NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, February 26, 2013

Serikali ya Tanzania kuwaibia wananchi wake.

Mkutano uliofanyika AICC Arusha
Ndugu zanguni mtaniwia radhi kwa kusema haya najuwa ni kipindi kirefu sana nimekaa kimya ni kutokana na hali tu na mambo kuwa mengi, Ila nikaona sio vyema napopata nafasi yakushirikiana nanyi katika mambo kadhaa hasa ya maisha ni vyema.Hivi Hii Serikali yetu haina ya kufanya inawaza namna ya kuwaibia wananchi wake kila siku bila kuwaboreshea maisha wananchi wake.Hebu tujiulizeni kodi wanazokatwa wafanyakazi zinawasaidia nini hao wafanyakazi na bado pia bado Nchi inaenda kukopa nchi za nje, Bado haitoshi inakopa kwenye mifuko ya jamii kama NSSF na mingineyo na bado hairudishi.Hivi tunakwenda wapi,Ikaona haitoshi sasa inataka kuzui wafanyakazi hao wanaokatwa kodi na pia kuchangia mifuko ya jamii wasipate hela zao hadi miaka 55 wakati kwa mtanzania wa kawaida anaishi miaka 47 hadi 49 sasa hiyo miaka 55 mfanyakazi huyo atachukuwa mafao yake akiwa kaburini kama sio uwizi ni nini tena sio uwizi ni ujambazi mkubwa. Hii imenitoka akili baada Mbunge wa Kigoma Mh Zitto nae kutaka mfuko huo uchukuliwe akipingana na sera ya Mbunge mwenzie toka Chama cha Demokrasia na maendeleo Mh John Mnyika kutaka watu wawewanapata fedha zao kila waachapo kazi au kusimamishwa.Kutoka na hiyo imenijenga kwamba wanasiasa wote ni sawa hakuna anatoka chama gani wala ni nani.Kuna jambo limenitoa imani kabisa na viongozi wetu, hebu tuchukue hii kama changa moto wote najuwa tunalijuwa kundi la wasanii wa bongo flavor linalojulikana kama leka tutigite kutoka Kigoma likiwa chini ya Mh huyo, Kama mheshimiwa huyu haja pata kitu kidogo kuwakandamiza wananchi ni nini.Kapata nafasi hiyo na kaliambia kundi lake hilo lifanye wimbo kwa ajiri ya mifuko ya jamii hapa wewe unakuwa na imani na viongozi hao,Sijatoa hewani ni mambo yanayoendelea ndani ya serikali yetu na sio kama wanataka kufunga kwa makubaliano bali inaonekana ni kwa lazima.

Mwenyewe husika na vidio au nyimbo hiyo maoni yako kuwakomboa wafanyakazi na wananchi na nchi kwa ujumla

Tuesday, February 5, 2013

MWENGE ILIVYOTEKETEA KWA MOTO JANA

Baadhi ya wafanyabiashara eneo la Mwenge stendi ya daladala wakijaribu kuokoa mali zao baada ya maduka yao kuungua moto.
MADUKA kadhaa ya vipodozi, nguo yameungua moto na kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wake.
Moto huo umetokea mishale ya saa 5.20 leo asubuhi baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye moja ya kibanda cha biashara.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto huo ulianza taratibu kisha kupamba moto.
Wafanyabiashara wa maduka ya vipodozi ndiyo waliopata hasara kubwa kwa mali zao kuharibika kufuatia kutaka kuziokoa.

Hata hivyo, Kikosi cha Zima moto kilichofika eneo la tukio kwa wakati na kimepongezwa kwa kufanya kazi nzuri na kuweza kuudhibiti moto huo.
Adha, jeshi la polisi limepongezwa kwa kazi nzuri lililoifanya ya kudhibiti vibaka ambao walijiandaa kufanya uhalifu wa kuiba mali katika kurupushani hizo za uokoaji.
Askari wa Kikosi cha Zima moto akizima moto huo uliokuwa ukiunguza maduka ya vipodozi.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya maduka ya vipodozi yakiungua moto.
Wanausalama wakidumisha amani eneo hilo.

BREAKING NEWS: MSANII WA BONGO FLEVA BUI BUI APATA AJALI

Tweet toka kwa Mh.Zitto Zuberi Kabwe

So I miss this whole session of parliament! My question to be asked by on new licenses to north Mara mine and Mkuju uranium
Mheshimiwa Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma kaskazini anasikitika kukosa bunge la leo pale ukizingatia swali zuri toka kwa Mheshimiwa Tundu Lissu akiulizia juu ya vibali vipya ikiwemo mgodi North Mara na Mkuju Uranium

Na tweet toka kwa watu wakiendelea kutafuta ufafanuzi zaidi
  1. lukuvi na ndugai wanaboa sana
  2. Why are you missing the entire session??
  3. Kwanini unamiss? unahitajika sana bungeni kwani changamoto zako zinaifanya SERIKALI isijisahau
  4. Why you miss that session, So what are the feedback from Mh. Lissu

Monday, February 4, 2013

KARUECHE TRAN KWENYE ROLLING OUT NA RIHANNA KWENYE ROLLINGSTONE COVERS

Baada ya Karrueche Tran kwa mara ya kwanza kutokea kwenye magazine cover Rolling Out na kuingia mtaani, Rihanna ametokea kwenye cover ya Rolling Stone Magazine akiongelea mahusiano yake na Chriss Brown. Rihanna ameliambia gazeti hilo anasema “ Niliamua ilikuwa muhimu zaidi kwangu kuwa na furaha, Nisingeacha maoni ya mtu yeyote yaje kiivyo, hata kama ni kosa , kosa ni langu, baada ya kuchafuliwa sana kwa miaka mingi, kunifanya niwe nahasira na kuniweka gizani, bora niishi maisha yangu ya ukweli na kujibu mashambulizi. Naweza sana” Alisema Rihanna Na kuendelea kusema “ Ukiongeza kipande kutoka nje, sio tatizo sana duniani. Unatuona tukitembea kuelekea sehemu Fulani, kuendesha gari kuelekea sehemu Fulani, studio, club na unadhani unajua. Lakini ni tofauti sasa hivi, hatuna yale malumbano ya aina ile tena. Tunaongea kuhusu upuuzi, Tunaheshimiana. Tunajua kabisa nini tunacho sasa, na hatutaki kupoteza. Siwezi kusema hakuna kitu tena kitaenda kinyume lakini na uhakika itamshtua, Alisema Rihanna kupitia Rolling Stone Magazine.

PICHA MBALIMBALI ZA KUUNGUA JENGO LA PPF TOWER

Jengo la PPF Tower jana liliwaka moto na chanzo cha moto huo haijajulikana.Kwa maelezo zaidi na habari zaidi tutaendelea kuwapa.