Kwa habari za burudani na michezo makaliery-t ndio blog yako nitumie na kutoa taarifa kwa email makalimachechi@yahoo.com ipate tangazwa hata biashara pia
Saturday, March 30, 2013
PICHA 6 ZA JENGO LA GOROFA LILILOANGUKA LEO DAR ES SALAAM
Kwa maelezo ya shuhuda, inasemekana limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo kuanza kazi.
Ni posta mtaa wa Indira Gandhi pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12 ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti nne.
Sehemu ya chini zinaonekana bado nzima hazijadondoka ila kifusi cha kutoka juu ndio kimefunika lakini kuna watu ndani yake wako hai na inaripotiwa wanapata hewa vizuri na wamekua wakiwapigia ndugu zao na kuwaita waje kwenye eneo la tukio.
Endelea kuwa karibu na millardayo.com taarifa zaidi zinazidi kufatiliwa.
Tuesday, March 19, 2013
STAMINA AFUNGUKA JUU YA UANDISHI WA MASHAIRI A.K.A MISTARI NA DAU LINAKWENDAJE
Baada ya kusumbuliwa sana na wasanii wachanga na wasanii wakubwa tu katika game la mziki wetu, kumtaka awaandikie nyimbo, Stamina ameamua kufunguka na kusema sasa ni wakati wa kuanza kutoza hela katika uandishi, baada ya kuandika hits kadhaa alizogoma kuzitaja..
"kuna swala moja nataka niliweke wazi, maana toka mwakajana mwishoni nasumbuliwa sana na watu wa kawaidaa, wasanii wa kawaida na wasanii wengine wakubwa tu amabao sitaki kuwataja, wamekuwa wakinitaka niwaandikie nyimbo, wengine wanauliza kabisa bwana utatuchaji sh ngapi, wengine wanataka kisela, na kuna baadhi ya hit songs nimeziandika...
"mwisho wa siku leo nataka nitangaze wazi kwamba, mtu yeyote atakaetaka nimwandikie wimbo, aidia ikiwa yake, naandika wimbo mmoja wenye verse 3 kwa 2,50,000 aidia ikiwa yake, na aidia ikiwa yangu yaani anataka kila kitu niandike mimi, yeye anataka tu wimbo naandika kwa 300,000, hizi ni bei zangu nimeona bora niziweke wazi, maana nasumbuliwa sana na watu...kama ni mwanangu naweza mfanyia bure tu lakini kwa sasa bora niweke wazi tu."
Friday, March 15, 2013
Audio) Nay wa mitego ft Diamond Platnumz - Muziki Gani
Nay na Diamond ndani ya studio wakiwa wanaandaa ngoma hiyo ya muziki gani |
SONG: MUZIKI GANI
ARTIST: NEY WAMITEGO FEAT DIAMOND
PRODUCER: MR TOUCH
CHORUS
Hivi nyi ma mc
mnachoimba kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
DIAMOND
Hata bibi yangu
mi aliniambia , mwanamke anahitaji kubembelezwa
Kupetipeti
matunzo pia, ukienda rafu utampoteza,
Muziki ni mfano
wa binti muzuri,
Na ndio maana
namtunza kwa vazi na uturi
NEY WA MITEG
Aaah piga
kimya, we ndo haufai kabisa hauna maana
Wabana pua kila
siku mnarogana, bibi yako alikuambia muziki ni kama binti
Mbona
unawachezea unawatema kama big g
Mara wema, mara
Jo keti, mara Naj, mara Penny, je mnafanya mziki mpate mabinti
DIAMOND
Uuuhhuuuu, hata
wazee wazamani, walishasemaga kazi na dawa
Chamuhimu
jukwaani, ni kuhakikisha wanapagawa,
Kwa michezo ya
kuringa ringa ndo huwa wanadata
Badilika usiwe
mjinga, utawakamata
CHORUS
Hivi nyi ma mc mnachoimba
kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
NEY WA MITEGO
Muziki wenu
ushirikina ndio umetawala, q chilla analalama anasema umemroga
Mganga wako aliekutoa umemkimbia
hujalipa, bila skendo za magazeti basi
huskiki
DIAMOND
Mi ni mti wenye
matunda, milele siogopi kupigwa mawe
Ubaya wenu
wengi kayumba, elimu mliitupa sandakalawe
NEY WA MITEGO
Bado
hujanishawishi, bongo fleva inanipa kichefu chefu
Kwanza nyie
malimbukeni wa umaarufu
Mnalenta
maringo mpaka kwa mashabiki , Wabana pua nyie watoto sio riziki,
Mnavaa nguo za
dada zenu, zinawabana mapaja nyie makaka duu
Aah nyie watoto
mchele mchele , kwenye show viuno mbele mbele X2
Nimewanyamazisha,
brazameni vipi we bado unabisha
DIAMOND
Mi nnamengi
nnayajua, ila we ni mtemi utaanzisha utata
Michezo yenu
kutoboa pua, bora ninyamaze usinipige mbata
Thursday, March 14, 2013
PAPA MPYA APATIKANA - FRANCIS WA KWANZA
Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki.
Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.
Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.

Tuesday, March 5, 2013
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma (UDom,) Bernadeta Minja, amefariki
dunia papo hapo na watu wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la
kampuni ya Muhamed Trans likitokea Dar es salaam kwenda Dodoma baada ya
kupata ajali katika eneo la Kiegea Gairo barabara ya Morogoro Dodoma .
Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi wakati akijaribu kupita
lori lililoharibika.
Ronaldo kwa mara ya kwanza Tangu 2009 ndani ya Trafoo ya Zamani
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Christiano Ronaldo kwa mara ya kwanza anarudi kucheza nyumbani tangu aondoke mahali hapo 2009.Mchezaji huyo anafurahi kufika kwa mara nyingine Old Traford kwani amenukuliwa akisema anajisikia amani sana anapofika mahali kama hapo na kumkumbusha mengi katika historia yake ya mpira.Na vile mashabiki wanavyomkaribisha anajisikia vyema ndio anakasema Manchester ni nyumbani kwangu.
Ronaldo anarudi kwa mara ya kwanza na timu yake Real Madrid inayochuana leo majira ya 10:45 PM saa tano kasorobo usiku katika mechi ya marudiano ya Mechi za mabingwa baada ya mechi ya kwanza timu hizo kutokuzidiana nguvu na kutoka sare ya 1-1 ndani ya Bernabeu
Ukiwa kama mshabiki na mpenzi wa mpira na hasa kwa wale washabiki wa Manchester United Unakumbuka nini unapoona vidio hii na ukihusisha na Cr7 alivyosema.
Coming Home

Sunday, March 3, 2013
HIVI TUNAENDA WAPI:MWALIMU AUAWA KWA RISASI NA POLISI HUKO MAKETE KWA KOSA LA KUTOVAA HELMET
Mwili wa mwalimu aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na polisi Makete kisa kutovaa Helment (kofia ya pikipiki)
Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma na kukutwa na umauti huo .
Inadaiwa kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi
Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao
Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi
Subscribe to:
Posts (Atom)