NJOMBE

NJOMBE

clock

Tuesday, March 19, 2013

STAMINA AFUNGUKA JUU YA UANDISHI WA MASHAIRI A.K.A MISTARI NA DAU LINAKWENDAJE
Baada ya kusumbuliwa sana na wasanii wachanga na wasanii wakubwa tu katika game la mziki wetu, kumtaka awaandikie nyimbo, Stamina ameamua kufunguka na kusema sasa ni wakati wa kuanza kutoza hela katika uandishi, baada ya kuandika hits kadhaa alizogoma kuzitaja..
"kuna swala moja nataka niliweke wazi, maana toka mwakajana mwishoni nasumbuliwa sana na watu wa kawaidaa, wasanii wa kawaida na wasanii wengine wakubwa tu amabao sitaki kuwataja, wamekuwa wakinitaka niwaandikie nyimbo, wengine wanauliza kabisa bwana utatuchaji sh ngapi, wengine wanataka kisela, na kuna baadhi ya hit songs nimeziandika...
"mwisho wa siku leo nataka nitangaze wazi kwamba, mtu yeyote atakaetaka nimwandikie wimbo, aidia ikiwa yake, naandika wimbo mmoja wenye verse 3 kwa 2,50,000 aidia ikiwa yake, na aidia ikiwa yangu yaani anataka kila kitu niandike mimi, yeye anataka tu wimbo naandika kwa 300,000, hizi ni bei zangu nimeona bora niziweke wazi, maana nasumbuliwa sana na watu...kama ni mwanangu naweza mfanyia bure tu lakini kwa sasa bora niweke wazi tu."

No comments:

Post a Comment