NJOMBE

NJOMBE

Thursday, May 23, 2013

MTWARA KUMEKUCHA TENA SAKATA LA BOMBA LA GESI KWENDA DAR


https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94727&d=1369210247 
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94726&d=1369210162 
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94725&d=1369210066 
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94724&d=1369209998 
 
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu. Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo. Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo. 
Kituo  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)
 
Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar. 

Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
 Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe. 
Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.
 
Maeneo yote yametawaliwa na ukimya.

No comments:

Post a Comment