NJOMBE

NJOMBE

Saturday, June 30, 2012

Msafara wa JK warushiwa mawe Kinondoni


MSAFARA wa Rais Jakaya Kikwete uliokuwa ukielekea Bagamoyo jana ulilazimika kusimama kwa muda baada ya kuzuka kwa vurugu kubwa za kurushiwa mawe katika eneo la Namanga Tegeta Manispaa ya Kinondoni jiji la Dar es salaam.
Wakazi wa eneo hilo walifunga barabara kwa muda, na hivyo kuzuia msafara wa Rais Kikwete kwa kile walichodai aweze kuona namna matajiri wanavyotumia uwezo wao wa kifedha kuwanyanyasa raia wanyonge.
Vurugu hizo zilisababisha mabaunsa wawili kujeruhiwa vibaya na wananchi na wamelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.
Vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya saa mbili, zilitokana na kitendo cha watu (mabaunsa) wanaoaminika kukodiwa na mmiliki wa kituo cha mafuta cha GAPCO aliyetajwa kwa jina Hemed Salum, kuvunja nyumba zao na mfanyabiashara huyo.
Hata hivyo, msafara huo wa Rais uliweza kuendelea baada ya askari wengi kumwagwa na kuanza kuwatawanya wananchi waliokuwa na hasira.
Wakiongea kwa hasira, wananchi hao walidai kuchoka na vitendo wanavyotendewa na baadhi ya wawekezaji.
“Watu wenye pesa wanafanya kila wanaloliona kuwa linawafaa bila hata kujali sheria za nchi, sasa sisi wananchi tulifanya makusudi ili Rais aone mambo tunayofanyiwa na hawa wawekezaji atusaidie, lakini kinyume chake tunapewa bakora,” alisema mwananchi mmoja ambaye hakupenda kutajwa jina lake.
Watu waliobomolewa nyumba zao wamesema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha mmiliki wa kituo hicho kuwavunjia nyumba zao akidai kuwa wamejenga kwenye eneo lake.
“Hili eneo ni letu tunalimiki kihalali, kwani tuliachiwa urithi na baba yetu na sisi tuko watoto kumi, kila mmoja alipewa eneo lake tukajenga, na eneo la barabarani halikuwa letu hivyo aliuziwa yeye (Salum) na mtu mwingine akajenga kituo cha mafuta.
“Kinyume chake ametafuta nyaraka za kugushi na kuanza kudai kuwa sisi tunaishi katika eneo lake tuondoke tumwachie, lakini hakuna mtu yeyote asiyejua kwamba eneo hili ni letu na tumeachiwa urithi na baba yetu,” alisema Fikiri Saidi mmoja wa waliobomolewa nyumba huku akitokwa na machozi.
Fikiri aliongeza kwamba kabla ya tukio hilo siku mbili zilizopita, mmiliki huyo aliwafuata nyumbani kwao kwa lengo la kutaka wamuuzie eneo hilo kwa shilingi milioni 100 ili wagawane lakini walikataa, ndipo akatoa vitisho akiwambia kuwa, kwa kuwa wamekataa pesa hizo atawapa wanaozihitaji ili wabomoe na hawataambulia kitu chochote.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alisema polisi wanamshikilia mmiliki huyo kwa kosa la kujichukulia hatua mkononi na kuwavunjia wakazi hao nyumba na kusababisha upotevu wa mali.
Hata hivyo, Kenyela alisema polisi watafanya msako wa watu waliohusika kupopoa mawe msafara huo, huku akiwataka wakazi hao kuwa watulivu wakati serikali ikiangalia namna ya kuwatafutia hifadhi ya muda.
Watu walioathirika na tukio hilo ni Fikiri Saidi, Rashid Said, Farida Said na Ally Mkwandu, wengine ni Shabani Said, Kassim Said, Sijali Said Rajab Said na Waziri Rashid, ambapo inakadiriwa kuwa thamani ya nyumba na mali zilizoharibiwa inafikia zaidi ya sh milioni 300.
Chanzo cha Habari Tanzania daima

Friday, June 29, 2012

Wageni watekwa wakiwa kambini Kenya

Polisi nchini Kenya wamesema kuwa wafanyikazi sita wa shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wametekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Ifo ilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Dadaab
kambi hiyo inatoa hifadhi wakimbizi nusu milioni
Waliotekwa ni wafanyikazi wa shirika la Norwegian Refugee Council, ambalo linatoa huduma kwa wakimbizi kutoka Somalia wanaoishi kwenye kambi hiyo.
Hata hivyo shirika hilo halijatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo na watu waliotekwa.
Mkuu wa wilaya ya Lagdera ambako kambi hiyo ipo Robert Kimanthi amesema waliotekwa ni raia wa Canada, Norway, Mfilipino, Mpakistani na Wakenya wawili. Wote ni wanaume.
Kulingana na polisi watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki walishambulia msafara wa magari katika kambi hiyo ambayo inatoa makaazi kwa zaidi ya wakimbizi nusu milioni kutoka Somalia. Mtu mmoja aliuawa kwenye tukio hilo.Dadaab
Polisi wanashuku kuwa wapiganaji wa kiisalamu wa Al shaabab walihusika na shambulio hilo.
Visa vya mashambulio ya kigaidi vimeongezeka katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya, baada ya wanajeshi wake kuingia nchini Somalia mwaka jana kupambana na wanamgambo wa al shabaab.
Katika miezi ya hivi karibuni, wafanyakazi kadhaa wa mashirika ya kutoa misaada wametekwa nyara katika kambi hiyo ya Daadab.
Wawili kati yao ni wanawake wawili raia wa uhispania ambao walitekwa nyara mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Dawa mpya kwa wagonjwa wa Ukimwi

Baadhi ya dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi
Huenda wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani.
Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao.
Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
Watafiti pamoja na kampuni za dawa wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.
Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.
Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya Wanawake ya Brigham huko Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha afya ya wagonjwa.
Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.
Licha ya mafanikio ya sasa watafiti wanasema raia wengi hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi na maambukizi bila kujua.

WENGI WAHUZUNISHWA NA KILICHOMPATA DR. ULIMBOKA: HIKI NDICHO ALICHOANDIKA FID Q -FACEBOOK

 Fareed Kubanda a.k.a Fid Q
 
"Maisha yako temporary kwahiyo UHAI ni kibarua/ tunashukuru hakumwagiwa TINDIKALI na hawakufanikiwa kumuua/tujiunge na MADAKTARI kumuombea 'ULIMBOKA' dua.."  Fid Q
 Hii ndiyo hali ya Dkt. Ulimboka baada ya kutekwa na kupigwa sana
 Wa pili kushoto ndiye Dkt. Ulimboka kijana mtanashati lakini sasa amejeruhiwa vibaya

TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA


YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012

Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka ,

Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja

Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.


Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!

Imetolewa na
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

Wednesday, June 27, 2012

Wahamiaji 42 wafa kwenye lori Tanzania

Tanzania
Tanzania
Wahamiaji haramu arobaini na wawili wamepatikana wakiwa wamekufa ndani ya lori walimokuwa wakisafiria katika mkoa wa Dodoma, nchini Tanzania.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Pereira Silima, amesema kuwa watu hao waliokuwa wamesongamana ndani ya lori waliaga dunia kutokana ukosefu wa hewa safi.
''Taarifa tuliyopata ni kwamba kulikuwa na wasafiri waliokuwa wakisafirishwa kwenye lori, ambalo lilikuwa kama kontena na halikuwa na hewa ya kutosha''.Bwana Silima ameambia BBC.

wahamiaji walikuwa wanatoka Ethiopia

Amesema wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikuwa wakijaribu kuingia Malawi.
Kulingana na bwana Silima wahamiaji hao walianza kufariki dunia wakiwa safarini. Jihudi za wahamiaji hao kumjulisha dereva kuhusiana na hali yao hazikufanikiwa, na hivyo kusababisha maafa ya watu arobaini na moja ndani ya lori hilo.
Kulingana na naibu waziri huyo wa mambo ya ndani tukio hilo lilifanyika Jumatatu usiku. Na baada ya dereva huyo kugundua kuwa watu wamefariki, aliondoa miili yao na kuitupa nje kabla ya kutoweka.
Mtu mmoja alifariki dunia akifanyiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Dodoma.

uhamiaji haramu umeenea

Polisi nchini Tanzania wamesema wanamsaka dereva huyo ambaye alitoroka punde tu baada ya kushusha miili ya wahamiaji hao haramu.
Biashara ya kuwasafirisha wahamiaji haramu hasa wanaotoka nchi za Somalia na Ethiopia kupitia Tanzania imeenea sana. Wengi huelekea mataifa ya kusini mwa Africa kutafuta maisha bora.

Marekani yataja makundi hatari Afrika

wapiganaji wa kiisilamu
Makundi matatu ya kigaidi Barani Afrika yameanza kushirikiana katika harakati zao. Hii ni kwa mujibu wa Mkuu wa jeshi la Marekani anayesimamia shughuli za usalama kanda ya Afrika. Jenerali Cater Ham amesema kundi la Al Qaeda Afrika Kaskazini limekuwa likiwasaidia wanachama wa Boko Haram nchini Nigeria na mabomu.
Akizungumza mjini Washington afisa huyo amesema waasi wanaodhibiti kaskazini mwa Mali wameendelea kutumia eneo hilo kuendesha harakati zao ikiwemo kupanga njama za kutekeleza mashambulio.Jenerali Ham ni kamanda wa kitengo cha idara ya ulinzi ya marekani kinachofuatilia masuala ya usalama barani Afrika{Africom} na makao makuu yako Ujerumani.
Kitengo hiki kinaimrisha harakati zozote za kijeshi Afrika ikiwemo mashambulio ya kutumia ndege bila rubani dhidi ya wapiganaji wa Kisomali wa Al shabaab.
Tayari kuna wanajeshi 100 wa Marekani wanaosaidia kumsaka kiongozi wa waasi Uganda Joseph Kony ambao wanasimamiwa na kitengo cha Jenerali Ham.
Afisa huyo ametaja makundi hatari zaidi ikiwa ni pamoja na kundi la Al Qaeda Afrika Kaskazini{AQIM}, Boko Haram na Al-Shabab.
Ameongeza tisho kubwa ni kwamba makundi haya yameanza kushirikiana katika kufanikisha harakati zao.
Mapema mwaka huu nchi ya Mali ilishuhudia mapinduzi ya kijeshi na kufuatiwa na kudhibitiwa kwa eneo nzima la Kaskazini na makundi yanayotetea kujitenga ya Tuareg na wapiganaji wa kiisilamu.

Tuesday, June 26, 2012

Maporomoka yahofiwa kuuwa wengi

Bududa, Uganda
Bududa, Uganda
Shughuli za uokozi zinatarajiwa kuanza tena leo asubuhi mashariki mwa Uganda ambako vijiji vitatu vilifunikwa na udongo kufuatia maporomoka ya udongo yaliyokumba eneo la Bududa.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Uganda limesema kuwa zaidi ya watu kumi na wanane wamefariki dunia katika maporomoko hayo.
Zaidi ya nyumba kumi na tano zimezikwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo.
Shirika hilo limesema maafisa wake wanaendelea kuwatibu waliojeruhiwa katika mkasa huo, katika eneo hilo lenye rutuba la Bududa, linalokuza kahawa na lililopo karibu na mbuga ya wanyama ya mlima Elgon.

nyumba zimefunikwa futi16 chini

Mwandishi wa habari, Stephene Mulaa, aliyezuru eneo la tukio amesema kuwa, ''kufikia jana jioni hakuna mwili hata mmoja ulikuwa umepatikana, kwa sababu inakadiriwa kwamba miili ya watu na nyumba zilizofunikwa na udongo ziko zaidi ya futi kumi na sita kwenda chini''

serikali kuwasaidia walioathirika

Serikali ya Uganda inatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusu janga hilo baadaye hivi leo.
Lakini kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, serikali imesema kuwa,'' inafanya juu chini kuhakikisha kuwa familia zilizoathirika zinapata msaada wa kutosha''.
Waziri anayehusika na maswala ya majanga, Dr Steven Malinga, amenukuliwa katika taarifa akisema kuwa hakuna madhara makubwa yaliyoripotiwa.
Mwaka 2010, maporomoko mengine ya ardhi yalitokea katika wilaya hiyo ya Bududa, na kuwauza zaidi ya watu mia tatu.
Eneo hilo linazungukwa na miinuko pamoja na mabonde, kando kando ya mlima Elgon, na hupokea mvua kubwa katika msimu wa masika.
Serikali imewashauri wakazi katika maeneo hayo kuhamia maeneo salama lakini wengi wamekataa kufanya hivyo wakihofia kupoteza mashamba yao yenye rotuba.

Mohammed Mursi kuunda serikali mpya


Mohammed Musri akifanya sala

Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri Mohammed Mursi, anaanza kuunda serikali mpya baada ya kuahidi kuwa kiongozi wa raia wote wa Misri.
Viongozi wa dunia wamempongeza Kiongozi huyo aliyeungwa mkono na mrengo wa Muslim Brotherhood baada ya kumshinda Waziri Mkuu wa zamani Ahmed Shafiq.
Bw Musri anatarajiwa kuapishwa rasmi hapo Juni 30, japo kuna hoja kuhusiana na madaraka gani anapata.
Watawala wa kijeshi wamedhibiti madaraka mengi anayopata Rais pamoja na kufuta bunge.
Kwenye hotuba yake ya ushindi, Mursi aliwahakikishia raia kuwahudumia wote bila kubagua.
Mohammed Mursi anaanza kuunda serikali ya kiraia lakini macho yote yanatazaman chaguo lake la Waziri Mkuu.
Mwandishi wa BBC Jon Leyne mjini Cairo amesema kuwepo na mazungumo na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Mohamed ElBaradei, ambaye atatuliza wasi wasi wa mrengo usiopendelea sheria za dini na vijana.
Mursi ameahudi kuwateuwa manaibu wake na mawaziri kutoka pande zote.

Wahamiaji haramu wafa maji Malawi

Polisi nchini malawi wanasema wahamiaji haramu hamsini wameaga dunia baada ya mashua walimokuwa wakisafiria kuzama kaskazini mwa nchi hiyo.
Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya wakimbizi UNHCR, limesema walioangamia ni raia wa Ethiopia.
Inaaminika kuwa saidi ya watu sitini walikuwa ndani ya mashua hiyo.
Mwandishi wa BBC nchini humo, anasema kwa sasa ni msimu wa baridi na hakuna dalili ya kupata manusura zaidi.
Meli hiyo ilizama katika ziwa Malawi siku ya jumatatu usiku, lakinin habari hizo zimeanza kutolewa kwa kuwa eneo hilo ni mbali na hakuna mawasiliano.
Wahamiaji wengi haramu kutoka mataifa ya pembe ya afrika huelekea nchini afrika kusini kupitia malawi.

Monday, June 25, 2012

Musri wa Muslim Brotherhood mshindi

Mursi
Mohamed Mursi

Mohammed Mursi ametangazwa mshindi katika uchaguzi wa Rais nchini Misri.
Mursi ameshinda kura kwa asili mia 51.7% akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.
Mkuu wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko 466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika.
Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi wengi wa Bw.Mursi walikua wamekuanyika.
Wafuasi hao wamekaa kwenye medani hio kwa siku kadhaa wakionyesha msimamo wao wa kuchukia sheria kadhaa zilizotangazwa na Baraza la juu la utawala wa majeshi ambayo wanadai zimeundwa ili kupunguza mamlaka ya Rais na kuelekeza uwezo mkubwa kwa majeshi.
Wafuasi wa Bw.Shafiq nao waliweka kambi yao katika eneo la kaskazini mwa mji ambako kuna makao makuu ya Tume ya uchaguzi huko Nasser City.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi Jaji Sultan alianza kwa kunena kua tangazo la matokeo ya uchaguzi yalikua yamezongwa na shinikizo pamoja na hali ya wasiwasi.
Wafuasi washangilia Cairo
Wafuasi washangilia Cairo
Tume ya uchaguzi ilizingatia sheria ilipochunguza visanduku vya kupigia kura, na Jaji.Sultan alisema hakuna kilicho juu ya sheria.
Jaji huyo akaongezea kukanusha madai mawili nyeti kuhusu njama za kuibia uchaguzi, kwamba baadhi ya karatasi za kupigia kura ziliwekwa ndani ya visanduku tayari zikiwa na majina ya mgombea wanayemtaka ashinde.
Hatimaye Jaji Sultan akamtangaza mshindi kua ni Bw.Mursi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Muslim Brotherhood cha Freedom and Justice, Bw.Mursi.
Baada ya dakika kadhaa akitangaza marekebisho kuhusu matokeo madomadogo ya kura ndipo akamtangaza Bw.Mursi kua mshindi kwa kuzoa kura 13,230,131, na Bw.Shafiq akiweza kuzoa 12,347,380, sawa na asili mia 48.27%.

Sunday, June 24, 2012

GARI LA BIA TBL LADONDOKA MJINI SUMBAWANGA WANANCHI WAKIMBILA GARI NAKULEWA CHAKARI!








imetokea jana jumamosi asubuhi majira ya saa tatu asubuhi baada ya gari ya kampuni ya Kanji Ladji inayobeba bia iliokuwa inatokea Mbeya kwenda Sumbawanga ikiwa imesheheni vinywaji kupata ajali na kuanguka majira ya saa tatu asubuhi.Sumbawanga ilikuwa kama sherehe kwa wengine kwani wanakijiji walivamia gari na wakaruhusiwa kunywa watakavyo ila hakuna kuondoka na chupa.....asubuhi watu walikuwa wamelewa chakari...Maisha bora kwa kila Mtanzania..

Saturday, June 23, 2012

DIANA HUSSEIN AFANIKIWA KUNYAKUA TAJI LA MISS DAR INDIAN OCEAN 2012!

 Mrembo Diana Hussein (kati) amefanikiwa kunyakua taji la Miss Dar Indian Ocean kutoka kwa mwanadada Stella ambaye amemaliza muda wake, mwanadada huyu alifuatiwa na Kudra Lupatu (kulia) na Zulfa Vuai (kushoto). Shindano la Miss Dar Indian Ocean 2012 limefanyika ndani ya Kijiji Cha Makumbusho Dar es Salaam
Hawa ndiyo warembo wa Tano Bora wakiwa na Miss Dar Indian.
 Warembo waliofanikiwa kuingia tano bora.
Warembo waliofika 10 bora kabla ya kuingia kwenye mchujo wa kutafuta tano bora.

Wabunge watahiriwa kupunguza HIV

Wabunge karibu 10 nchini Zimbabwe wametahiriwa kama moja wapo ya hatua zao ya kukabiliana na kusambaa kwa virisi vya Ukimwi nchini humo
Zahanati walipotahiriwa wabunge ,Zimbabwe
Njee ya majengo ya bunge mjini Harare , kulijengwa zahanati ndogo kwa sababu ya shuhuli hizo za kuwapasha wabunge tohara.
Blessing Chebundo, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanaopambana na Ukimwi amesema nia yake hasa ya yeye kuamua kupashwa tohara ni kuchochea wanaume nchini Zimbabwe kutairiwa.
Bwana Chebundo anasema kuna wabunge zaidi ya 120 na wafanyikazi wa bungeni ambao wameonyrsha nia yao ya kutairiwa.
Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza atari ya wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 60.
Zimbabwe ni moja wapo wa mataifa 13 barani Afrika ambapo mwaka wa 2007 shirika la WHO inasema kuna haja kubwa ya kuanzisha harakati za kuwatahiri wanaume.
Jana, wabunge hao walijitokeza hadharani ili kupimwa hali yao ya Ukimwi.
Wabunge hao wanachochea wanaume nchini Zimbabwe kukubali kutahiriwa, kama njia mojawapo ya kupumguzu maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Hii nikutokana na takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa karibu robo ya wanaume wote nchini Zimbabwe wameambukizxwa virusi.

Maelfu waandamana Misri dhidi ya Jeshi

Waandamanaji Misri
Melfu ya waandamanaji wamefurika katika medani ya Tahrir mjini Cairo, Misri kulaani watawala wa kijeshi kwa kujiongezea madaraka makubwa. Wiki iliyopita watawala wa kijeshi walifuta bunge na kujilimbikizia mamlaka ya kutunga sheria.
Raia wa Misri wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa Urais ambao mgombea wa mrengo wa Muslim Brotherhood Mohammed Mursi anataka yatolewe mara moja.
Wanajeshi wametetea hatua yao wakisema inasaidia kukabiliana na tisho lolote la usalama. Katika taarifa kupitia runinga ya taifa, Baraza la utawala wa Kijeshi limelaumu mgawanyiko wa kisiasa ulioko nchini kwa kusababisha ucheleweshwaji wa matokeo hayo.
Baraza hilo halijataja lolote kuhusu mgombea wa chama cha Freedom and Justice ambacho hapo Jumanne kilisema bw Mursi alikua ameshinda uchaguzi kwa asili mia 51.7.
Mpinzani wake Ahmed Shafiq ambaye aliwahi kua Waziri Mkuu ametangaza pia kushinda.Makundi yanayotetea sera isiyofuata dini na wanaharakati wa kiisilamu wameitikia maandamano yaliyoitishwa na Muslim Brotherhood baada ya sala ya Ijumaa.
Viongozi wa kidini walioongoza maombi katika medani ya Tahrir walisema Mohammed Mursi ndiye mshindi katika raundi ya pili ya uchaguzi wa pili.Akihutubia waandishi wa habari Mursi alisema atakubali matokeo ikiwa shughuli nzima itafanyika kwa njia ya uwazi.
Aliongeza endapo atatangazwa Rais atahakikisha Misri inapata Waziri Mkuu anayeungwa na pande zote.
Shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema mzozo wa sasa unavunja matumaini ya kuyakabidhi madaraka kwa raia nchini Misri na hivyo kuyumbisha mchakato wa demokrasia.

Friday, June 22, 2012

Marekani inazuia ripoti kuhusu uasi DRC

                                                                      Bosco Ntaganda
Marekani iinauzuia kutolewa kwa ripoti muhimu kuhusina na waasi wanaoongozwa na Jenerali wa jeshi anayesakwa na Mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la kutetetea haki za binadamu Human Rights Watch.
Shirika hilo limesema Marekani imekuwa ikipinga kutolewa kwa ripoti ya harakati za waasi wanaoongozwa na Bosco Ntaganda Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tayari Umoja wa Mataifa umetoa taarifa inayoangazia jinsi Rwanda ambayo ni mshirika wa karibu wa Marekani imekuwa ikifadhili waasi Mashariki mwa Congo.
Hata hivyo Marekani imekanusha kuzuia kutolewa kwa ripoti hiyo.Ripoti hiyo ilitarajiwa kutolewa siku kadhaa zilizopita na jopo maalum{Group of Experts}.
Vuguvugu la sasa linaongozwa na Jenerali Bosco Ntaganda aliyeasi jeshi la Congo pamoja na baadhi ya maafisa wengine wa jeshi.
Ntaganda ameripotiwa kudhibiti eneo karibu na mpaka na Rwanda. Makundi mengi ya waasi wa Congo yamekuwa yakifadhili harakati zao kutokana njia za magendo hususan mauzo ya madini.
Maelfu ya raia mashariki mwa Congo wamekimbia makaazi yao kutokana na harakati za jeshi la serikali na makundi ya waasi.

Thursday, June 21, 2012

Pope Benedict XVI ataka amani Nigeria


Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Papa Benedict XVI ametoa wito wa kokomeshwa kwa kile alichokitaja kama mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wakrito nchini Nigeria.
Papa Benedict XVI aomba utulivu Nigeria

Kiongozi huyo alikuwa akizungumza mjini Vatican wakati wa hotuba yake ya kila wiki.
Siku ya jumapili makanisa matatu yalishambuliwa na watu wa kujitolea mhanga na kusababisha vifo vya watu 16.
Wanaharakati wa Boko Haram walidai kuhusika na shambulizi hilo.
Kutokana na shambulizi hilo la jumapili ,kumekuwa na mashambulizi mwengine ya ulipizaji kisasi katika miji ya Kaduna na Damaturu na kusababisha vifo zaidi.
Lakini katika hutuba yake Papa Benedict amewataka wa-Nigeria wajenge jamii iliyona maelewano.
Amsema amekuwa akifuatilia kwa masikitiko makubwa yale yanayotokea nchini Nigeria ambapo mashambulizi ya kigaidi yanaendelea hasa yakielekezwa kwa wa-kristo.
Papa ametaka hali hiyikomeshwe ili kuzuia umwagikaji zaidi wa damu nchini humo.

Matokeo ya uchaguzi yahairishwa Misri

Tangazo la matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwishoni mwa wiki limehairishwa, hii ni kulingana na taarifa kwenye televisheni ya kitaifa.
wafuasi wa Mohammed MursiMatokeo hayo yalikuwa yatangazwe alhamisi, lakini tume ya uchaguzi imelazimika kuhairisha tangazo hilo ili kushughulikia malalamiko yaliowasilishwa na wagombea.
Mgombea wa muslim brotherhood anadai ushindi
Wagombea hao Mohammed Mursi na Ahmed Shafiq wote wamedai kushinda uchaguzi huo.
Kulingana na tume ya uchaguzi jumla ya malalamiko 400 yamewasilishwa lakini haijasema matokeo hayo yatatangazwa lini.
Msemaji wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, Nader Omran amesema kuwa tangazo hilo halifai kuhairishwa.
"Hatua hii itachochea hali ya wasiwasi itakuwa bora zaidi suala hili limalizwe alhamisi" amesema Bw Omran.
Wasimamizi wa kampeni ya mgombea wa Muslim Brotherhood, Mohammed Mursi wanasema kuwa kura zinaonyesha kuwa alishinda duru hiyo ya pili ya uchaguzi.
Lakini mshauri wa karibu wa Ahmed Shafiq, amewaelezea waandishi wa habari mjini Cairo kuwa, Shafiq- aliyekuwa waziri mkuu chini ya Utawala wa rais Hosni Mubarak-alishinda uchaguzi huo.
Maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani ya Tahriri tangu juzi kulaani baraza kuu la jeshi ambalo juzi limejilimbikizia mamlaka baada ya mahakama kuu kulivunja bunge la nchi hiyo.

Wednesday, June 20, 2012

Ahukumiwa jela maisha kwa kumuua Malkia

Majaji katika mahakama ya ICTR
Mahakama ya kimataifa inayochunguza mauji ya kimbari nchini Rwanda{ICTR} imemhukumu mwanajeshi wa zamani kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na mauaji hayo ya mwaka 1994.
Ildephonse Nizeyimana,alipatikana na hatia ya kuamrisha mauaji ya aliyekuwa Malkia wa jamii ya Tutsi Rosalie Gicanda pamoja na mauaji mengine.Nizeyimana alikamatwa nchini Uganda mwaka wa 2009.
Aliongoza kitengo cha ujasusi na operesheni za jeshi katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha ESO,wakati wa mauaji ya kimbari.
Mahakama hiyo iliyoko mjini Arusha, Tanzania ilimpata na hatia mwanajeshi huyo wa zamani ambapo aliamrisha mauaji ya raia kadhaa akiwemo malkia huyo wa Tutsi.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch mwaka wa 1999, wanajeshi wa Ki-Hutu walimchukua Malkia huyo kutoka makaazi yake Kusini Mashariki katika mji wa Butare na kisha kumpiga risasi nyuma ya jumba la makumbusho.
Pia waliwaua wanawake wakadhaa waliokuwa wajakazi wa malkia huyo.Marehemu alikuwa mjane wa Mfalme Mutara III, aliyefariki dunia mwaka wa 1959 kabla ya nchi hiyo kutangazwa jamuhuri.
Mahakama ya ICTR ilibuniwa kuwafungulia kesi wafadhili na washiriki wa mauaji ya kimbari. Tayari imewahukumu watu 54 na kuwaachia huru wanane. Mahakama hiyo inafunga shughuli zake baadaye mwaka huu.

Sheria ya kutotoka nje yatangazwa Nigeria

Maafisa wa Nigeria wametangaza sheria ya kutotoka nje katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Damaturu kufuatia makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa kisiilamu na pia sheria hiyo imerejeshwa tena katika jimbo la Kaduna.
Makabiliano kati ya jeshi na wapiganaji wa kiisilamu eneo la Damaturu yalianza Jumatatu, siku moja baada ya kutokea mashambulio ya mabomu yaliyolenga makanisa jimbo la Kaduna na kudaiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram.
Ramani ya jimbo la YobeMashambulio ya Boko Haram yalisababisha vifo vya watu 16 na kuchochea machafuko ya kulipiza kisasi ambapo makumi ya watu waliuawa.
Afisa mmoja katika hospitali ya Damaturu ameambia shirika la habari la AFP kwamba usalama umezorota na imekuwa hatari kwa wafanyikazi kuondoka hospitalini.
Polisi wa Nigeria wamelaumu Boko Haram kwa kulenga vituo vyao na jeshi ambapo maafisa watano waliuawa eneo la Damaturu hapo Jumatatu.
Rubaa za karibuni zinasema milio ya risasi imepungua katika jimbo la Yobe. Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa polisi jimbo hilo Patrick Egbuniwe.
Damaturu,ni makao makuu ya jimbo la Yobe ambalo , Magharibi mwa jimbo la Maiduguri na ngome kuu ya Boko Haram.
Jina la Boko Haram linamaanisha kwamba elimu ya kisasa ni haramu. Kundi hilo linashinikiza sheria ya kiislamu {Sharia} kutangazwa kote nchini Nigeria na limetekeleza mashambulio makali nchini humo.

Mubarak yupo 'hali taabani'

Taarifa za kutatanisha zimeibuka kuhusu afya ya Hosni Mubarak aliyeondolewa madarakani kufuatia maandamano ya kutaka mageuzi nchini Misri mwaka jana.
Hosni Mubarak
Baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa uhai wake unasitiriwa kwa kutumia mashine baada ya kuhamishwa kutoka gerezani hadi kwenye hospitali ya kijeshi mjini Cairo.
Mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha jela

Mubarak mwenye umri wa miaka 84 aliugua kiharusi akiwa jela, hali iliosababisha ahamishwe hadi hospitalini akiwa mahututi.
Kiongozi huyo aliondolewa mamlakani mwaka jana kufuatia maandamano ya raia wa nchi hiyo yakupinga utawala wake.
Mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuamrisha mauaji ya baadhi ya waandamanaji hao.
Mara kadhaa kumekuwepo na taarifa za kutatanisha kuhusu afya ya rais huyo wa zamani lakini kila mara zimepuuzwa.
Taarifa hizo kuhusu afya yake zimetokea wakati ambapo maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kwenye bustani ya Tahrir kulaani uamuzi wa baraza la kijeshi wa kujilimbikizia mamlaka.
Maandamano hayo yamepangwa na viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood. Mgombea wa kundi hilo wa kiti cha urais Mohammed Musri anadai kushinda uchaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Lakini pia mpinzani wake ambaye pia alikuwa waziri mkuu chini ya utawala wa Rais Mubarak, Ahmed Shafiq naye anadai ushindi.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatanzagwa alhamisi.
Vuguvugu la Muslim Brotherhood limeahidi kumfungulia mashtaka mapya Hosni Mubarak punde tu litakapo pata madaraka na linataka ahukumiwe kifo.

Detroit man gambles away $1.5 million accidentally given by ATM

(Alan Diaz/AP)
Ronald Page seemingly had it made when Bank of America unintentionally changed his account status, allowing the 55-year-old man to make unlimited ATM cash overdraft withdrawals.
But ABC News reports that Page, who in reality had only $300 in his checking account, used the accidental loophole to withdraw more than $1.5 million—losing it all on gambling.
And even worse for Page, the U.S. Attorney's Office in Detroit says he is now facing 15 months in prison after pleading guilty to charges of theft of bank funds, $1,543,104 in total between December 1, 2008 and May 31, 2009.
"In this case, the bank's glitch allowed the defendant to lose a significant amount of money that was not even his in the first place," reads the U.S. Attorney's sentencing memorandum, obtained by ABC. "The fact that defendant acted on an impulse does not minimize the seriousness of his conduct and the need for a custodial sentence."
The day the Bank of America glitch went into effect, Page reportedly withdrew $312,000 from ATMs at the Greektown Casino in Detroit and an additional $51,727 from the MGM Grand Casino. Bank of America placed a hold on his account 17 days later, but he had already withdrawn $1.5 million by that point.
Ronald Page (Local 10)
The glitch reportedly occurred because Page originally had a banking account with LaSalle Bank. When Bank of America acquired LaSalle, the glitch somehow occurred while the two banking institutions were transferring account information.
Page, who does not have a prior record, could have faced a steeper sentence but prosecutors said his crime was a "lapse of judgment" and placed blame with Bank of America for allowing the withdrawals to take place.
In addition to the recommended 15-month sentence and order to repay the funds, the U.S. Attorney's Office has suggested that Page be prohibited from gambling in any capacity.
"If his gambling addiction is not addressed, he is very likely to cause further financial hardship to himself and his family," the memorandum reads.

Tuesday, June 19, 2012

Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa


Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia.
Neno Dyspareunia tamka (dis-pa-roon-ia) linatokana na neno la kigiriki lenye maana ya shida katika kuingiliana wakati wa kufanya tendo la ndoa (difficulty mating au badly mated).

Utafiti unaonesha kwamba kati ya wanawake watatu, wawili wamewahi au hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Imefika kwamba baadhi ya ndoa, mwanamke anapata maumivu kiasi cha kutokuwa na hamu tena ya tendo la ndoa na matokeo yake wamekuwa na wakati mgumu linapokuja suala la kufanya mapenzi na pia kila wakirudia kufanya tendo la ndoa, mambo ni yamekuwa ni yaleyale kwa mwanamke kuumia zaidi kuliko mara ya kwanza.

Kawaida huwa haifurahishi kabisa na haina hata ladha kufanya tendo la ndoa huku mmoja kati yenu akiwa anapata maumivu makali au shida hiyo husababisha kutojishughulisha katika kuleta raha ya kweli na hatimaye kuridhishana kimapenzi wakati wa tendo la ndoa.
Tendo la ndoa halikuwekwa ili kukupa shida au maumivu bali kukupa raha, furaha na kuridhishwa.
Moja ya kanuni muhimu sana katika tendo la ndoa ni
K
ama unapata maumivu usifanye
Badala yake tafuta nini kimesababisha na tafuta jibu sahihi la kuondoa hiyo hali au muone daktari akusaidie.
Na baada ya kupata tiba na kupona ndiyo unaruhusiwa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kufurahia na kukupa raha zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuleta maangamizi.

Ni kweli kwamba kama moja wapo ya mahitaji ya msingi ya kihisia (emotions) kama hili la tendo la ndoa halipatikani katika ndoa linaweza kusababisha mmoja ya wanandoa kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake na kutoka nje kwenda kutafuta mtu wa kumridhisha zaidi, hata hivyo kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa huku anapata maumivu au kuumia kwa kuogopa kwamba asipompa Mume wake haki yake basi anaweza kutoka nje na kutokuwa mwaminifu hilo si sahihi kwani ni kutojiamini na kutojali si afya yako tu bali haki yako ya msingi ya kufanya tyendo la ndoa kwa kupata raha.
Mnahitaji kujulishana na kuelezana ukweli ili muweze kupata dawa na hatimaye kurudi kwenye raha upya badala ya kuumizana.

Kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke au hata mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na inaweza kuwa ni wakati mwanaume anapoingia (penetrate) au wakati wa kitendo chenyewe au baada ya kitendo chenyewe.
Inaweza kuwa ni maumivu makali sana au inaweza kuwa ni kuwashwa au inaweza kuwa ni maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida au inaweza kuwa ni maumivu ambayo unasikia
kama moto unawaka vile ndani yako wakati wa tendo la ndoa.

 Sasa pata sababu zinazosababisha Maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke
1. Fibroids; uvimbe katika kizazi unaowatesa wanawake Tanzania
KATIKA siku za hivi karibuni, wanawake nchini wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokwenda kujifungua basi hukutwa na uvimbe katika nyumba ya uzazi.

 Uvimbe huo, ambao si saratani, umekuwa ni tishio kwa maelfu ya wanawake nchini jambo linalosababisha wengi wao kuondolewa vizazi vyao.

Daktari Bingwa  wa magonjwa ya uzazi wa kitengo cha Patholojia wa Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili, Henry Mwakyoma, anaulezea ugonjwa huu na kusema kuwa  fibroids kwa kitaalamu ‘leimyoma’ ni uvimbe unaowapata asilimia 25 ya wanawake wa Kiafrika na asilimia 50 ya Wazungu.

“Nasisitiza kuwa, uvimbe huu  si saratani, unajitokeza ama katika ukuta wa kati, wa nje au ndani  kabisa ya nyumba ya uzazi,” anasema.

 Anasema; “uvimbe huu huwa katika umbile la misuli myembamba na laini  na hukua siku hadi siku,”  anabainisha Dk Mwakyoma  na kuongeza kuwa, sababu kuu ya ugonjwa huu,  bado haijajulikana.

 Anafafanua kuwa, pamoja na kuwa sababu kuu haijajulikana, lakini zipo sababu ambazo zimehakikiwa kusababisha  mwanamke kupata uvimbe wa fibroids.

“Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya ‘estrogen’ ambavyo vipo katika miili ya wanawake,” Anasema.

Dk Mwakyoma anafafanua kuwa, vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi.

“Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu, huwa ni wanawake walio katika balehe au ambao tayari wamevunja ungo, kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogen,” anabainisha mtaalam huyo.

Lakini, pia anasema kuwa endapo inatokea mwanamke akapata matibabu ambayo yatamtaka kuongezewe vichocheo hivi, huwa katika hatari ya kupata uvimbe huu.

 Aidha, daktari huyu anabainisha kuwa, ndiyo maana wanawake walio katika kikomo cha hedhi(menopause) na  watoto hawawezi kupata uvimbe huu.

Anazitaja sifa kuu za ugonjwa huu na kusema, huwa ni nyingi kwa sababu ni uvimbe ambao asili yake ni mishipa midogo midogo na inapokuwa huweza kufikia urefu wa sentimeta tano na zaidi na uzito wa kilogram 10.

Anaongeza kuwa, uvimbe huu unaweza kutokea katika kuta zote za kizazi cha mwanamke na kusababisha mwanamke ang’olewe kizazi chake.

“Hata hivyo, wanawake wengi hupata uvimbe huu katika ukuta wa ndani kabisa wa kizazi,” anasema.
 Anataja sifa nyingine za uvimbe huu ni kuwa na tabia yake ya kubadilikabadilika sana.

 Kwa mfano, fibroids huweza kubadilika rangi na kuwa ya njano, ikabadilika na kuwa katika hali ya kimiminika, baadaye kuwa ngumu au kuwa laini yenye kutomasika.

Dalili za Fibroids
Dk Mwakyoma anazitaja sababu za ugonjwa huu na kusema kuwa, ni vigumu mwanamke kubaini au kuhisi dalili zake.

“Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa, wengi hugundulika wakati wa kujifungua, na ujauzito au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi, basi huweza kutokwa damu kwa wingi,” Anasema.

 Anasema: “Hata hivyo, asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,”
Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi.
Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo  sana zikiambatana na maumivu makali.

 “Asilimia 30 ya wanawake wanaopata maumivu na damu nyingi  wakati wa hedhi huwa na uvimbe wa aina hii” anasema
Anasema wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.

 “Nina mifano hai, wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito, wakakosa kabisa siku zao za hedhi, wakapata dalili zote za ujauzito na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids,” anasema.

Anasema, mara nyingi uvimbe unaojitokeza katika ukuta wa nje wa kizazi na kuning’nia, ndiyo hucheza na kuleta dalili za ujauzito.

Mwanamke huweza kuvimba miguu kwa sababu uvimbe huu husababisha damu isitembee.
Anataja dalili nyingine kuwa ni mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

 Wakati mwingine, fibroids hukua na kuzuia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusababisha mwanamke avimbiwe.

Vile vile, uvimbe huo huweza kuzuia kibofu cha mkojo, na kumfanya mwanamke apate haja ndogo kwa taabu , au akatokwa na uchafu ukeni.

“Hatari kuu ya uvimbe huu ni ugumba, asilimia 27 hadi 40 ya wanawake wanaopata uvimbe katika kuta zote za kizazi, hushindwa kupata watoto,” anafafanua Dk Mwakyoma

 Hatari nyingine ni kwa wanawake wajawazito wenye uvimbe huu ambao wengi hufanyiwa upasuaji kwani fibroids huweza kuzuia mlango wa kizazi na mwnamke kushindwa kujifungua.

 Imebainishwa kuwa, asilimia 30 ya wanawake hutolewa vizazi mara baada ya kujifungua kutokana na uvimbe huu.

Mtaalam huyo anatahadharisha kuwa, wanawake walio katika umri wa kuzaa lakini hawazai wapo katika hatari ya kupata maradhi haya.

“Hii ni kwa sababu vichocheo vya estrogen hukua kwa wingi na kusababisha misuli ya fibroids kukua, lakini vichocheo hivyo huacha kukua wakati wa ujauzito,” anasema.

 Anataja walio katika hatari hii ni watawa ambao hawatakiwi kuzaa au wale wanaopitiliza umri wa kuzaa.
 Matibabu ya maradhi haya mara nyingi ni kufanyiwa upasuaji na kuondoa uvimbe huu au kutolewa kabisa kizazi.

“Hii inategemeana na umri wa mgonjwa, idadi ya watoto na maamuzi yake binafsi,” anasema
Katika mahojiano na Mwananchi na wanawake wenye umri tofauti waliowahi kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa fibroids, wengi wanauzungumzia kuwa ugonjwa unaosumbua.

 Mmoja wapo ni Janeth Ngaiza (23) ambaye anasema, alikuwa akitokwa damu wakati yu mjamzito, ndipo daktari alipomfanyia vipimo na kugundua uvimbe huo.

“Kwa kuwa uvimbe wangu ulikuwa bado mdogo, alinishauri kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua, nilifanyiwa upasuaji na uvimbe ulitolewa,” anasema Janeth ambaye hiyo ilikuwa ndiyo mimba yake ya kwanza.

 Mwanamke mwingine, Juliana Kasembe anaeleza kuwa, alipata ujauzito kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kujifungua tu, ndipo alipoanza kupata maumivu makali wakati wa hedhi.

“Damu zilikuwa zikinitoka kwa wingi, maumivu makali mno, nilipofanyiwa uchunguzi daktari aligundua uvimbe huo uliokuwa na kilo tano,” anasema.

 Kwa kuwa uvimbe wa Kasembe ulikuwa mkubwa mno, daktari alishauri atolewe kabisa kizazi chake, kwa usalama wa maisha yake.

Watalaamu mbalimbali wa afya ya uzazi wanashauri wanawake kwenda kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara ili kubaini maradhi ambayo mengine yanaweza kutibika au kuzuilika.
Huu sio mwisho kunanyingine pia zinafuata

Monday, June 18, 2012

Bwana alitoa bwana ametwaa jina la Bwana liabudiwe pumzika kwa amani Wille


Kapumzike kwa amani Wille wa Ogunde

Salaamu wasomaji, Moyo naupiga konde,
Sihitaji hata maji, kama viazi mviponde,
Nimejawa na simanzi, Kifo cha kaka Ogunde,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.

Tusimlaumu Mungu, sote tulio waungwana,
Najua tuna uchungu, yowe ni kwamaulana,
Mola angetupa fungu, kifo siwe cha kijana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.

Twasema kasitukizwa, Wille kaenda kijana,
Alipo kuja hatukuulizwa, tulimwona tu mvulana,
Mungu we ndo muweza, kifo leo twakimbizana,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.

Mwaka ule 74 machi saba, Wille ukaiona dunia,
Leo amegonga siku ya saba, ukamtwaa hii dunia,
Tena tarehe kumi na saba, Wille kaiga dunia,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.

Wille ulilia kaka, siku  uliyo iona dunia,
Pinto, Mroki na  Kisaka, sasa zamuyetu kulia,
Wengi wanatafuta kichaka, lini nao watatwaliwa,
Kapumzike kwa amani, Wille mwana wa Ogunde.

Pigo la wana habari, Tanzania na Afrika pia
Hakika kifo ni bahari, hakuna ajuae ilikoanzia,
Kifo ni jemedari, Wille amesha twalia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.

Salamu kawape jalia, wote walo kutangulia,
Mwakiteleko alotulia, na wote wana familia,
Wanahabari tunalia, Wille Ogunde kutangulia,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.

Father Kidevu tamatia, nangoja nami kufuatia,
Siku itapo fikia, hakuna atakae bakia,
Kifo kitendawili, Mola ndie atakae kitegua,
Kapumzike kwa amani, Wile mwana wa Ogunde.