NJOMBE

NJOMBE

Wednesday, May 29, 2013

SOMA ALICHOKISEMA BUSHOKE AKIWA SOUTH AFRIKA KUHUSU KIFO CHA NGWAIR

Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia jana. Inadaiwa kuwa Mangwea alikuwa pamoja na mtu aitwaye M TO THE P ambaye naye yupo mahututi kwa sasa.



Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki jana jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi amefariki akiwa usingizini.



Akiongea na Clouds FM , mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia jana Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.

“Sijui hata huko alitumia nini,” amesema.

Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.

Hata hivyo amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi jana nchini.

Awali Tulizungumza na Bushoke anayeishi jijini Pretoria ambaye amesema alikuwa akutane naye Jana jijini Johannesburg lakini alishangaa kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washkaji ambao ni wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki.

“Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke.

Bushoke amesema leo amepanga kwenda Johannesburg kujionea mwenyewe.

Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Kilimanjaro Lager ‏

Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji. Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.

Ndovu Special Malt

R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many Tanzanians.

Adam Nditi

Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta #RIP #Mangwair #akaCowbama

Diva ‏

Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?

 
Makali Machechi
Duuuuuu jamani Ngwear mungu ailaze roho yako mahala pema peponi amina.siajataka kuamini hadi siku ya mazishi ndio nitajuwa kweli umetutoka RIP Ngwear
 
Clever
 
R.I.P Cowboy mwana Chamber

1 comment:

  1. kifo cha magwear ni cha ghafla na kimesikitisha watu wengi
    Rest In Peace

    ReplyDelete