NJOMBE

NJOMBE

Thursday, May 31, 2012

Kuvuja kwa nyaraka za siri za papa

Papa Benedict
Papa Benedict
Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican, amesema kuvuja kwa nyaraka za siri za kiongozi wa kanisa hilo duniani ni kitendo cha kikatili dhidi ya Papa Benedict.
Afisa huyo ambaye ni naibu waziri wa mambo ya nje wa Vatican Angelo Becciu, amesema nyaraka hizo ni pamoja na fikra binafsi, na pia shutuma kali kutoka kwa watu waliomwandikia Papa barua za siri kutokana na nafasi yake ya kipekee.
Nyaraka hizo zinashutumu vitendo vya rushwa na kushindania madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki.
Mwandishi wa BBC mjini Vatican amesema hii ni kashfa kubwa kuliko zote dhidi ya Papa Benedict tangu apate wadhifa wake huo miaka saba iliyopita, na ni tukio lililochafua Kanisa Katoliki nyakati hizi.
Mhudumu mkuu wa Papa, Paolo Gabriele, amekamatwa na tume ya Vatican inachunguza watu wengine ambao wamehusika katika kashfa hiyo.

HIVI NDIVYO ILEVYOPELEKEA TAYLOR KUTUPWA JELA

Kesi dhidi ya Charles Taylor

Charles Taylor
Charles Taylor
Waendesha mashtaka katika kesi ya rais wa zamani wa Liberia Charles Charles Taylor, wameomba adhabu ya kifungo cha miaka 8 jela itolewe dhidi yake.
Bw Taylor alipatikana na hatia ya makosa ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa mjini The Hague, wiki iliyopita.
Katika pendekezo lao lililowasilishwa mbele ya mahakama hiyo maalum inayosikiza kesi ya Seirra Leone, waedesha mashtaka walisema hukumu hiyo inamfaa kutokana na uzito wa uhalifu wa kivita alioufanya bwana Taylor.

makosa

Mahakama hiyo inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa ilimpata bwana Taylor na hatia ya kuuga mkono makundi ya waasi waliofanya mauaji ya kikatili, ubakaji, na kukata viungo vya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi na moja nchini Sierra Leone.
Kiongozi huyo wa zamani wa Liberia anatarajiwa kuhukumiwa Mei 30.
Mahakama hiyo haitoi hukumu ya kifo.

Wednesday, May 30, 2012

Mabalozi wa Syria wafukuzwa Magharibi

Maiti za raia huko Houla
Dola kuu za Magharibi zimetangaza kwamba zinawafukuza mabalozi wa Syria kama hatua ya kulaani mauaji ya zaidi ya raia 100 katika eneo la Houla Ijumaa wiki jana.
Ufaransa, Uingereza, Ujeremani, Italia, Hispania Canada na Australia zimethibitisha kuwafukuza mabalozi hao.
Wengi wa raia waliouawa wakiwemo watoto na wanawake waliuawa kinyama kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Wakaazi wa eneo hilo wamesema wapiganaji wanaounga mkono serikali waliingia makaazi ya raia na kuwaua watu kiholela.Tukio la sasa linajiri wakati Mjumbe maalum wa Kimataifa Koffi Annan amefanya mkutano na Rais Bashar al Assad mjini Damascus.
Waangalizi wa Umoja wa Mataifa ambao walizuru eneo la Taladou wamesema waathiriwa wengi waliuawa kwa kupigwa risasi au kudungwa visu.
Utawala wa Syria umelaumu makundi ya waasi kwa mauaji haya kama hatua ya kuhujumu mpango wa amani na kutoa nafasi kwa dola za magharibi kuendelea kulalamikia utawala huo.
Urusi ambayo imeendelea kutoa silaha kwa utawala wa Syria imesema mauaji yalitekelezwa na pande zote.Koffi Annan ametaja mauaji haya kama ya kinyama na ameonya athari mbaya kufuatia matukio ya sasa.
Kabla ya kukutana na Rais Assad, Bw. Annan amesema serikali ya Syria sharti ionyeshe nia ya kufanikisha majaaliwa ya amani.
Mpango wa amani uliopendekezwa na Koffi Annan kwa Syria ulizitaka pande zote kumaliza mapigano hapo Aprili 12, kutumwa kwa waangalizi wa kimataifa pamoja na wanajeshi wa serikali kuondoka maeneo ya raia.

Charles Taylor asukumwa jela miaka 50

Charles Taylor
Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50m jela na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.
Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.
Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa.
Mwandishi wa BBC aliyeko The Hague Anna Holligan anasema rufaa dhidi ya hukumu hii huenda ikachukua miezi sita. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu.
Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.
Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani.
Charles Taylor amelalamikia upande wa mashtaka kwa kuwatisha mashahidi katika kesi dhidi yake. Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kuwapa silaha waasi na kubadilishana na almasi.
Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kuhudimia kifungo chake nchini Uingereza.

Tuesday, May 29, 2012

HIVI WATANZANIA TUNAKWENDA WAPI?MANA KILICHOTOKEA ZANZIBAR

ZANZIBAR KUMENUKA


Kiongozi wa Jumuiya ya kikundi cha uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed
Baada ya jeshi la polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya wafuasi wa kikundi cha  uamsho kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa kiongozi wao, hali inaendelea kuwa tete na hivi sasa baadhi ya wafuasi hao wameingia mtaani wakishinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo huku jeshi la polisi likilazimika kutumia mabomu kuwatawanya wafuasi hao …..

                            
Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
  
Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini.
                                          
Waanamanaji  hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed walitembea kutoka viwanja vya Lumumba na kupitia barabara ya Kinazini, Mpigaduri, Michenzani Maskani ya CCM Kisonge, kwa Biziredi na kurudi tena viwanja vya Lumumba.
Maandamano hayo walioyaita matembezi ya amani yalifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya wazanzibari ambapo awali kuliandaliwa kongamano kubwa lililoandaliwa na Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa lengo la kuzungumzia mfumo wa elimu Zanzibar.

Akizungumza na maelfu ya wazanzibari kabla ya kuanza maandamano hayo yaliitwa ni matembezi ya amani, Sheikh Farid alisema wazanzibari wana haki kama walivyokuwa na haki wananchi wengine ulimwenguni kote kudai haki yao ndani ya nchi yao....................
                                                 
“Sisi wazanzibari kama wananchi wengine wowote duniani tuna haki ya kikatiba kudai nchi yetu kama walivyodai Sudan ya Kusini, mbona Sudan ya wameweza kujitenda na kupata nchi yao kwa nini sisi kama wazanzibari tusikubaliwe kudai nchi yetu sasa sisi tunampelekea salam katibu mkuu wa umoja wa mataifa kumwambia kuwa wazanzibari sasa wanataka nchi yao” alisisitiza Sheikh Farid huku akiungwa mkono kwa mamia hao kuinua mikono na kusema ndiooooo.
Awali Sheikh Farid alisema salamu hizo anataka zimfikie Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin moon ambaye kwamba wazanzibari wamechoshwa na kuwepo ndani ya Muungano ambao umedumu kwa miaka 48 lakini bado ukiwa na kero nyingi na malalamiko ambayo yanaonekana utatuzi wake ni mdogo na usiowezekana ambapo alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna manufaa yena na wazanzibari.
Katika kuonesha kwamba hawataki tume ya katiba ije kuchukua ya maoni ya katiba mpya Sheikh Farid alisema wanataka kwanza kuamuliwe suala la Muungano kabla ya jambo lolote na kuahidi kwamba wataendelea kufanya makongamano, mihadhara na maandamano kwa kadiri wawezavyo hadi hapo serikali itakaposikia kilio hicho.
“Ujumbe huu tunautoa kwa Ban Kin moon, na kwa ulimwengu mzima lakini pia tunataka rais wetu Dk Shein asikie kilio hiki na Rais Kikwete ambaye yeye ni mtetezi wa haki za binaadamu na pia ni mfuatiliaji wa nchi zinazovunja haki za binaadamu tunataka asikie kilio cha wazanzibari kuwa wanataka nchi yao” alisema.
Alisema juzi wamefanya maombi maalumu ya kumuombea Rais wa Zanzibar lengo likiwa ni kumjaaliwa kheri na awe na maamuzi sahihi juu ya wananchi wa Zanzibar sambamba na kuwaomba Makamu wa Kwanza na makamu wa Pili wa Zanzibar kusikia kilio cha wazanzibari wasiotaka Muungano.
“Tunamuomba Rais wetu Dk Shein, Makamu wa Kwanza Maalim Seif na Makamu wa Pili Balozi Seif kwamba sisi wazanzibari tunahitaji Zanzibar huru, tunahitaji heshima ya nchi yetu na tupo tayari kwa lolote kwa hivyo tunataka salamu hizi na ujumbe huu ukufikieni” alisema Sheikh Farid huku akiungwa mkono na maelfu waliohudhuria katika kongamano hilo ambalo awali liliandaliwa kwa lengo la kuzungumzia masuala la elimu na mfumo wake.
Akiendelea kutoa salamu hizo mara Sheikh Farid alisoma kifungu cha 16 cha katiba na kuwaleza wananchi kwamba haki ya kutembea ni haki ya kila mwananchi ambayo imeainishwa katika katiba na sheria za haki za binaadamu hivyo aliwageukiwa na kuwataka wasimame na kisha kumfuata yeye.
“Haki ya kutembea ni haki ya msingi kwa mujibu wa sheria na kifungu cha 16 kinatupa haki ya kutembea sasa mimi nataka kutembea jeee mpo tayari kutembea na mimi? Alihoji Sheikh huyo huku akijibiwa na umma mkubwa kwamba ndioooo”
Aliongeza kwamba “Tunaanza kutembea na tuone mtu atukamate tunakwenda njia ya kinazini, tunapita michenzani, tunapita barabara ya kwa biziredi na kisha tunarejea hapa hapa kuendelea na kongamano letu kwa amani kabisa mmesikia….akajibiwa ndiooooo”
baada ya kusema hivyo Sheikh Farid alitoa takbir na kuanza kukamatana mikono na viongozi wenzake na huku ummati mkubwa ukiwa umekamatana mikono nyuma na kuanza safari kwa pamoja na kutembea katika barabara ambazo walizitaja awali.
Waandamani hao walikamata mabango yenye maandishi mbali mbali ikiwemo hatutaki muungano, tunataka nchi yetu, zanzibar bila ya muungano inawezekana na wengine kadhalika huku wakitembea njiani na kupiga takbir ambapo walikuwa wakisema Mwenyeenzi Mungu Mkubwa, Mwenyeenzi Mungu Mkubwa sisi hatuna uwezo isipokuwa tunakutegemea wewe Mwenyeenzi Mungu.
Waandamanaji hao walianza kutembea kwa utaratibu maalumu huku magari yakisimama na kuwapisha bila ya kuwepo jeshi la polisi ambapo viongozi wa jumuiya hiyo na wananchi wengine waliongoza utaratibu huo na kutembea katika barabara kwa utaratibu mzuri hadi kumaliza maandamano yao waliyoyaita matembezi ya amani.
Baadae jeshi la polisi lilifika katika eneo ambalo kumefanyika maandamano hayo na kufungua mabango yao ya kuwataka watu kuondoka lakini wakati magari hayo ya polisi matatu yanafika eneo hilo la Kariakoo tayari ummati mkubwa ulikuwa umeshapita katika eneo hilo na hivyo kuingia ndani ya magari yao na kuondoka kwa salama.
Awali akitoa mada katika kongamano hilo, Maalim Abdulhafidh Malelemba alisema sekta ya elimu imekuw aikidorora Zanzibar kutokana na kukandamizwa na mambo ya Muungano ambapo kila mwaka wanafunzi wanapofanya mitihani kufelishwa kwa makusudi huku idadi ya wanafunzi wanaokwenda katika vyuo vikuu wakiwa kidogo kutokana na kufelishwa katika mitihani ambapo husainiwa na baraza la mithani Tanzania (NECTA).
Wakizungumza katika nyakati tofauti katika kongamano hilo, baadhi ya walimu walisema kukosekana kwa baraza la mitihani Zanzibar kusimamia mitihani ya elimu ya juu ndio sababu ya wazanzibari kufelishwa kwa wingi na kushindwa kuingia katika vyuo vikuu kwa kuwa wanafunzi wengi wa Zanzibar hufelishwa.
Walimu hao walitoa ushahidi wa hivi karibuni wa kufelishwa wanafunzi wa kidatu cha nne ambapo walisema lile ni tukio la makusudia lililofanywa na baraza la mitihani ikiwa ni kuwadhoofishwa wanafunzi wa Zanzibar ili wasiendelee katika masomo kwa kuwafelisha.
Habari kwa hisani ya zanzibaryetu.wordpress.com

Makao makuu ya mgombea Misri yavamiwa

Waandamanaji mjini Cairo, Misri
Waandamanaji mjini Cairo,Misri
Waandamanaji nchini Misri wameshambulia makao makuu ya mgombea urais Ahmed Shafiq mjini Cairo.

Bwana Shafiq anashutumiwa kuunga mkono utawala wa zamani wa Bwana Mubarak, madai ambayo yeye na wafuasi wake wanakanusha vikali.
Uvamizi huo umetokea muda mfupi baada ya tume ya uchaguzi kuthibitisha kuwa uchaguzi wa marudio utafanyika mwezi ujao kati ya Bwana Shafiq, ambaye alikuwa waziri mkuu wa zamani katika utawala wa Rais Hosni Mubarak, na Mohamed Mursi wa chama cha Muslim Brotherhood.
Hakuna aliyedai kuhusika na mashambulio hayo.
Mwandishi wa BBC katika eneo la tukio amesema jengo liliwaka moto kidogo, lakini halikupata uharibifu mkubwa.
Waandamanaji wapatao elfu moja wanaopinga matokeo ya uchaguzi huo pia walikusanyika katika medani ya Tahrir.

Sunday, May 27, 2012

Mtumishi wa Papa Benedict akamatwa

 Polisi wa Vatikani wamemshtaki rasmi mtumishi wa Papa Benedict, katika kesi inayohusu wizi wa nyaraka za siri.

Paolo Gabriele na Papa Benedict
Paolo Gabriele - ambaye akitumika kwenye fleti ya papa - amezuwiliwa Vatikani, na ameruhusiwa kuonana na mawakili wawili.
Wakuu wanachunguza vipi, katika miezi ya karibuni, magazeti ya Utaliana yalipata nyaraka ambazo zinaeleza mashindano kati ya wakuu wa kanisa - kisa ambacho kimeanza kuitwa 'Vatileaks'.
Inaarifiwa kuwa Papa Benedict ameshangazwa na kusikitishwa kuwa mtumishi wake mmoja amekamatwa.
Mkuu wa Benki ya Vatikani alitolewa kazini Alkhamisi, kutokana na kashfa hiyo.

Friday, May 25, 2012

Mawakili wa Guantanamo walalamika

Mawakili wa watu watano walioshtakiwa kupanga njama ya mashambulio ya September 11, wamelalamika hadharani kama mahakama ya kijeshi ya Guantanamo Bay ni ya haki kweli.
Mfungwa wa Guantanamo
Washtakiwa, akiwemo Khalid Sheikh Mohammed, anayeshukiwa kupanga mashambulio ya Septemba 11, na vitendo vengine ya ugaidi, walishtakiwa rasmi Jumamosi.
Mawakili wa washtakiwa wanasema mahakama yanazinga ushahidi kuhusu mateso.
Mawakili wa upande wa washtakiwa huko Guantanamo, ni mchanganyiko wa mawakili wa kijeshi na kiraia, ambao walizungumza na waandishi wa habari kwa pamoja.
Walilalamika juu ya kile walichoeleza kuwa "sheria iliyopangwa" na ambayo "imevikwa pazia la siri"; ambayo walisema inawazuwia kuzusha maswala mahakamani kuhusu yale waliyotendewa washtakiwa wakati wanazuwiliwa na Marekani.
Khalid Sheikh Mohammed alitishiwa mara nyingi kuzamishwa, kwenye magereza ya siri ya CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo.
Wakili wake, David Nevin, alisema: " kila kitu kinafanywa ili kuzuwia kesi hii kuwa ya haki".
Kufuatana na kanuni za mahakama, mawakili piya wanakatazwa kuzungumza na wateja wao kuhusu mateso.

Marekani ya kata misaada kwa Pakistan

Kamati ya baraza la senate nchini Marekani, imekata misaada ya kwa serikali ya Pakistan kwa dola milioni thelathini na tatu kila mwaka.
shakil afridi
Marekani inasema hakutendewa haki
Hatua hiyo imechukuliwa kujibu uamuzi wa mahakama moja nchini humo wa kumfunga daktari ambaye alisaida Idara ya Ujasusi CIA, kumnasa Osama Bin Laden.
Shakil Afridi alihukumiwa kifungo cha miaka thelathini na tatu baada ya kupatikana na hatia ya uhaini.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton, amesema dakatari huyo kamwe hakufanyiwa haki na haikubaliki.
Mwaka jana, kikosi maalum cha jeshi la Marekani kilimuua Osama bin Laden, mjini Abbottabad Pakistan, alipokuwa amejificha.
Mauaji ya Osama, yalizua tofauti kati Marekani na Pakistan, nchi ambazo zimekuwa na ushirikiano wa karibu hasaa katika juhudi za kukabiliana na ugaidi.
Pakistan ilichukulia operesheni hiyo ya kumsaka Osama bila idhini yake kama kuishushia hadhi yake ya kitaifa.

Thursday, May 24, 2012

Nzi zaidi ya wawili wasipige kelele China

Serikali ya China imetangaza kuwa choo chochote cha umma hakitakiwi kuwa na nzi zaidi ya wawili wanaoruka kwa wakati wowote.
Hiyo ni moja kati ya mfululizo wa viwango vipya vilivyowekwa na mamlaka hiyo kujaribu kufanya bora maeneo ya umma mjini humo.
Malengo mengine yanahusu usafi, matumizi ya vifaa na mafunzo kwa watendaji.
Mwandishi wa BBC aliyeko Beijing anasema sheria hizo mpya zimelenga watu wanaoishi katika maeneo ya zamani ya mji huo.

FLAVIANA MATATA AKABIDHI MSAADA WA MABOYA



Flaviana akionesha moja ya maboya yenye nembo ya foundation yake aliyokabidhi katika kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya MV Bukoba ikiwa ni kampeni yake ya kupunguza ajari za majini hapa nchini.

Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori kulia ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service,Kapten Obadia Nkongoki. Igoma jijini Mwanza,

Flaviana Matata akishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo yaliyopi Igoma jijini Mwanza, katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza pia mama yake mzazi.

flaviana na wageni wakiweka  mashada kwenye makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo Igoma Mwanza

Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo

ICC : Waafrika waonyeshe ushujaa

Mwendesha mashtaka mkuu mpya katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Fatou Bensouda, amesema wababe wa kivita wanawatisha viongozi wanaojaribu kuwatia mbaroni.
Bi Bensouda ametoa wito kwa viongozi wa Afrika wasikubali kutishwa na viongozi kama vile jenerali muasi Bosco Ntaganda.
Bosco Ntaganda
wababe wanawatisha viongozi Afrika
Jenerali Ntaganda anakabiliwa na tuhuma za uhalifu wa kivita na kwa kuwasajili watoto vitani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Akizungumza na BBC, Bi Bensouda amesema kuwa wababe hao wanawatisha viongozi kuwa ikiwa hawata legeza kasi ya kuwasaka basi wataendelea kuwaua watu.
Katika siku za hivi karibuni, mamia ya watu wameuawa huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wanajeshi wanamsaka Jenerali Ntaganda.
Mwezi March mwaka huu, mahakama ya ICC ilimpata mshirika wake mkuu wa Jenerali Ntaganda, Thomas Lubanga na hatia ya kutekeleza uhalifu wa kivita mashariki mwa Congo.
Bi Bensouda ambaye ni wakili kutoka Gambia ni mwaafrika wa kwanza kuteuliwa kama mwendesha mashtaka katika mahakama hiyo.
Ataanza kutekeleza majukumu yake mwezi ujao baada ya kustaafu kwa Louis Moreno Ocampo.

Tuesday, May 22, 2012

Mhemko kwa vijana

TUMEKUTANA tena kwenye kona yetu tuipendayo ya mahaba ili kujuzana machache kuhusiana na maisha ya kila siku.
Leo nataka kuzungumzia kichaa cha mapenzi kwa wanafunzi, hii imetokea baada ya kupokea simu nyingi za wanafunzi waliojiingiza kwenye mapenzi na kusahau kuwa wapo katika masomo.

Najua kila mmoja amepitia hatua hii ambayo mwanadamu huanza kujengeka kimuhemko ambayo humuandaa kwa ajili ya kufanya tendo la ngono. Kila mwanaume anapopevuka huanza kuwa na tamaa ya kufanya ngono hasa anapoziona sehemu zinazomshawishi kufanya ngono kwa mwanamke.
Mwanaume akiishapevuka akiziona sehemu za mwanamke kama matiti mapaja mgongo ukiwa wazi makalio yaliyovimba. Na baadhi ya sehemu za mwili wa mwanamke ambazo zina kishawishi cha ngono kwa asilimia 90, pia humshawishi kutamani ngono.

Kwa msichana naye akishavunja ungo huanza kupata mihemko hata mwenyewe akijishika baadhi ya sehemu uhisi kuitaji kitu fulani ambacho si kingine, ni kufanya ngono. Msichana anapojisugua sehemu za siri au kwenye matiti ambayo huwa na maumivu ya mbali ukiyakanda hupunguza muwasho.

Vitu hivi vimekuwa vikiwafanya wasichana wengi wasio na uvumilivu kuanza kutafuta mtu wa kumpunguzia vitu vinavyomsumbua au mwanaume kutafuta msichana kwa ajili ya kufanya naye mapenzi.
Katika kufanya uchunguzi wangu wa kina nimegundua pamoja na hali hiyo vipi vitu vinavyo waingiza vijana kwenye ngono kabla ya wakati wake, kimoja ni tamaa ya kutaka akiwa shuleni naye awe na baadhi ya vitu vilivyopo nje ya uwezo wake ambavyo humfanya ajirahisi kwa kuutoa mwili wake.

Hata wanaume ambao kwa sasa wamekuwa wakisakwa na Mama Sukari kwa kuwahonga na kufanya nao ngono kwa kugeuzwa chombo cha starehe.
Pia wapo wanaoingia katika mtandao huu kwa kufuata mkumbo kwa kupenda kusikiliza simulizi za ngono kwa watu wenye tabia hizo naye kujaribu kutokana na kusikia sifa ya kitu kile bila kujua muda wake bado. Wengine kuangalia picha za ngono ambazo humfanya apate muhemko na kujikuta akimtafuta wa kumtuliza muhemko wake.

Lakini vitu hivi vinawezekana kabisa kuvishinda, kwanza lazima ujijue una umri gani, nini madhara ya kufanya mapenzi katika umri mdogo. Pia kujua nini malengo yako katika maisha ngono na elimu, nini kitakacho kubeba hata kama wazazi wako wamekufa.

Tatu, kuijua thamani ya usichana wako au uvulana wako kwa kujitunza ili siku moja ufikie malengo yako. Kwa mwanamke ambaye ndiye aliye katika kundi baya la kuathirika kama ataendekeza ngono, jivunie kukutwa bado msichana japo kwa sasa ni jambo gumu kama kuliona jua saa mbili usiku. Kumbuka kosa lako moja linaweza kukuharibia mfumo mzima wa maisha.
Jiepusheni na vitendo ambavyo mnaamini ndivyo vitakavyo kufanyeni muonekane mnakwenda na wakati. Kufanya ngono katika umri mdogo kuna hasara nyingi mojawapo kuunguza mayai ambayo huungua na kukufanya uwe tasa.

Pia kuvuruga ndoto zako ambazo zinatakiwa uvumilivu na kujiepusha na chochote ambacho unakiona kitakupotosha na kukuvurugia malengo yako. Kama utayafuata haya machache, hakika utashinda na kufikia ulichopanga.

WAHUKUMIWA KIFO KWA KUENDESHA TOVUTI YA NGONO

 
Wanaume wawili wa nchini Iran wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa kutengeneza na kuendesha tovuti ya picha na video za ngono. Mahakama za nchini Iran zimewahukumu watu wawili adhabu ya kifo kwa kuendesha tovuti ya ngono, shirika la habari la Iran, IRNA limeripoti.

"Watu wawili waliokuwa wakisimamia tovuti mbili tofauti za ngono wamehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama mbili tofauti, hukumu zao zimetumwa mahakama kuu ili zithibitishwe kabla ya kutekelezwa", lilisema shirika hilo la habari bila ya kutaja majina ya watu hao.

Mwezi disemba mwaka jana, serikali ya Canada ilielezea kusikitishwa kwake na raia wa Canada mwenye asili ya Iran kuhukumiwa kunyongwa kwa kutengeneza tovuti ya ngono.

Raia huyo wa Canada, Saeed Malekpour, 35, alipatikana na hatia ya kutengeneza na kuisimamia tovuti ya ngono ambalo ni kosa la kwenda kinyume na maadili ya kiislamu.

Malekpour alitiwa mbaroni nchini Iran mwaka 2008 baada ya kurudi nchini humo akitokea Canada ili kumuuguza baba yake ambaye alikuwa mgonjwa.

Alihukumiwa adhabu ya kifo mwezi disemba mwaka jana.

mahusiano, tamaduni, maumivu, hisia na ashiki

Naam katika mahusiano tamaduni na miiko mbali mbali huingilia kati. Vijana hukutana na vizingiti zaidi katika hili. Dini za kigeni zinamaoni yake katika hili wakati tamaduni na dini za kiasili nazo huwa na mitizamo yake.
Tamaduni nyingi za kiafrika zilipinga sana upatikanaji wa Mimba kwa binti kabla ya kuoelewa. Katika jamii za wahaya kwa mfano, binti aliyepata mimba katika kipindi hicho alikabiliwa na hadhabu kali ya kifo cha kikatili. Mchumba alitafutwa na kukubaliana kati ya wazazi husika na wanandoa kukutanishwa baadae
Dini nyingi za kigeni kama vile ukristo na uisilamu nazo zina tamadmuni zake kwa wachumba na wanandoa. Wale waliobahatika kupata mimba kabla ya kufungishwa ndoa na kiongozi wa dini, hupewa adhabu Fulani Fulani za kiimani kama kutoshiriki kiitwacho chakula cha bwana au hata kutengwa mbali kabisa na nyumba za ibada
Katika mahusiano ya kisasa vijana nao huja na mambo yao. Huu utumika kama wakati wa kujifunza mapenzi yenye ashiki na hisia kali. Hapa wengi hawaambiliki na hujiona wamefika na wanajua kila kitu katika massuala ya mahusiano. Kumbuka tunapokua na kujijua na kutoka nje ya nyumba za wazazi/walezi wetu, jambo kubwa huwa ni mahusiano ya kimapenzi a watu wa jinsia tofauti na za kwetu.
Huwa ni kipindi kigumu cha kujifunza masmuala haya magumu bila kufata utaratibu wowote namwisho huwa ni maumivu ya kuachana na Yule ambaye mtu aliamini ni wa milele. Hata hivyo maumivu haya huwa sio halisi kwani huko mbeleni huja kukutana na wapenzi wengine ambao hupendani sana kuliko wale wa zamani. Kuna wanaozunguka na kurudiana na wale wa zamani
Wazazi wengi hawawasaidii vijana wao katika masuala ya mahusiano isipokuwa wengi huwaingilia na kutaka kuwa tafutia wenza au hata kuwapiga mkwara juu ya mambo haya.
Ndoa hunukia kwa mbali

Tetemeko la ardhi Italia

Maelfu ya watu walioachwa bila makao kufuatia tetemeko kubwa la ardhi Kaskazini mwa Italia watalazimika kulala kwenye mahema kufuatia wasiwasi wa kuzuka tetemeko jingine.
Watu sita walifariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika tetemeko hilo la ardhi lililotokea Jumapili.
Serikali imetoa mahema mengi kwa wananchi hao walioathirika na tetemeko la ardhi ingawa wengine wameamua kulala katika magari yao.
Wataalamu walisema tetemeko hilo lilifikia kipimo ya Richa 6.
Waziri Mkuu wa Italia, Mario Monti, atakatiza mkutano wake na viongozi wenzake wa NATO unaoendelea Marekani kwa ajili ya hali ilivyo nchini mwake.

Sunday, May 20, 2012

Malawi kubatilisha sheria ya mapenzi

Rais Joyce Banda

Rais wa Malawi,Joyce Banda amesema kuwa anataka nchi hiyo ibatilishe sheria inayoharamisha ndoa za jinsia moja na kuifanya nchi ya kwanza ya kiafrika kufanya hivyo tangu mwaka 1994.
Wananume wawili raia wa nchi hiyo walihukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani mwaka 2010 baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana.
Baadhi ya viongozi wa nchi za magharibi, hivi karibuni wametishia kusitisha msaada kwa nchi za kiafrika ambazo hazitatambua haki za mashoga.
Rais Banda alichukua hatamu za uongozi mwezi jana kutoka kwa mtangulizi wake, Bingu wa Mutharika, aliyeaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo.
Hadi sasa rais huyo amegeuza baadhi ya sera zake ikiwemo kushusha thamani ya sarafau ya nchi kwa lengo la kuanza kupata msaada .
Wafadhili wengi walisitisha msaada chini ya utawala wa Mutharika, wakimtuhumu kwa uongozi duni pamoja na ukandamizaji.
Katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge la anchi Banda alisema kuwa baadhi ya sheria zilizopitishwa na bunge, zitafutiliwa mbali kama hatua ya dharura ikiwemo sheria zinazopinga vitendo visivyo vya kawaida.
Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani mjini Blantyre, anasema kuwa rais anaungwa mkono na wabunge wengi, na kwa hivyo ataweza kuwashawishi wabunge kubatilisha sheria hiyo.

Friday, May 18, 2012

Baa la njaa la sambaa nchini Niger

Hata baada ya kutahadharishwa kwa miezi kadhaa kwamba baa la njaa linakuja ,sasa Niger inakumbwa na kiwango kikubwa cha utapiamlo.
Akina mama na watoto wao wakisubiri chakula nchini NigeR

Shirika la Save the Children katika taarifa yake limesema hali huko Niger inazidi kuwa mbaya zaidi.
Shirika hilo linasema kuwa watu zaidi ya milioni sita wanakabiliwa na njaa. Na katika eneo zima la Sahel karibu watu milioni 18 wanakabiliwa na tishio la njaa.
Taarifa hiyo inasema kuwa idadi ya watoto wanaohitaji matibabu kutoka na maradhi yanayotokana na ukosefu wa chakula imefikia kiwango cha kutisha.
Onyo hilo la Save the Children linakuja wakati mataifa tajiri zaidi duniani G8 yanakutana kujadili hali ya chakula duniani.
Shirika hilo linasema kuwa kwa wakati huu wanafanya mipango ya dharura kukabiliana na hali hiyo.
Tangu mwaka jana wakati mvua ya masika iliyotarajiwa haikunyesha vizuri jamii ya kimataifa ilianza kutoa ilani kuwa hali huenda ikawa mbaya katika eneo la Sahel na hasa Niger.
Kijumla asilimia 25 ya watoto wote duniani wanakabiliwa na matatizo ya utapiamlo. Wengi ya watoto hao wako bara la Afrika.
Sasa shirika la Save the Children limeomba vingozi wa nchi za G8 wanaokutana Marekani washughulikie hali hiyo.

Kikosi cha Ecowas chawasili Guinea

Mkutano wa viongozi ECOWAS

Kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa usalama kutoka Afrika Magharibi, kimewasili nchini Guinea-Bissau kusaidia kuleta uthabiti nchini humo. Hii ni baada ya tukio la mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi jana.
Takriban wanajeshi 70 wote kutoka Burkina Faso ni sehemu ya vikosi vya usalama vilivyopangiwa kufika nchini humo na jumuiya ya Ecowas.
Takriban wanajeshi 600 wanatarajiwa kufika nchini humo katika siku chache zijazo kulingana na taarifa iliyotolewa na Ecowas.
Guinea-Bissau ilikuwa imesalia na wiki kadhaa kuandaa duru ya pili ya uchaguzi wa urais, wakati jeshi lilipofanya mapinduzi.
Wanajeshi hao waliwasili siku moja na waziri mkuu wa serikali ya mpito, Rui Duarte Barros, aliyetawazwa baada ya mapinduzi.
Viongozi wa mapinduzi hayo, walikubaliana hapo awali kuhusu kipindi cha mwaka mmoja wa ukabidhi wa mamlaka, kama ilivyotakiwa na jumuiya ya Ecowas.
Vikosi hivyo vya usalama, vinapelekwa nchini humo kuweza kusaidiana na wanajeshi kutoka Angola na vile vile kuweza kusaidia harakati za kurejesha utawala wa kikatiba.

Thursday, May 17, 2012

Bosco Ntaganda aingiza watoto jeshini

Jenerali mtoro Bosco Ntaganda, ambae anasakwa na mahakama ya kimatiafa ya jinai -ICC bado anajumuisha watoto katika jeshi lake.
Watoto wapiganaji wa Bosco Ntaganda

Shirika la Human Rights Watch (HRW) linasema kuwa katika mwezi uliopita watoto wapatao 150 wa kike na wakiume wamejumuisha jeshini.
Watoto hao wote wanatoka katika eno la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
wale ambao wamefaulu kutoroka wanaelezea kuwa wengi wao walichukuliwa toka shuleni na vijijini na kuamrishwa kwa bunduki kiunga na wapiganaji wa Bosco Ntaganda.
Mahakama ya ICC mwaka wa 2006 iliamuru Jenerali Bosco Ntaganda akamatwe na kushitakiwa.
Sasa Shirika la Human Rights Watch lenye makao yake New York, Marekani limesema kuwa watoto wanaolazimishwa kuingia jeshini ni wa kati ya umri wa miaka 12 hadi 20.
Uchunguzi wa Human Rights watch unasema kuwa shughuli hiyo ya kuwakamata watoto na kuwaingiza jeshini lilianza kutekelezwa pale wafuasi wa Bosco Ntaganda kuasi jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wafuasi hao walikuwa chini ya kikosi cha Ntaganda cha CNDP ambao walijumuishwa katka jeshi la Congo.
Lakini kufikia sasa Jenerali Ntaganda amekanusha kuchochea maasi katika jeshi la Jamhuri ya Congo.
Inaaminika kuwa Jenerali Bosco Ntaganda anajificha katika mbuga ya Virunga , sehemu iliyo maarufu sana kwa sokwe.
Hata hivyo serikali ya Congo imeahidi kumsalimisha Bosco Ntaganda katika mahakama ya kimatiafa ya jinai -ICC -iwapo itamtia nguvuni.

Wednesday, May 16, 2012

Hoteli yashambuliwa na magaidi Mombasa

Hoteli moja maarufu visiwani Mombasa imeshambuliwa kwa maguruneti na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Magaidi washambulia hoteli kando ya mahali hapa

Hoteli hiyo ,Bella Vista Restaurant,ni maarufu sana kwa watalii na wenyeji na iko kando ya barabara kuu itokayo bandari ya Mombasa.
Mkuu wa kitengo cha polisi wa jinai mjini Mombasa Bwana Ambrose Munyasya aliambia BBC kuwa watu watano walijeruhiwa vibaya katika kisa hicho.
Polisi wanasema kuwa uchunguzi wao wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na milipuko mitatu katika klabu hicho cha Bella Vista Restaurant.
Milipuko hiyo ilisababisha uharibifu wa magari sita yaliokuwa yameegeshwa kando ya hoteli hiyo.
Mkuu huyo wa polisi alisema kufikia sasa wanahofia kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na magaidi.
Inadaiwa kuwa watu wawili walikwenda katika Klabu hicho wakitaka kuruhusiwa kuingia.
Lakini walipotakiwa kupekeliwa na maaskari wa hoteli hiyo walikataa na ndipo wakarusha maguruneti hayo.
Walioshuhudia mkasa huo wanasema kuwa magaidi hao walifyatua risasi ovyo ovyo wakati walipokuwa wakitoroka.
Hata hivyo polisi wanasema hawaja mkamata mtu yeyote kutokana na kisa hicho.

Tuesday, May 15, 2012

Rais mpya wa Ufarnsa Hollande aapishwa


Rais Francois Hollande

Francois Hollande ametawazwa kama rais mpya wa Ufaransa, na kumfanya kuwa rais wa kwanza wa kisosholisti kuapishwa katika miaka kumi na saba.
Bwana Hollande alisema kuwa anafahamu vyema changamoto ambazo Ufaransa inakabiliana nazo ikiwemo, madeni na uchumi unaojikokota.
Baadaye hii leo rais Hollande atamteua waziri mkuu na kisha kwenda nchini Ujerumani kwa mazungumzo na Chansella Angela Merkel.
Bwana Hollande angependa kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mpango wa Ujerumani wa kutafuta suluhu kwa mgogoro wa kiuchumi unaokumba bara la Ulaya.
Hapo jana thamani ya Euro ilishuka masoko ya hisa nayo yakishuka huku hali ya kisiasa nchini Ugiriki ikiendelea kuwa tete.
Mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa fedha wa ulaya, Jean-Claude Juncker, alisisitiza hapo jana kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Ugiriki inasalia katika muungano wa Ulaya.
Bwana Juncker anasubiri kuundwa haraka kwa serikali mpya ya Ugiriki siku tisa baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Lakini pia alionya kuwa Ugiriki haina budi ila kuendelea na juhudi muhimu zilizoanzishwa kuweza kuokoa uchumi wake licha ya sera hizo kupingwa na wapiga kura wengi.
Wengi mjini Berlin wanamshuku bwana Hollande. Hawapendi kuwa wakati wa kampeini zake alionekana kupinga mipango ya kupunguza matumizi ya serikali kwa lengo la kuokoa uchumi pamoja na kuukuza.
Wengi walitafsiri hilo kama juhudi za Ufaransa kutaka kuongoza tena muungano wa Ulaya.

Raia wa Sudan Kusini wafika nyumbani

Raia wa Sudan Kusini

Ndege ya kwanza iliyowabeba wakimbizi waliokwama kwa miezi kadhaa nchini Sudan imewasili mjini Juba Sudan Kusini. Raia hao wapatao 164 wanatarajia kusafirishwa kwa barabara hadi katika kambi mpya wakisubiri kutafutiwa jamaa zao.
Kundi hili ni la raia laki tano ambao walipoteza uraia wao baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake mwaka jana. Nchi hizo nusura kuingia vitani kutokana na mzozo wa raslimali za mafuta na mipaka.
Raia waliofika leo wamekuwa katika jimbo la Nile ambapo walipewa hadi Mei 20 kuamua ikiwa watachukua uraia wa Sudan au kurejea Sudan Kusini.
Maafisa wa Sudan wamepinga hatua ya kuwasafirisha raia hao kwa wingi kwa hofu ya usalama.
Punde baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake maelfu ya raia wake waliofanya kazi katika iliyokuwa serikali ya taifa moja la Sudan waliachishwa kazi na utawala wa Khartoum.
Kuna kambi maalum mjini Juba ya raia hao kabla ya kutafuta maeneo yao ya asilia.
Maelfu ya raia wa Sudan Kusini walihamia Kaskazini wakati wa vita na kutafuta ajira.

Sunday, May 13, 2012

Honi kali zitatumiwa kwenye Olimpiki


Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa chombo kama honi, kitatumiwa kama silaha mjini London wakati wa michezo ya Olimpiki.
Mazoezi ya ulinzi kwenye Mto Thames, London

Kelele za chombo hicho zinaweza kuvuma kwa masafa marefu na kuumiza masikio.
Chombo hicho kimetumiwa sehemu kadha za dunia kutawanya mkusanyiko wa watu; na kinatengenezwa Marekani ambako kimearifiwa kuharibu masikio daima.
Lakini Wizara ya Ulinzi inasema kitatumiwa tu kwenye vipaza sauti kuzuwia misafara kwenye Mto Thames; na ni sehemu ya zana kadha zitazotumiwa kuhakikisha usalama wa Olimpiki.
Chombo hicho kinatumiwa kupambana na maharamia wa Somalia.

Gaidi asakwa Kenya


Maafisa wa polisi nchini Kenya wamesema wanamsaka raia mmoja kutoka Ujerumani anayetuhumiwa kuhusika na mashambulio ya hivi karibuni nchini humo.
Raia wa Uingereza aliyefikishwa mahakamani Mombasa kwa tuhuma za ugaidi
Mtu huyo kwa jina Ahmed Khaled Mueller anadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la al- Shabaab.
Kenya imeshambuliwa mara kadhaa tangu majeshi yake kuingia nchini Somalia kuwasaka wapiganaji wa Al shabaab.
Mmwandishi wa BBC mjini Nairobi anaarifu kuwa maafisa wa polisi nchini Kenya wametoa picha ya raia huyo kwa jina la Ahmed Khaled Mueller na kusema ana uhusiano wa karibu na kundi la al- Shabaab.
Japo maafisa wa polisi hawasemi ni lini aliingia nchini Kenya, wanasema aliingia nchini kinyume cha sheria na kwamba amejihami.
Aidha, polisi imesema mtu huyo anadaiwa kuhusika na mashabulizi ya hivi karibuni nchini.
Hii sio mara ya kwanza kwa polisi kutoa picha ya mtu anayeshukiwa kuhusika na kupanga mashambulizi nchini Kenya.
Mapema mwaka huu, polisi ilitoa picha ya raia mmoja wa Uingereza ambaye anadaiwa kuhusika na kupanga mashambulizi pwani mwa Kenya, na wiki iliyopita maafisa wa polisi walichapisha picha nyengine ya mtu anayedaiwa kuhusika na shambulio la guruneti la mwezi wa Aprili, katika kanisa moja mjini Nairobi, mbapo watu wawili waliuwawa na zaidi ya 15 kujeruhiwa.

Friday, May 11, 2012

Kukosa mwangaza wa jua hatari

Utafiti uliofanywa hivi karibuni juu ya kupungua kwa nuru ya macho kumeonyesha kua hadi asili mia 90 ya wanafunzi wanaohitimu masomo huathiriwa na tatizo la kuona

Jua muhimu kwa macho Macho yahitaji kutunzwa vizuri.

Wataalamu wanasema kua ongezeko hili la kutisha juu ya tatizo la macho limesababishwa na wanafunzi kusoma sana na kukosa mwangaza wa jua.
Wataalamu wameliambia jarida la kiafya la Lancet kua mmoja kati ya wanafunzi watano anaweza kukabiliwa na mapungufu ya macho na hata kupofuka macho.
Kulingana na Professor Ian Morgan wa Chuo Kikuu cha Australian National University, aliyeongoza utafiti huu,asili miaka 20-30% waliwahi kua watu wa kawaida wasiokua na matatizo huko Bara Asia kusini mashariki.
Idadi ya wagonjwa wa maradhi haya ya macho imepanda kutoka asili mia 20 waliopungukiwa na nuru ya kuona na kuzidi asili mia 80 na kuelekea asili mia 90 miongoni mwa vijana na watakapoingia umri wa watu wazima maradhi hayo yataenea zaidi miongoni mwa jamii nzima.Bila shaka hili ni tatizo kubwa la kiafya.
Wataalamu wa masuala ya macho wanasema kua una mapungufu ya macho ikiwa unachotazama hukiona vizuri kutoka umbali wa mita 2 yaani futi sita.
Tatizo hili husababishwa na kurefuka kwa mboni ambako hutokea mtu akiwa na umri mdogo.
Kwa mujibu wa utafiti, tatizo hili husababishwa na masuala kadhaa- kusoma kwa kupindukia na kukosa mwangaza wa jua.
Professor Morgan anasema kua watoto wengi huko Asia ya kusini mashariki hutumia mda mrefu wakisoma shuleni na baadaye kudurusu nyumbani. Hili huwazidishia shinikizo kwenye macho yao, lakini wangeweza kutoka nje kwa mda wa saa mbili hadi tatu ili kurekebisha mapungufu na umuhimu wa mwqangaza inawezekana kulinda afya ya macho yao.
Jicho
Jicho bandia

Wataalamu wana imani kua aina ya kemikali ijulikanayo kama dopamine ambayo huenda ina mchango katika hili. Kukaaa katika mwangaza wa nje huongeza viwango vya kemikali hii ya dopamine ndani ya jicho na hilo huzuia kurefuka kwa mboni.
Nyenzo za kitamaduni nazo zinachangia. Watoto wengi wa Bara Asia kusini mashariki, hupenda sana kupumzika nyakati za adhuhuri. Kulingana na Professor Morgan tabia hii huwakosesha mwangaza wa jua la mchana ambao ni muhimu katika kuzuia maradhi haya ya kupungua kwa nuru ya macho, myopia.
Pamoja na shinikizo za kutaka kufanikiwa katika elimu na kupangiwa siku kwa watoto, mda ambao mtoto hukaa nje kunufaika kwa mwangaza wa jua unapunguwa. Wasiwasi mkubwa ni idadi ya wanafunzi ambao wanazidi kupatwa na maradhi ya myopia.
Kwa miongo kadhaa wataalamu wameamini kua kuna uhusiano mkubwa wa jeni au urithi kutoka kwa wazazi kuhusiana na hali hii ya ugonjwa wa macho.Ikiaminika kua watu kutoka Uchina,Japan,Korea na nchi nyingine wanaweza kukumbwa na myopia.Lakini utafiti huu unaonyesha mtazamo tofauti.
Hili litahitaji utafiti zaidi lakini la muhimu ni kuwatia moyo watoto watumie mda mwingi nje ya nyumba jua linapochomoza. Huenda likapunguza madhara ya macho.

Je Umoja wa Mataifa umeshindwa Syria

Mapigano yanaendelea Syria

Tume ya UN SYRIA
Tume ya UN Syria
Idadi ya watu waliofariki kufuatia mashambulio ya bomu inazidi kuzua masuali juu ya jukumu la waangalizi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo.
Jukumu lao ni kusimamia na kuona kua mapigano yanasimamishwa. Lakini ingawa hilo limetimizwa katika baadhi ya maeneo ukweli ni kwamba mapigano bado hayajamalizika.
Mapigano bado yapo
Mapigano bado yapo
Na hili linazua suali nyeti juu ya umuhimu na uwajibikaji wa tume ya Umoja wa Mataifa.
Imani iliyokuepo ilikua kwamba endapo watatumwa wasimamizi kutoka nje huenda wakasaidia kushawishi wakuu wa serikali kutimiza ahadi zao za kukomesha ghasia.
Lakini tangu mwanzo, kuwepo kwa wasimamizi hawa kulizua suali jipya kuu: Endapo mashambulizi dhidi ya raia yataendelea Je nini kitafuata?
Umoja wa Mataifa utachukua hatua gani zaidi ya hio? Na ni mazingira gani yatafanya Umoja wa Mataifa ukubali kua mpango wake umeshindwa?
Tatizo ni kua hakukuepo mpango mbadala endapo huu utashindwa.
Mpango pekee ambao Jumuia ya kimataifa uliweza kukubaliana kwa sauti moja ni huu wa kutuma wasimamizi. Pamoja na maneno mazuri ya kuvutia ya njia za kupitia kunusuru maisha bila bughdha au njia nyingine za upatanishi, hakuna yeyote aliyetaka kuhusika moja kwa moja na matatzio ya Syria.
Makundi yananufaika kwa ghasia
Makundi yananufaika kwa ghasia
Ingawaje kuhusika kupitia makundi ni njia nyingine. Bila shaka silaha zimekua zikitiririshwa kutoka nje ya nchi. Kukiwa na makundi ndani ya nchi ambayo yanafurahia kuzusha fujo kwa manufaa yao.
Mgogoro wa Syria umeanza kujenga sura ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Na Umoja wa Mataifa haujajiweka tayari kutangaza ujumbe wa tume yake umeshindwa kwa sababu hakuna yeyote anayyeweza kujibu suali - Nini kitafanyika sasa.

Waasi washambulia gereza nchini Nigeria

  Watu wenye silaha wamevamia gereza nchini Nigeria, katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno, na kuua walinzi wawili wa gereza hilo na kuwafungulia wafungwa.

Polisi wamesema wapiganaji kutoka kikundi la Kiislam la Boko Haram, kwanza walikishambulia kituo cha polisi katika mji wa Banki, kabla ya kwenda kuvamia gereza karibu na kijiji cha Kunshi.
Msemaji wa polisi amesema wamewakamata watu 23.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo lakini kikundi cha Boko Haram kimelaumiwa kwa kuhusika na matukio ya aina hii kaskazini mwa Nigeria.

Wednesday, May 9, 2012

JAMANI HIVI HATUJUI MAZINGIRA YETU : Ubaya na Uzuri wake…

Jamii zetu zinazoendelea zinahitaji sana Elimu.  Elimu itakayotusaidia kupambana na maadui kama : kutojua kupanga muda (Time Management) tatizo linalotufanya tuchelewe, tusiwe na mpangilio wa maisha ; halafu, kutoyajali mazingira yetu (vyoo vichafu na kutupa taka ovyo).Uchafu wa mazingira DarWataalamu wameshatuonya kuwa makaratasi ya plastiki tunayoyaacha kiholela kila mahali (yenye madawa hatari) yanaharibu rutuba na uhai ; yatakaa ardhini miaka 500 !!!
Bougainvillea -Silversands
Si mbali  na palipotupwa plastiki hizi pana hoteli hii marufu na nzuri ya Silversands ambapo watalii na wenye uwezo wanakaribishwa kwa maua  mazuri yenye asili ya Kimarekani yaitwayo Bougainvillea.  Ikiwa tunaweza kuyapamba mazingira ki-azizi,  hatushindwi kuyaacha safi…
Madafu
Nilishangazwa nilipoelezwa na muuza madafu mmoja Dar kuwa kinywaji (chakula) hicho muhimu siku hizi hakipatikani kirahisi. “Minazi inakatwa ovyo…” akalalama.
Minazi ya Dole
Nilipokuwa kitongoji hiki cha Dole, Unguja, nikawa nawaza lile balaa la minazi kukatwa bandari  ya Dari Salama. Minazi imesimama dede mithili ya twiga au mbuni malishoni.  Je, itadumu?
Matunda ya Afrika  Sehemu nyingi Zanzibar bado vyakula asilia vinathaminiwa. Cheki  matunda, mboga na makulaji : mjini na vijijini. Ama kweli inatia moyo…maana chakula ni utamaduni wa nchi; kama huna au unaiga (huthamini chako) huna jicho…
Chakula cha Zanzibar
Huku unakula huku unafikiria namna ambavyo bado wananchi wengi tunatupa chupa za maji ovyo nje; tunavyofungia bado vyakula vyetu kwa magazeti badala ya mifuko isiyokuwa na sumu na madawa…
Chupa ya maji- uchafu
Kinamasi hiki kimejaza si tu plastiki  na dawa zenye sumu bali pia wadudu kama mbu. Kila anayeweza (kutumia mtandao na kompyuta ni uwezo na nafasi) kuelemisha watu wetu ajitahidi na kujaribu…maana hizi blogu hazisomwi na wengi.
Silversands-2
Hapa natia tizi katika moja ya bichi za Dar…ukweli si rahisi siku hizi kupata ufukwe msafi mjini hapa. Na hata zile safi baada ya kuogelea unahisi macho yakikuwasha washa. Watalaam wameonya kuhusu kutupa taka ovyo baharini, kunya (na kukojoa) ovyo ufukweni, kuchafua michanga kwa vyupa vya vinywaji tunapostarehe kando ya bahari mama ya Hindi.
Jani la Mnazi
Pwani ya Dar