiwani imepata Ushindi katika Kata za Kirumba mkoani Mwanza na Kiwira mkoani Mbeya.
Chanzo Fatherkidevu

Wabunge wa Chadema wacharangwa mapanga

WABUNGE wawili wa Chadema wamejeruhiwa vibaya kwa mapanga na mashoka huko Mwanza katika tukio lililotokea saa nane usiku katika eneo la Ibanda Kabuhoro baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM usiku wa kuamkia uchaguzi wa diwani Kata ya Kirumba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow alisema jana kwamba mbali na wabunge hao, Samson Highness Kiwia wa Ilemela na Salvatory Machemuli wa Ukerewe, wengine walioshambuliwa ni pamoja na Ahmed Waziri ambaye inasemekana kuwa ni kada wa UVCCM aliyekatwa kiganja chake cha mkono wa kulia.

Wengine ni Haji Mkweda (21), ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia, Judhith Madaraka (26), aliyechomwa kisu kwenye titi lake la kushoto na mkono wa kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni. Majeruhi wote ukiondoa wabunge hao na Waziri, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Awali, wabunge hao walilazwa katika Hospitali ya Rafaa Bugando lakini baadaye walisafirishwa kwa ndege kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam. Kwa upande wake, Waziri amelazwa Bugando.

Mbali ya Mwanza, katika uchaguzi mwingine wa udiwani Kata ya Kiwira, Mbeya nako damu ilimwagika baada ya watu kadhaa kushambuliwa kwa mapanga na nodo. Katika tukio hilo polisi imewatia mbaroni watu 10.

Kamanda Barlow alisema katika vurugu hizo magari matatu likiwemo la Kiwia yaliharibiwa.

Alisema polisi ilipata mapema taarifa za tukio hilo lakini ilichelewa kufika kutokana na eneo hilo kuwa lenye mawe na milima hivyo kufika wakati tayari wabunge wameshajeruhiwa vibaya na mali hizo kuharibiwa.

“Kiwia alionekana kushambuliwa kichwani na kitu chenye ncha kali na magari nayo yakiwa yameharibiwa vibaya. Kwa mazingira hayo ya usiku na hali ilivyotokea, jeshi langu linafanya uchunguzi wa kina kuweza kujua kiini cha vurugu hizo, lakini tumewaelekeza wenzetu wa Takukuru kufuatilia kujua kama mazingira ya wabunge hao kutembea usiku huo yalikuwa na uhusiano wowote na masuala ya rushwa,” alisema.

Bunge latoa tamko
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alithibitisha taarifa za kuvamiwa kwa wabunge hao na kusema wamepelekwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Ndugai alisema utaratibu ulivyo ni kwamba mbunge yeyote akiumia, Bunge ndilo linaloshughulikia matibabu yake na ni katika hospitali za Serikali tu.

“Nimepata taarifa hizo na tumetuma timu yetu ya Bunge kwenda kushughulika suala hilo. Mara ya kwanza nilisikia ni mbunge mmoja tu ndiye aliyepelekwa Dar es Salaam, lakini baadaye nikaambiwa ni wote wawili hivyo tunafuatilia kujua hali zao,” alisema Ndugai

Chadema
Akizungumzia tukio hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema tukio hilo lilitokea saa 7:00 usiku baada ya kutokea kundi la watu ambao idadi yao haijajulikana na kuanza kuzuia gari la Mbunge Kiwia, huku wakilishambulia kabla ya kulimwagia gesi ya kuwasha baada ya kuvunja vioo kisha kumtoa na kuanza kumshambulia.

“Kabla ya kushambuliwa baada ya kuona gari lake limevamiwa alibahatika kumpigia simu Machemli akimwomba awahi eneo alilokuwepo, naye alipofika alijikuta akiwa mikononi mwa vijana hao na kushambuliwa pia,” alisema Zitto na kuongeza:

“Wakati tukio hilo linatokea, askari wa jeshi la polisi walikuwa katika maeneo hayo lakini walishindwa kutoa msaada kitu ambacho kilitushangaza.”

Chadema jana kilitoa tamko kulaani tukio hilo kikisema ni kitendo kinachopaswa kukemewa na wapenda amani na demokrasia ya kweli wote.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema katika taarifa yake kuwa Chadema hakitaishia kulaani na kusikitika, bali kitachukua hatua stahiki ili kukomesha vitendo hivyo.

Mwenyekiti wa CCM

Tukio hilo limekuja siku saa chache baada ya Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina kukaririwa akiwaagiza wana CCM, kwa ujumla kutowavumilia Chadema akidai kuwa wamekuwa watu wa vurugu akisema katika uchaguzi uliopita waliaachia wakafanya walivyotaka ikiwemo kuchoma ofisi za CCM.

Mabina ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni alisema: “Nawaambia wafuasi wa CCM hakuna kuwaogopa Chadema, lazima tupambane nao kwa hili.”

Jana Mabina, alikiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na kusema: “Chadema wamezoea fujo. Bila ya kufanya fujo hawawezi kushinda, sasa angalia usiku wa manane walikuwa wanafanya nini?” alihoji na kuendelea:

“Kama siyo kutoa rushwa, ninachojua wao ndiyo walianza kushambulia vijana wangu, mfano huyu mmoja (Ahmed) wamefanikiwa kumvunja mkono na hivi tunavyoongea ameingizwa chumba cha upasuaji kufanyiwa oparesheni mkono wake.”

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema jana kuwa anazo taarifa za tukio hilo lakini asingependa kulizungumzia kwa kuwa chama kimejipanga kuzungumza na waandishi wa habari leo.

Mapanga Mbeya

Huko Mbeya, watu wanne waliokuwa wakitoka katika kituo cha kupigia kura cha Kiwira Mjini wamejeruhiwa kwa kukatwa mapanga katika eneo la Hilondo ambalo ni maarufu kwa machimbo ya mchanga.

Waliojeruhiwa ni John Andengenye (26), Daud Hamis (27), Jacob Kalua (30) na mwingine ambaye hakutambuliwa mara moja.

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Makandana, Rungwe Grace Kapungu alithibitisha watu hao kufikishwa katika hospitali hiyo ya wilaya kwa ajili ya matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa watu 10 wamekamatwa wakihusishwa nalo.

Habari hii iemandikwa na Sheilla Sezzy, Mwanza; Godfrey Kahango, Mbeya na Frederick Katulanda, Geofrey Nyang'oro, Boniface Meena Dar.
Habari na Mwananchi.

CCM hali mbaya Arumeru

Mkazi wa Arumeru Mkoani Arusha, akipiga kura yake katika kituo cha Ngaresero, katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
                                                                  CHADEMA YAFANYA VIZURI KATA 11KATI YA 17, YASHINDA PIA UDIWANI MWANZA. SONGEA,MBEYA,CUF YAPETA TANGA
Waandishi Wetu
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeongoza kwenye kura za awali kwa mgombea wake, Joshua Nassari kupata kura nyingi katika kata 11 kati ya Kata 17 za Jimbo la Arumeru Mashariki.

Dakika chache kabla ya kutangaza matokeo hayo, baadhi ya wafuasi wa CCM waliokuwa wamefurika katika Ofisi za Mji Mdogo wa Usa River na baadhi ya polisi, walikuwa wameondoka eneo hilo, wakiwaacha wapambe wachache wa mgombea wao, Sioi akiwamo, Beno Malisa.

Huu ni uchaguzi wa kwanza mdogo kwa Chadema kushinda katika jimbo lililokuwa likishikiliwa na CCM na uchaguzi wa pili kwa chama hicho cha upinzani, kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya ule uliofanyika katika Jimbo la Tarime, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe.

Katika matokeo hayo yanayokusanywa na kujumlishwa katika ofisi za mji mdogo wa USA River, CCM,  imefanya vema katika kata tatu ambako mgombea wake, Sioi Sumari amepata kura nyingi ikilinganishwa na Nassari.

Takwimu zinaonyesha kuwa Chadema wanaongoza katika kata za Akheri ambako ni nyumbani Kwa Sioi, Poli, USA-River, Mbuguni, Seela, Sing'isi, Nkoarua, Maji ya Chai, Kikwe, Maroroni, Nkoaranga, King'ori na Songoro ambako ni nyumbani Kwa Nassari. Jimbo la Arumeru Mashariki lina kata 17.

Mgombea wa CCM Sioi ameongoza katika kata za Makiba, Leguruki na Mkoandrua hadi saa 7:15 usiku jana ambapo msimamizi wa uchaguzi, Trasias Kagenzi alikuwa akisubiri masanduku ya kura kutoka kata mbili.

Kata ambazo masanduku na matokeo yake yalichelewa kutokana na umbali wa maeneo hayo ni Kikatiti na Ngarenanyuki.

Mbali na Chadema kuongoza Arumeru chama hicho pia kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Mwanza.

CUF imeambulia kiti kimoja cha udiwani Tanga na CCM Dar es Salaam.

Katika tukio lingine, wakala wa Chadema katika chumba Cha kujumlisha kura, Godbless Lema, jana alilazimika kutumia nguvu dhidi ya msimamizi msaidizi wa kata ya Maroroni ambaye jina lake halikupatikana mara moja baada ya kumtuhumu kutaka kubadili tarakimu za matokeo kwenye fomu rasmi zilizowasilishwa.

"Yule msimamizi alikuwa akitaka kuchezea tarakimu katika fomu za matokeo kutoka kwenye kata yake bila kujua kama nilikuwa namfuatilia," alisema Lema.Habari na Mwananchi

JE WAJUA HATA WANAUME WANAWEZA KUPATA SARATANI YA MAZIWA ?


 Breast cancer (malignant breast neoplasm) is a type of cancer originating from breast tissue, most commonly from the inner lining of milk ducts or the lobules that supply the ducts with milk.Cancers originating from ducts are known as ductal carcinomas; those originating from lobules are known as lobular carcinomas. Breast cancer is a disease of humans and other mammals; while the overwhelming majority of cases in humans are women, men can sometimes also develop breast cancer.

The size, stage, rate of growth, and other characteristics of the tumor determine the kinds of treatment. Treatment may include surgery, drugs (hormonal therapy and chemotherapy), radiation and/or immunotherapy. Surgical removal of the tumor provides the single largest benefit, with surgery alone being capable of producing a cure in many cases. To somewhat increase the likelihood of long-term disease-free survival, several chemotherapy regimens are commonly given in addition to surgery. Most forms of chemotherapy kill cells that are dividing rapidly anywhere in the body, and as a result cause temporary hair loss and digestive disturbances. Radiation is indicated especially after breast conserving surgery and substantially improves local relapse rates and in many circumstances also overall survival. Some breast cancers are sensitive to hormones such as estrogen and/or progesterone, which makes it possible to treat them by blocking the effects of these hormones.
Worldwide, breast cancer comprises 22.9% of all cancers (excluding non-melanoma skin cancers) in women.In 2008, breast cancer caused 458,503 deaths worldwide (13.7% of cancer deaths in women).Breast cancer is more than 100 times more common in women than breast cancer in men, although males tend to have poorer outcomes due to delays in diagnosis.
Prognosis and survival rates vary greatly depending on cancer type, staging and treatment, and geographical location of the patient. Survival rates in the Western World are very good,for instance, overall, more than 8 out of 10 women (84%) in England that are diagnosed with the disease survive it for at least 5 years.In the developing countries, however, survival rates are much poorer

Sunday, April 1, 2012

WANANCHI WA ZILIZOKUWA KOTA ZA BANDARI GEREZANI WAMEVAMIWA NA KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO KINYUME NA SHERIA MAHAKAMA YAUNGANA NA SERIKALI KUWAHUJUMU WANANCHI.


Wakili wa waliokuwa wenye nyumba zilizokua kota za Bandari na TRC, Dkt. Sengondo Mvuni akizungumza na wateja wake leo na kusema kuwa mahakama iliungana na Serikali kuwahujumu Wananchi hao kwa kuwa hakuna notice ya masaa sita tena kwa kutangaza katika kituo kimoja tu cha TV.
Mwenyekiti wa wakazi wa Kota za Bandari Bi.Fatma Msindi akizungumza kwenye mkutano huo leo.
Wananchi wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa kuhusu kesi yao ya msingi leo.
Baadhi ya wakazi waliokuwa wakiishi katika kota za Bandari Gerezani wakisikiliza mada mbalimbali wakati wa mkutano wao leo.
Wakili wa waliokuwa wenye nyumba zilizokua kota za Bandari na TRC, Dkt. Sengondo Mvuni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kuhusu kufungua kesi mahakamani. (Picha na Rajab Mhamila)